Je, Mungu anajua utakwenda motoni au mbinguni?

Anajua mwisho wa matendo yangu??

Kwahiyo ananihukumu vipi sasa kama alijua fika nitaenda motoni? Na ndie alienipangia hilo?
Vishu Mtata mbona unakuwa mtata😂😂

Hajakupangia ndio maana tukashushiwa manabii na mitume watuambie lipi jema na lipi ovu

Sasa tukiamua kufanya mema tutaingia peponi na maovu motoni vile vile

Kwa maana nyingine na kama vile Mungu amekupa hoja ya kujitathimini mwenyewe ili siku ya hukumu usiwe na kisingizio

Atakwambia walikuja mitume na manabii lkn hukuwafuata wala kuwasikiliza ona sasa huna wa kumlaumu pambana na hali yako

Kama yeye ndio angatuhukumu basi hakukuwa na haja ya kuwaleta mitume ambao ingekuwa kazi bure kama tayar hakuna uhuru wa kufanya mema au mabaya

Kwa maana nyingine jichunguze mwenyewe je mpaka sasa unaishi katika misingi gani
 
Kama Mungu anajua mwisho wako, Je wewe unaweza kwenda kinyume na vile anavyojua Mungu?

Kama Mungu anajua wewe utakwenda jehanamu, Wewe ukabadilika ukachagua kutenda mema tu, Je bado utakwenda jehanamu?

Kama Mungu anajua destiny ya kila mtu na hataki watu waangamie motoni, Kwa nini anaacha watu wengine waende motoni wakati ana uwezo wa kuwabadilisha?
Kwanza expert wangu fahamu kwamba dunia ni sehemu ya mtihani,hapa tunatahiniwa

Kama kusingekuwa na uovu na wema basi hii isingekuwa dunia bali bustani ya peponi

Nashindwa kuelewa ni kipi kwenu kuelewa kwamba kujua kwa Mungu hakuhusiani na matendo yako mema na maovu,,

Yeye anajua mwisho wako,mfano Mungu anajua ntaingia peponi,kwahiyo hata kama sasa hivi nafanya maovu ujue nitabadilika na mwisho wa siku ntaenda peponi kudhibitisha au kutimiza yale ambayo tayari yamejulikana mapema

Anatuacha tuingie motoni kwakuwa tayar tumeonyeshwa njia ya kufuata,sasa ni juu yetu kuamua tunataka kwenda wapi

Je utamlaumu Mungu?

Kinachofuata hapa ni ubishi tu,maana hoja iko wazi
 
Mungu ni nani kwako?
Umejuaje kama Mungu yupo?
Kwanini lazima uhangaike kufuatilia uwepo wake kama yeye kakaa kimya?

Kama yupo, yuko wapi au yupoje?
Kwa nini unaamini kuwa Mungu anajua future yako?
Kama huamini, je umejuaje kama Mungu anajua future yako?

Kama Mungu anajua kila kitu kuhusu wewe, bado unasema una uhuru wa kuchagua?
Kama alijua utakwenda motoni, kwa nini alikuumba wakati wewe ni wa motoni tu?

Je, future inaweza kubadilika kama Mungu tayari ameshakupangia?
Kama haiwezi kubadilika, ina maana matendo yako hayana maana?
Kwa nini ahukumu kitu alichojua kabla hakijatokea?

Hata socrates alinyongwa baada ya watu wa dini kushindwa kumjibu maswali kama haya!!
 
Mungu hapendi hata mtu mmoja apotee anapenda atubu dhambi zake aishi milele,(2Petro3:8-10)
Kwa hiyo mtu mwenyewe atapotea kama atazikataa rehema za Mungu pale atakapokataa kutubu dhambi zake ili apate Msamaha wa dhambi,(Matendo2:38)(Warumi6:23)
(Ufunuo21:8)
KUhusu kujua kuwa mtu ataenda motoni au mbinguni! Mungu anajua kabisa,wapo watakaokataa kutubu dhambi na kuangamia na anajua wapo watakaotubu dhambi na kusamehewa hatimaye kwenda mbinguni.
Kwa kuwa ametupa Nafasi ya Kuishi tuitumie Siku ya LEO kutubu dhambi zetu ili atusamehe dhambi zetu,mwisho wake tukakae naye Mbinguni milele,(Waebrania4:7-10)
(Luka15:7,10)-Ni FURAHA MBELE ZA MUNGU NA MALAIKA MBINGUNI PALE UNAPOTUBU DHAMBI.
Lakini tukikataa,
(Waebrania10:26-31)
Mungu ATUSAIDIE!
 
Hapo kuna mawili:

1. Mungu anajua kila kitu mwanzo mwisho. Kwahiyo anajua kabisa huyu atakuja kuishia motoni, na huyu atakuja kwenda mbinguni. Kama hivyo ndivyo, manake kuna watu wameumbwa specifically kwaajili ya kuja kuchomwa moto wapende wasipende!

