Je, mgonjwa akifika kitengo cha emergency/idara ya dharula anatakiwa kupata huduma baada ya muda gani?

Je, mgonjwa akifika kitengo cha emergency/idara ya dharula anatakiwa kupata huduma baada ya muda gani?

Joined
Apr 28, 2017
Posts
36
Reaction score
87
Emergency Department au kwa kiswahili Kitengo cha magonjwa ya dharula ni miongoni mwa idara mpya kuanzishwa katika nchi zetu za africa, kitengo hiki hakina miaka hata kumi na tano, mwanzilishi wa kwanza kwa Tanzania ilkuwa ni Muhimbili National Hospital wakishirikiana na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili mnamo mwaka 2011.

Then baada ya hapo ndo hospitali nyingine zikafutata na kwa sasa hospitali nyingi sana zina hii idara. Kabla ya Idara hii/kitengo hiki kuanzishwa wagonjwa wote waliokuwa wanafika katika hospitali walikuwa wanafikia sehemu inaitwa casuality.

Kwenye hili eneo la casuality au OPD hamna matibabu yoyote ya maana yalikuwa yanafanyika, mgonjwa alikuwa akifika anapelekwa wodini, kiufupi matibabu yalikuwa yaanzia wodini, mpaka ufike wodini, upate kitanda, umuone daktari, kufanya vipimo na kuhudumiwa ilikuwa inachukua muda kidogo, hivyo wagonjwa wengi walikuwa wanazidiwa zaidi au wanakufa kutokana na hii delay/uchelewaji wa kuanza matibabu stahiki.

Lengo la uanzishwaji wa idara ya magonjwa ya dharura ndo ukaja hapa sasa, ingawa kwetu bado ni tasnia ngeni, kwa nchi zilizoendelea zimekuwa na idara ya magonjwa ya dharula muda mrefu sana. Lengo la idara hii ni kwamba mgonjwa anapofika hospitalini mwenye magonjwa ya dharula badala ya kusubiri kwenda kuanzia matibabu wodini, matibabu aanzie hapa mwanzo kabisa anapofika hospitalini ili kama kuna mambo ya dharula yanayoweza kumuua mgonjwa au kunfanya azidiwe yaweze kuanza kutatuliwa hapa kabla ya kwenda wodini.

Tofauti na wengi wanavyodhani au kufikiri, Idara hizi za magonjwa ya dharula zinapokea wagonjwa wa aina zote, nikimaanisha kuanzia wagonjwa mahututi, wanaofika wamekufa tayari, wagonjwa wa ajali mbalimbali, wagonjwa wasioumwa wanaokwenda kwa ajili ya check up, wagonjwa wanaoumwa lakini sio mahututi, n.k

Kutokana na hali ya rasilimali mbalimbali katika eneo husika, mfano idadi ya madaktari, wauguzi, majengo/ vyumba vyaa kuonea wagonjwa n.k, sio kila mgonjwa atakaefika eneo la emergency depertment atahudumiwa papo kwa papo, kuna ambao watahudumiwa haraka sana, kuna ambao wataambiwa wasubiri kidogo.

Katika kufanya haya maamuzi kuwa ni yupi awahi kuhudumiwa na yupi asubiri, daktari au muuguzi anatumia vigezo vya kitaalam katika kuwasort hao wagonjwa, kitaalam hii inaitwa Triage, kutokana na dalili au matatizo aliyokuwa nayo mgonjwa kuna ambaye hawezi kusubiri kabisa lazima aonwe mara moja na kuna ambaye anaweza kusubiri, hivyo ni kawaida sometimes kuona mgonjwa anafika anapelekwa chumba cha watu wanaoumwa sana ‘ Resuscitation room’ kupata huduma kabla yako.

Niweke angalizo hapa, hapa nimezungumzia misingi ya tiba kitaalam na sio wale anatoa rushwa ili apate huduma mapema, au wale wa fast track na VIP.

Lakini pia ni jukumu la Daktari au muuguzi kupita kila mara kuwaangalia hawa wagonjwa aliowaweka katika kundi la kusubiri kama hali zao za afya zimebadilika ili waende kupata huduma mara moja au waendelee kusubiri.

Hivyo ingawa ni idara ya magonjwa ya dharula lakini haimaniishi kila mtu atakayefika eneo hili atapata huduma punde tu afikapo, vitu vitakavyochangia uharaka wa kupata huduma ni pamoja na miundombinu, rasilimali watu na vifaa tiba, aina ya ugonjwa/dalili alizonazo mgonjwa, na hii ndivyo inavyofanyika duniani kote sio Tanzania pekee.

Mwisho kabisa, lengo la kuandika hapa sio kuwatetea watoa huduma wazembe ambao hawafiki kazini, hawatoi huduma kwa wakati, ili watoe huduma wanataka rushwa n.k,
 
Back
Top Bottom