Hivyo Mungu alimuumba shetani ili aje kutesa na kunyanyasa wanadamu huku yeye kabaki mbinguni anacheki game tu.
Huo siyo upendo tena, hiyo ni system.
Sasa muacheni Shetani afanye kazi aliyopewa na boss wake.
Je, unamlaumu Shetani au boss wake aliyemtuma kuchezesha Squidgame?
Mungu ndiye aliamua kutuumba sisi, na alituumba Kwa Mapenzi yake kwetu, Mungu alipotuumba alitaka tuishi vizuri, na ili tuishi Vizuri akatuwekea taratibu na Sheria....! Pia akasema tumuabudu yeye pekee Kwa sababu ndiyo muumba wetu.
Mungu ilibidi aachilie Shetani aje kutawala hapa Duniani ili Tumuabudu yeye, hata sisi Wachache tunaomuabudu, tunamuabudu ili tuwe huru Toka Vifungo vya Shetani, kama Shetani asingekuepo means Jehanamu isingekuepo coz Jehanamu aliumbiwa Shetani, hivyo hakuna Binadamu ambaye angemwabudu Mungu, So pale Shetani akitubana kwenye Kona ndipo tunamwendea Mungu Sasa, na pale tunapomwendea yeye ndipo hapo akaweka Kanuni. (Mungu anazo kanuni na Shetani anayo Masharti)
Kanuni za Kuomba, kanuni za kupigana Vita vya kiroho, kanuni za kusinda n.k.... Na ili umshinde Shetani lazima ufate kanuni hizo, ufate Sheria zake.
Dunia hii ilipoumbwa haikuanza tu na Vita, haikuanza tu Magonjwa, haikuanza na Ajari, mabaya yote yaliyokua yanatokea ni Kwa sababu Binadamu hataki kufata Sheria na Kanuni ambazo Mungu alituwekea.
Mfano tunazo Amri za Mungu, Mungu anasema USIUE, kwani wewe Binadamu usipoua kama Mungu alivyosema, Mungu anapata faida Gani, ama unadhani Ukiua Mungu anapata Hasara Gani, ila usipoua ni wewe ndiyo unapata faida, coz ukiua na wewe utauwawa, ama utafungwa Maisha Jela.
Alisema Usizini, usipozini wewe unadhani Mungu anapata faida yoyote..!? Ila ukizini ni wewe utapata hasara, utakamatwa Ugoni, utapigwa faini, utavuruga familia na Watoto utapata Ukimwi n.k.
Hivyo utaona yote aliyotukataza ni Kwa faida yetu wenyewe, ili tuishi Kwa raha na Upendo sawa na maono yake.
Sisi Binadamu hatutaki kufata Sheria Wala Kanuni, na alisema msipofata Sheria na Kanuni mtakutana na Shetani, ana Hasira kama Simba....! Mabalaa yakitukuta hatutaki kurudi kwenye Sheria zake na Kanuni zake, tunataka Mungu atuokoe huku tuliendelea na njia zetu mbaya.
Kama wewe ni Mama ama Baba nyumbani Watoto wako umewapa Sheria zako, na wanafata, na wasipofata unawaadhibu, Tena kama Baba tutasema Baba hakosei, akisema kasema...!
Dunia hii Haina maana yoyote ya sisi kuwepo bila kumwabudu Mungu, nje ya hapo Haina Maana yoyote, ni muhimu kuacha lDhambi na kumrudia Mungu.
The Creator is Coming.