Je, kikao cha Rais na Wenyeviti wa Vyama vya siasa isipokuwa CHADEMA ni mpango wa kuzigawa kura za Urais za Tundu Lissu?

Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.

Lissu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule! Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!

Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata Sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lissu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi

Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lissu kama mgombea hakika Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo !Ndipo tunapotazama kikao cha juzi! Je, Lissu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani, CCM watauweza mziki wake tena katika kipindi ambacho Tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia.

Je, CCM wataambulia hata kura milioni moja?

Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu Lissu na ugombea wake wa kiti cha Urais!! Rais Magufuli anataka kuzigawa kura za Lissu ili asijegaragazwa vibaya Oktoba mwaka huu!!!

Rais Magufuli yupo tayari Maalim Seif ashinde Zanzibar kuliko Lissu ashinde Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Lissu anamnyima usingizi Rais Magufuli na ndio maana ya kile kikao juzi kuzigawa kura zake huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo Oktoba mwaka huu!

Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!
Unacheza na CCM wee. Walishapiga kampeni mapemaa. Kwanza lissu wanaotetea Ushoga na msaliti wa Madini. Kitendo cha kujihita mtetezi wa wanyonge, tangu mwaka juzi, kumewajenga watu wa chini, ambao ni wengi sana. Ni mtaji tosha wa ushindi wa JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mitandao ya kijimii. 60% Taifa 23% JPM 72%
Kura za Lissu zitakuwa kwwnye 60% na wagombea waliobakia watagombania 40%. Watu washachoka kuishi kwa vitisho na kejeli kila wakiamka! Nchi imekuwa kama Scania iliiyofungwa tairi za basikeli? Inaahindwa kusonga mbele na kila tairi limeinamia opposite direction!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lisu alipigwa risasi hadharani akiwa kazini akaomba apatiwe huduma za matibabu kulingana na stahiki zake akanyimwa na ubunge akanyang'anywa
IMG-20200305-WA0021.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma mitazamo mbali mbali ya kikao hiki lakini bado sikupata mwanga wa moja kwa moja kuhusu dhumuni kuu la kikao hiki.

Lissu ndio mwanasiasa pekee ambae anauzika kwa sasa kuliko wakati wote ule! Kama mbobezi wa sheria,kama mwanasiasa mwenye utashi na uwezo mkubwa wa kujieleza,mwenye uthubutu wa kugusa hata wale wasioguswa kwa kusema ukweli wa wazi pasipo uoga!

Katika kipindi hiki kigumu cha nchi yetu inachopitia hasa kutofuata Sheria na kudhulumu haki ya kuishi na uoga wa wananchi kwa Chama dola CCM Lissu ndio suluhisho pekee la nchi yetu hakuna mwingine!mimi simuoni hata kwa tochi

Iwapo upinzani hasa CHADEMA wakisimama na Lissu kama mgombea hakika Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana na yeye analijua hilo !Ndipo tunapotazama kikao cha juzi! Je, Lissu akiungwa mkono na vyama vyote pinzani, CCM watauweza mziki wake tena katika kipindi ambacho Tanzania inatazamwa kwa jicho la tatu na hao wanaowaita mabeberu kwenye la demokrasia.

Je, CCM wataambulia hata kura milioni moja?

Kikao kile kwa maoni yangu kinamhusu Tundu Lissu na ugombea wake wa kiti cha Urais!! Rais Magufuli anataka kuzigawa kura za Lissu ili asijegaragazwa vibaya Oktoba mwaka huu!!!

Rais Magufuli yupo tayari Maalim Seif ashinde Zanzibar kuliko Lissu ashinde Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Lissu anamnyima usingizi Rais Magufuli na ndio maana ya kile kikao juzi kuzigawa kura zake huku akilitafuta bao la mkono jingine hapo Oktoba mwaka huu!

Tuendeleze tafakuri ndugu zangu!!!
Kwani ni Chadema tu ndo hawakuitwa Ikulu? Sijamuona Dovutwa, Mrema, Sipunda, Makaidi (Eti na yeye ni Mwenyekiti wa chama Taifa), na wengineo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh! Kwani mgombea wa Chadema ni Lissu? Mbona taarifa nyeti nilizonazo toka Ufipa mgombea urais 2020 wa Chadema ni Bernard Camillius Membe?
 
Back
Top Bottom