lord atkin
Senior Member
- Sep 30, 2018
- 197
- 683
Kufuatia kuibuka kwa mjadala wa ruzuku za vyama vya siasa kufuatia kauli ya Makamu mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Kinana aliyonukuliwa akisema CHADEMA wamechukua ruzuku ya shilingi za kitanzania bilioni 2.7 nimeona ni vyema nikaleta mgawanyo wa ruzuku za vyama vya siasa kama ilivyoripotiwa kwenye gazeti la Mwananchi la Tarehe 15 Januari 2021 mwezi mmoja tu baada ya uchaguzi habari yenye kichwa "VYAMA SITA VYALAMBA SH 1.4 BILIONI ZA RUZUKU".
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Kila mwezi hutoa shilingi bilioni 1.4 kama ruzuku kwa vyama vya siasa. Na mgawanyo wa ruzuku hiyo kwa vyama vya siasa kwa Kila mwezi kutokana na mafanikio na kura za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni kama ifuatavyo
1. CCM
Chama cha Mapinduzi hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania bilioni 1.33 kila mwezi. Kwa hesabu za haraka haraka mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi CCM wameshapokea shilingi Bilioni 47.88
2. CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania Milioni 109.68 Kila mwezi.Mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi wameshapokea shilingi Bilioni 3.8.
3. ACT
Chama cha ACT wazalendo hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania Milioni 14 Kila mwezi. Mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi mkuu wamepokea shilingi Milioni 504
4. CUF
Chama cha Wananchi CUF hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania Milioni 5.7 kwa mwezi, na mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi mkuu wamepokea shilingi za kitanzania Milioni 205.2
5. NCCR Mageuzi
Chama cha NCCR MAGEUZI hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania 316,937/= kwa mwezi na mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi mkuu wamepokea shilingi za kitanzania Milioni 11.4
6. DP
Chama cha DP hupokea ruzuku ya shilingi za kitanzania 67,387/=, mpaka sasa miaka 3 baada ya uchaguzi mkuu wamepokea shilingi za kitanzania Milioni 2.3.
Source: Gazeti la Mwananchi la Tarehe 15 Januari 2021

Vyama sita vyalamba ruzuku ya Sh1.4 bilioni
Miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, vyama sita vyenye sifa ya kupata ruzuku vimeanza kuneemeka baada ya kuingiziwa mgawo wa fedha na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
www.mwananchi.co.tz