2. Mungu hajui nani ataenda mbinguni wala nani ataenda motoni. Itategemea na matendo ya mtu mwenyewe. Kama hivyo ndivyo, manake huyo hawezi kuwa Mungu maana sifa mojawapo ya mungu ni kujua kila kitu!
Ina maana wakati nazaliwa hata yeye anakua hajui mi nitaenda motoni au peponi?
 
Kwanza expert wangu fahamu kwamba dunia ni sehemu ya mtihani,hapa tunatahiniwa
Mungu anakupa mtihani ili agundue nini?

Kuna kipi huyo Mungu asichokijua hadi atupime kwa kutupa mitihani?
Kama kusingekuwa na uovu na wema basi hii isingekuwa dunia bali bustani ya peponi
Kwa hiyo huyo Mungu alidhamiria kabisa kuweka uovu na wema duniani ili tu pasiwe kama peponi?
Nashindwa kuelewa ni kipi kwenu kuelewa kwamba kujua kwa Mungu hakuhusiani na matendo yako mema na maovu,,
Kama Mungu hausiani na matendo yetu, mbona mnamuhusisha huyo Mungu kwenye uumbaji wetu binadamu?

Mnamuhusisha huyo Mungu kwenye uumbaji halafu likija suala la mema na maovu hamtaki ahusishwe.

Sasa huu uovu ulijileta wenyewe sio?

Je huyo Mungu hakujua kwamba uovu utakuja kuwepo duniani audhibiti na kuuzuia mapema?
Yeye anajua mwisho wako,mfano Mungu anajua ntaingia peponi,kwahiyo hata kama sasa hivi nafanya maovu ujue nitabadilika na mwisho wa siku ntaenda peponi kudhibitisha au kutimiza yale ambayo tayari yamejulikana mapema
Kama Mungu anajua mwisho wa mtu, na anaweza kubadilisha destiny ya mtu, Kwa nini hawabadilishi watu waovu watende mema ili mwishoni waingie peponi?

Kama Mungu anajua mtu fulani ataingia jehanamu, Je mtu huyo anaweza kubadilika yeye mwenyewe ili aingie peponi?

Kama mtu hawezi kubadilika yeye mwenyewe ili aingie peponi, Je Mungu ndie mpangaji wa watu kuingia jehanamu?
Anatuacha tuingie motoni kwakuwa tayar tumeonyeshwa njia ya kufuata,sasa ni juu yetu kuamua tunataka kwenda wapi
Kwa nini huyo Mungu anaacha watu waingie motoni ikiwa yeye ndiye mpangaji wa maisha yetu tangu mwanzoni na hata milele?

Huyo Mungu, Alishindwaje kufanya binadamu wote wafuate njia moja tu ya wema ili wote tuingie peponi?

Kama ni juu yetu kuamua tunataka kwenda wapi, Je sisi ndio wapangaji wa maisha yetu na destiny zetu?
Je utamlaumu Mungu?

Kinachofuata hapa ni ubishi tu,maana hoja iko wazi
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba hapendi uovu, audhibiti na kuuzuia mapema usiwepo duniani?

Au alijua na kufanya makusudi uovu uwepo duniani?
 
Mungu hapendi hata mtu mmoja apotee anapenda atubu dhambi zake aishi milele,(2Petro3:8-10)
Huyo Mungu kama hapendi hata mtu mmoja apotee, Je Alishindwaje kuumba dunia isiyo na dhambi?

Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao mtii na kumwamini siku zote ili waishi milele?
Kwa hiyo mtu mwenyewe atapotea kama atazikataa rehema za Mungu pale atakapokataa kutubu dhambi zake ili apate Msamaha wa dhambi,(Matendo2:38)(Warumi6:23)
(Ufunuo21:8)
Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu wenye uwezo kuzikataa rehema zake?

Huyo Mungu alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao zikubali rehema zake siku zote na wakati wote?
KUhusu kujua kuwa mtu ataenda motoni au mbinguni! Mungu anajua kabisa,wapo watakaokataa kutubu dhambi na kuangamia na anajua wapo watakaotubu dhambi na kusamehewa hatimaye kwenda mbinguni.
Huyo Mungu anashindwaje kufanya binadamu wote watubu dhambi ili wote twende mbinguni?

Yeye si ni Mungu muweza wa vyote?

Kwa nini huyo Mungu anaacha watu wengine waende mbinguni na wengine motoni?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Kwa kuwa ametupa Nafasi ya Kuishi tuitumie Siku ya LEO kutubu dhambi zetu ili atusamehe dhambi zetu,mwisho wake tukakae naye Mbinguni milele,(Waebrania4:7-10)
(Luka15:7,10)-Ni FURAHA MBELE ZA MUNGU NA MALAIKA MBINGUNI PALE UNAPOTUBU DHAMBI.
Lakini tukikataa,
(Waebrania10:26-31)
Mungu ATUSAIDIE!
Mungu Alishindwaje kuumba dunia isiyo na dhambi?
 
