Hiyo ni maana ambayo haijakamilika...
Mwanamke anapoamua kuolewa maana yake ni kwamba anakubali kuhamishwa kutoka milki moja kwenda milki nyingine...
Gharama ya uhamisho huu huambatana na malipo ya mahari na kwa makabila au jamii nyingi hufanyika sherehe ya kumuaga binti...
Pia kwa tafsiri nyingine ni kwamba mwanamke anapoolewa baba wa mwanamke huwa anauza madaraka yake na kumkabidhi mwanaume anayeoa, na ndio maana wakati wa tukio la ndoa baba humtembeza bintiye na kumkabidhi mwanaume mbele ya kadamnasi...
Sasa mila nyingi za kiafrika zipo hivi, mwanamke akishaolewa hana ruksa ya kurudi kwa wazazi wake isipokuwa awe amepewa kibali maalumu kinachoambatana na taarifa kabla...
Pia mwanaume hapaswi kwenda ukweni pasipo taarifa yoyote rasmi kwa wakwe zake...
Mimi ninachoona hapa ni huyo dada kutokuongea mapema na mume wake ili safari zote mbili zipangwe kwa kufuata protokali...