Amatuumba kwanza wewe hapo ulipo
Bila yeye usingekuwepo
Sikweli, Bila Mama yangu na Baba yangu kukutana ndiyo nisingekuwepo au labda My mother angetoa mimba kipindi mjamzito.
Hata wewe unauwezo wa kuleta kiumbe kuja kuteseka au kubaki bila kuzalisha.
Kuna watu wana vipawa vya biashara, kilimo, ujuzi tofauti tena wengi na hawamuamini huyo mungu.
Kwa kutambua karama uliyonayo
Na kama bado haujui Muombe akujulishe
Kama baba yako mzazi mwenyewe ulikua ukimuomba pesa ya matumizi kuna mda hana sembuse kumuomba huyo baba mliyemtunga kichwani?
Hiyo siyo shida ya afya ya akili kweli?
Kwanini unajilazimisha kuamini bila sababu?
Ili uwe Superhero?
Ili watu wakuone mwema?
Ili upate pesa, mali, amani na hivyo vingine mnavyodanganywa?
Kwanini ili upate amani na mafanikio ya kimungu lazima ufanye yale ambayo hata wasioamini pia wanafanya like kazi, biashara n.k?
Unakuta mtu anachangamoto za kisaikolojia maybe ni Single parented haswa mother hivyo ana lack Father figure na anakosa discipline kwenye maisha yake kisha anakua addicted to alcohol, porn, weed or movies/series, kula junk foods etc.
Psychologically Badala ya kutafuta real father figure like doctor wa kiume wa saikolojia ili azibe pengo hilo yeye anahangaika na baba asiyeonekana na mwisho huwa mbaya zaidi sababu expectations huwa hazifikii kuwa reality.
Fanya utafiti utagundua wengi wanaostruggle na dini na Imani wamerithi imani kwa wazazi au wamelack malezi ya real father.
Sibuni kichwani ninachoandika, pitia vitabu hivi utaanielewa.
•Faith of the Fatherless: The Psychology of Atheism – Paul Vitz
- kinaeleza kuwa wanaume wengi wanaohangaika na Mungu walikua bila baba na mara nyingi wanamtafuta baba wa mbinguni kuziba hilo pengo.
•In the Realm of Hungry Ghosts – Dr. Gabor Mate.
-Anaonesha jinsi trauma ya utotoni ikiwemo malezi duni au yasiyojali hujenga watu waliojawa na hamu ya kujificha, kujiliwaza, na kuepuka ukweli wenye Maisha ya addiction.
•12 Rules for Life: An Antidote to Chaos — Jordan B. Peterson
-Anasisitiza umuhimu wa malezi ya baba na male role models, akiamini vijana wa leo wanaangamia kwa sababu hakuna wa kuwaambia simama wima, fanya hivi n.k.
- kInafaa kwa mtu aliyekata tamaa na mwenye maisha ya ovyo.
•Spiritual Bypassing — Robert Augustus Masters
- kInaeleza jinsi watu wanavyotumia sala, ibada, au maandiko kufunika maumivu ya ndani badala ya kuyakabili.
-Mfano: mtu ana trauma ya baba lakini anasema Mungu Baba ananitosha lakini ndani anateseka, hana nidhamu, na anajirudia kwa uraibu.
Tatizo mmekazana kusoma tu bibble na Quran.