Je, kikao cha Rais na Wenyeviti wa Vyama vya siasa isipokuwa CHADEMA ni mpango wa kuzigawa kura za Urais za Tundu Lissu?

Je, huyo mnayemuita Magufuli atakubali Lissu agombee Urais? Au anaweza kumzuia asiingie nchini kama Kabila alivyomzuia Katumbi? Au anaweza kupeleka sheria kwa spidi ya mwendokasi bungeni ili kumzuia!?
 
Lakini itabidi kwanza TL akili kwamba alitupotosha katika vita ya mageuzi ya madini. Aliwasihi sana wabunge wasipitishe marekebisho ya sheria za madini kwamba tutashitakiwa MIGA na akasisitiza kwamba ACCACIA itatufilisi sisi watanzania. Sasa kwasababu hayo yote yalienda mrama- proved failure, akianza kwa kuomba msamaha hapo kura tutampa. Tutajua ni mwenzetu sisi waTz wa hali ya chini.
Hoja dhaifu, kwani ile 420 t. aliyotudanganya jiwe kwamba tutalipwa iko wapi?
 
Ila ukiangalia kwa undani uchaguzi kwa upande wa bara kwa upinzani hasa kura za ubunge na udiwani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja ni pigo sana kwa ccm hivyo ccm wanataka wasambaratike na kama chadema watatoa Rais basi ubunge na udiwani watataka uwiano sawa na kwa sheria na maandishi ili baadaye wasigeukane
 
Nashukuru kwa kuwa uzi wangu una 2000 viewers nawaomba moderators wanifanye platnum member haraka sana kabla sijaenda mahakamani kudai!!!
 
LABDA tume ya uchaguzi itoke ULAYA .AFRICA KINA JECHA NI WENGI SANA
About 3,000 people were killed during post-election violence 10 years ago, when the former President Laurent Gbagbo refused to step down after losing to Mr Ouattara.
 
Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.

Lissu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule! Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!

Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata Sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lissu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi

Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lissu kama mgombea hakika Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo !Ndipo tunapotazama kikao cha juzi! Je, Lissu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani, CCM watauweza mziki wake tena katika kipindi ambacho Tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia.

Je, CCM wataambulia hata kura milioni moja?

Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu Lissu na ugombea wake wa kiti cha Urais!! Rais Magufuli anataka kuzigawa kura za Lissu ili asijegaragazwa vibaya Oktoba mwaka huu!!!

Rais Magufuli yupo tayari Maalim Seif ashinde Zanzibar kuliko Lissu ashinde Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Lissu anamnyima usingizi Rais Magufuli na ndio maana ya kile kikao juzi kuzigawa kura zake huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo Oktoba mwaka huu!

Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!

You guys mnaotakaga sana na kusahau reality

Mkikutana na wanababe wanawaburuza maana mna ukoko kichwani


Huyo Lissu yuko wapi? Lini CDM itamsimamisha Lissu?

Tume ya uchaguzi imekuwa huru?
 
Kura za Lissu zitakuwa kwwnye 60% na wagombea waliobakia watagombania 40%. Watu washachoka kuishi kwa vitisho na kejeli kila wakiamka! Nchi imekuwa kama Scania iliiyofungwa tairi za basikeli? Inaahindwa kusonga mbele na kila tairi limeinamia opposite direction!
Kuna vitu namkubali sana tena sana ila dish lake huyumba sana
1.Kushtakiwa MIGA kwa ajili ya madini liliyumba

2. Kushabikia kulana tigo a.k.a USHOGA liliyumba pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhakika wa kura za Lissu ni moja tu ambayo ni ya kwake. Lissu mwenyewe Hana uhakika kama mke wake atampigia yeye au CCM achilia mbali watu wake wa karibu, Kwa mantiki hii ushindi kwa Lissu ni mdogo sana.

Miaka ya nyuma hazina ya CHADEMA ilikuwa ni wale wenye umri kati ya miaka 18-25, kwa Sasa kundi hilo wamekuwa ni watu wazima ,wengine wameamua kubadilika, wengine wamejiunga CCM na wengine wanaona CHADEMA si sehemu salama kwa vijana kisiasa.

Mpaka hapo umeona ni kwa namna gani kura za CHADEMA zitakavyopungua kutoka kundi Hilo. Cha kukumbuka zaidi, Lowassa ndio mpinzani wa mwisho kupata zaidi 35% ya kura ,kwa miaka zaidi ya 100 Tanzania haitashuhudia tena wingi wa kura za upinzani wa zaidi ya 20%.

Huu ni uhalisia. Lakini ni uhalisia mchungu.
 
Wewe wasema
Lazima tuangalie mifano ya yaliowakuta viongozi wabishi wa kuachia madaraka
Magufuli alifanya kosa kubwa kumshambulia Jemadari Tundu Antipas Lissu kaharibu taswira ya Tanzania na kakiua rasmi chama cha Mapinduzi
Sasa kimekuwa chama cha kuua na kuhonga wapinzani huku Takukuru na Polisi wakiimba nyimbo za kumsifia na kumpigia vigelegele
 
Upinzani bado sana ikiwa wanashindwa kufanya coalition ya ukweli na dhati. Ndipo napochoka kuwa Tanzania bado sana upinzani kuwa na team madhubuti yenye watu wenye nia ya kudumu pamoja na focus. Wengi wanafocus na wan hofu ya chakula pekee na siyo wananchi. Tutaweza kumpa TL lakini sasa team iko wapi ikiwa wanahama na kutangatanga na kuwa na price tag aliyosema Nyerere? Sitaki kutumia lile neno la mwalimu dhahiri lakini tumewaona. Anyhow "mwanasiasa anayejiuza ni malaya na chama kinachonunua wanasiasa pia ni malaya na jumba lenye watu hawa kwa pamoja linaitwa danguro" -- Mshiiri 2020. Hiyo ni quote yangu mshiiri in relation to this subject matter!
 
Back
Top Bottom