GREAT ! Nadhani kama wengi watakuwa na mtazamo kama wako nafikiri tutapiga hatua na hii ishu itakuwa solved huku tukikata ishu nyingine lakini watu wanajifanya kama mbowe asihojiwe ndio kitu kinachokwamisha hii thread kuwepo hapa na nadhani itakuwepo as long as it can hadi atakapotoa maelezo sahihi !
hizi ndizo hoja zisizo na mguu wala kichwa, nani kakataa Mbowe asihojiwe hapa? Hakuna mtu anayeogopwa hapa kama watu wanamsema Rais wao kwa uhuru Mbowe ni nani asihojiwe. Tatizo linakuja pale ambapo watu wanatunga story na kuzilazimisha alimradi tu ili ionekane Mbowe ahojiwe au mtu mwingine vile vile.
Mtu kaja na kusema "Mbowe kafeli mtihani" watu na akili zao timamu wanarukia na kuanza kurusha madongo ya mtu aliyefeli; mtu kaja na taarifa "Mbowe Kaifisili NSSF" watu na akili zao wanarukia na kusema Mbowe arudishe mkopo yaishe! Lakini hakuna anayejiuliza ni lini walisikia NSSF imefilisika!
Watu wanakimbilia na kusema "arudishe mkopo bwana" kwani huu ni mkopo wa gengeni? Huu si mkopo wa Juma kwenda kwa Marko ambapo mtu anasema "nikopeshe shilingi 1000 bwana nitakulipa"! Mkopo huu una masharti na vipengele kibao na kama mtu anafikia mahali mkopo haulipiki mtu anahaki ya kunegotiate terms za mkopo huo.
Hivi sasa tunasikia kuhusu matatizo ya mikopo ya nyumba Marekani hadi watu wanaanza kunyang'anywa nyumba zao, mabenki na serikali si wangeacha tu watu wafikishane mahakamani? Lakini kwa nini leo wanahangaika kuwasaidia na mikopo hiyo? Hata wale wenye mikopo ya elimu, au mingine kuna wakati inabidi mtu azungumze na chombo kilichomkopesha kujadiliana nao kupunguziwa riba n.k Hii yote ni sehemu ya uwajibikaji katika kukopo.
Je mtu kuchelewa kurudisha mkopo ni jambo geni? La hasha isipokuwa katika nchi ya kufikirika. Tanzania ilikuwa na madeni hadi tukapiga magoti kuomba yasamehewe kwa maana hayalipiki! Kama mtu umekopa mkopo wa biashara, na ile biashara haiendi unavyotaka wewe au hailipi kiasi cha kukuachai faida ya kutosha kuweza kulipa mikopo yako, unayo haki ya kukaa chini na taasisi yako ya fedha kufanya tathmini.
Lakini wajenga hoja wa hapa wao wamesikia "Mbowe anadaiwa" wao wanakurupuka na kuaanza kutoa laana na kuona kuwa mbowe naye ni fisadi. Wanachoshindwa kukiri ni kuwa Mbowe kafikishwa mahakamani, na hata kama anataka kulipa haendi kulipa hadi mahakama itoe uamuzi wake. Sasa kama Mahakama ingekuwa imesema Mbowe ana makosa na afilisiwe au alipe mkopo huo kwa masharti x,z na Mbowe akakataa kulipa au akapoteza na rufaa basi sisi sote tungeshangaa kwanini serikali imeshindwa kumchukulia hatua. Sasa mtu anayefuata mfumo wa mahakama katika kesi ambayo imefunguliwa na mtu mwingine anaitwa fisadi, je wale wanaofanya maamuzi kana kwamba hakuna mahakama tuwaitaje?
I understand kuna karaha fulani ka kuonesha Mbowe, Mrema, Mtikila, Lipumba n.k kuwa na wenyewe mafisadi na hivyo CCM waweze kujisikai "sisi siyo mafisadi peke yetu"; sasa hiyo ni hoja isiyo na kichwa kwani angalau onesha basi ufisadi wenyewe usipachike ufisadi!
Well, nikuulize kosa la Mbowe ni lipi katika hili? Kuchukua mkopo, kushindwa kulipa mkopo, kugoma kulipa mkopo, kuchelewa kulipa mkopo, kusubiri amri ya mahakama, n.k ? Ni nini hasa kosa lake kwa mujibu unavyoelewa wewe maana nimeiangalia mada hii tangu mwanzo ilipopachikwa hadi hivi sasa sijaona hoja hasa ya kosa la Mbowe ni lipi? Naomba unifahamishe maana naona mwenzangu umelijua hasa kosa lake. Ukiweza kunishawishi na mimi nitakuunga mkono kutaka Mbowe arekebishe kosa hilo bila kupatwa na kigugumizi.