Je, Mungu anajua utakwenda motoni au mbinguni?

Je, Mungu anajua utakwenda motoni au mbinguni?

Ni kweli Mungu amempangia kila mtu maisha yake kuanzia mwanzo hadi mwisho, ila sio lazima kila kitu kifanyike kama alivyokupangia.

Ili kukamilisha kila ambacho Mungu alikupangia, Mungu alimuumba mwanadamu kufanya mambo yake yote kwa kushirikiana na yeye(kwa utaratibu wa Mungu mwenyewe), na Kitu Kizuri(Wakati mwingine Kibaya) ni kwamba Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa kuamua, hata kama ataamua kinyume na mipango ya Mungu.

Kuhusu kwenda Mbinguni au Motoni ni jukumu lako mwenyewe based na maamuzi unayofanya maana lipo ndani ya uwezo wako.

Majibu:
1. Mungu anajua unauwezo wa kwenda mbinguni na anataka hivyo. Kwenda motoni means ume fail.
2. Yes, future inaweza kubadilika, inategemea umekaa karibu au mbali kiasi gani na Muumba mwenyewe.
Kweli
 
Kabla ujazaliwa ukiwa tumboni kwa mama ako..
Ulishaandika kabisa kama wewe ni wa motoni au wa peponi mkuu...

Kwahyo Mungu anajua kila kitu ni kazi yako ww kujirekebisha au laah sawa shekhe..

Kingine hili swali lako limekaa kikafiri
Kobazi mbona vurugu mapema yote hii
 
Kabla ujazaliwa ukiwa tumboni kwa mama ako..
Ulishaandika kabisa kama wewe ni wa motoni au wa peponi mkuu...

Kwahyo Mungu anajua kila kitu ni kazi yako ww kujirekebisha au laah sawa shekhe..

Kingine hili swali lako limekaa kikafiri
Kwa tafsiri hiyo basi itakua hajui mwisho wako upoje.

Maana unaweza kubadilika dakika za jioooni.
 
Kwa mufundisho ya Kiislamu

Allah/Mwenyezi Mungu anajua mwisho wa kila kiumbe chake,kwahiyo ni sahihi kusema anajua wapi wataingia peponi na wapi motoni

Amesema Mtume swala aallahu alaih wa sallamu, mwaadamu akifikisha miezi minne ndani ya tumbo la mama yake,anakuja Malaika kufanya mambo manne
Anapuliziwa roho yake

Kwanza, anaandikiwa umri wake,je ataishi miaka mingapi

pili, anaandikiwa riziki yake

tatu, anaandikiwa kheri na shari yake [kwa maana mitihani na changomoto,pamoja na kheri unazozipata]

nne,kuandikiwa kama mtu wa peponi au motoni [ hapa sio kwamba unapangiwa fate yako laa,bali tayar maisha yako yanajulikana utaishi vipi na utaishia wapi]

Kinachoweza kubadilika ni kadari ya kheri na shari,hapa dua au sala hubadilisha haya mambo

Ndio ile ulikuwa unaomba upate nyumba,unashangaa badala ya kupewa nyumba umeepushwa na ajali fulani

Nikifafanua zaidi kuhusu kwenda motoni na peponi ni kwamba, amesema Mtume wa Allah Mtu maisha yake yote anaweza kufanya matendo ya watu wa peponi,lakini ikiwa imebaki kidogo umri wake kuisha akabadilika na kufanya matendo ya watu wa motoni na kuingia motoni

Na mtu anaweza kuishi maisha yake yote anafanya matendo ya watu wa motoni na ikabaki kidogo tu umri wake kuisha akabadilika na kufanya matendo ya watu wa peponi na kuingia peponi

Ndio maana sisi waislamu tunahimizwa sana kuomba mwisho mwema,na vile vile haifai kumhukumu mtu fulani kwamba ataingia motoni hata kama matendo yake ni mabaya,kwasababu hujui huenda mwisho wa siku akatubu na kufanya mema na kuingia peponi
 
Setfree Na inakuaje unafikiria utaenda mbinguni na kuna makosa hujajua
Utajihakikishiaje 100% utaenda huko?
 
Na mtu anaweza kuishi maisha yake yote anafanya matendo ya watu wa motoni na ikabaki kidogo tu umri wake kuisha akabadilika na kufanya matendo ya watu wa peponi na kuingia peponi

Ndio maana sisi waislamu tunahimizwa sana kuomba mwisho mwema,na vile vile haifai kumhukumu mtu fulani kwamba ataingia motoni hata kama matendo yake ni mabaya,kwasababu hujui huenda mwisho wa siku akatubu na kufanya mema na kuingia peponi
Kwa nini mnasema Peponi?
Na Kama mtu anafanya Dhambi akifa anaenda kuteswa huko kuzimu
Alafu na wale ambao hawajampokea Yesu na ambao hawajamuamini
 
Kwa hiyo yeye mwenyewe hajui mwisho wako ni upi(kulingana na swali la mleta maada)
Yeye ni mwanzo na mwisho, yeye ndiye aliyekuumba, hawezi kushindwa kujua mwisho wako, isipokuwa amekupa uhuru wa kuchagua giza au nuru, uende peponi au jehanamu
 
Back
Top Bottom