Vishu Mtata mbona unakuwa mtata😂😂

Hajakupangia ndio maana tukashushiwa manabii na mitume watuambie lipi jema na lipi ovu

Sasa tukiamua kufanya mema tutaingia peponi na maovu motoni vile vile

Kwa maana nyingine na kama vile Mungu amekupa hoja ya kujitathimini mwenyewe ili siku ya hukumu usiwe na kisingizio

Atakwambia walikuja mitume na manabii lkn hukuwafuata wala kuwasikiliza ona sasa huna wa kumlaumu pambana na hali yako

Kama yeye ndio angatuhukumu basi hakukuwa na haja ya kuwaleta mitume ambao ingekuwa kazi bure kama tayar hakuna uhuru wa kufanya mema au mabaya

Kwa maana nyingine jichunguze mwenyewe je mpaka sasa unaishi katika misingi gani
Mkuu mi nataka kujua tu pale ninapozaliwa, je Mungu anakua amejua mwisho wangu ama nae anakua hajajua ila itategemeana na matendo yangu.?

Nyongeza..
Kuna watu mtu akifa husema ni mapenzi ya Mungu, siku yake ilifika na mambo kama hayo kumaanisha kua Mungu ndio alipanga afe kwa namna ile.
Sasa najiuliza, mtu alichomwa moto kwa wizi, aliepigwa risasi, aliejiua kwa ufupi kifo kilichosababishwa moja kwa moja na mkono wa binadamu nayo pia ni mapenzi ya Mungu? Ilipangwa tangu awali mtu huyu afe kwa kudungwq bisu la koromeo na kaka yake??

Karibu.
 
Hapo kuna mawili:

1. Mungu anajua kila kitu mwanzo mwisho. Kwahiyo anajua kabisa huyu atakuja kuishia motoni, na huyu atakuja kwenda mbinguni. Kama hivyo ndivyo, manake kuna watu wameumbwa specifically kwaajili ya kuja kuchomwa moto wapende wasipende!

2. Mungu hajui nani ataenda mbinguni wala nani ataenda motoni. Itategemea na matendo ya mtu mwenyewe. Kama hivyo ndivyo, manake huyo hawezi kuwa Mungu maana sifa mojawapo ya mungu ni kujua kila kitu!
Mimi nipo namba mbili hapo, life style yetu huamua mengi na hata hatma zetu hapa duniani.
 
Kabisa
Vishu Mtata mbona unakuwa mtata😂😂

Hajakupangia ndio maana tukashushiwa manabii na mitume watuambie lipi jema na lipi ovu

Sasa tukiamua kufanya mema tutaingia peponi na maovu motoni vile vile

Kwa maana nyingine na kama vile Mungu amekupa hoja ya kujitathimini mwenyewe ili siku ya hukumu usiwe na kisingizio

Atakwambia walikuja mitume na manabii lkn hukuwafuata wala kuwasikiliza ona sasa huna wa kumlaumu pambana na hali yako

Kama yeye ndio angatuhukumu basi hakukuwa na haja ya kuwaleta mitume ambao ingekuwa kazi bure kama tayar hakuna uhuru wa kufanya mema au mabaya

Kwa maana nyingine jichunguze mwenyewe je mpaka sasa unaishi katika misingi gani
 
Kama anajua basi wewe huna uhuru wa kwenda tofauti na anavyojua.

Kama Mungu anajua wewe Samson Ernest utakwenda jehanamu, Huna uhuru wa kubadilisha destiny yako, Hata ukichagua nuru bado utaenda jehanamu. Maana tayari Mungu anajua utakwenda jehanamu na ni lazima uende. Huwezi kubadilisha destiny yako.

Kama Mungu anajua kwamba wewe Samson Ernest utakwenda Peponi, Hata ukichagua giza bado destiny yako itabaki vilevile kwenda peponi. Kama ajuavyo Mungu.

Kwa hiyo ni either Mungu anajua yote na huwezi kubadilisha destiny yako au Mungu hajui yote na unaweza kubadilisha destiny yako.
Mungu anajua usipomwamini Yesu na kuishi maisha matakatifu utaenda Jehanamu, anakupa nafasi ya kumwamini Yeye na kutembea katika njia sahihi. Kwa kuwa anajua kinachofuata kwako sio kizuri, anatumia watumishi wake hapa Duniani kutangaza habari njema za Yesu.
 
mungu Allah yeye kashapangia watu kabla hawajaziliwa

...Allah created for Paradise those who are fit for it while they were yet in their father's loins and created for Hell those who are to go to Hell. He created them for Hell while they were yet in their father's loins. Sahih Muslim 2662c
 
Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu wenye uwezo wa kuto kumtii?

Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu wenye uwezo wa kutomuamini?

Huyo Mungu Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote?
 
mungu Allah yeye kashapangia watu kabla hawajaziliwa

...Allah created for Paradise those who are fit for it while they were yet in their father's loins and created for Hell those who are to go to Hell. He created them for Hell while they were yet in their father's loins. Sahih Muslim 2662c
They why he created us, na anajua tupo tutakaoenda motoni and what is the point ya yeye kuleta dini na kutaka tumtukuze
 
Back
Top Bottom