CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
Habari za weekend wadau wa jukwaa hili...
Kuna dada mmoja alikuwa anatusimulia baadhi ya maisha yake ya ndoa. Moja kati ya mambo yaliyonigusa ni hili...
"Sitaki kuamini kama nilipitishwa nyumbani kwetu kama kituo cha polisi"
Ilikuwa ni nyakati za sikukuu za mwisho wa mwaka, familia ile ilifunga safari kwenda Kijijini kwao nwanaume kama ilivyo ada kwa makabila fulani.
Ukitaka kufika kijijini kwao na yule mume ilikuwa lazima upite kijiji cha na yule dada, basi safari ikaanza toka Mjini, haoooo wakafika Kijijini kwao na yule dada. Basi mdada akafikiri huenda wanaweza kupita hata kwa dakika chache wakaisalimia familia ya yule dada.
Thubutuuuu... Mume alinyoosha mguu wakapitiliza mpaka kwao, mdada kwa busara akafikiri huenda wangelipita wakati wa kurudi, holaaaa!!! Kama kawaida mume akanyoosha mguu...
Mwisho wa siku mdada akamtolea uvivu na kumuuliza kulikoni hata asipite kuwasalimu wazazi, ndugu na jamaa hata kwa muda mfupi?? Yule mume akamjibu MIMI NDIYE MWENYE MAMLAKA YA KUAMUA KUKUBALI AMA KUKATAA uende ama usiende kwenu kusalimia. Labda tu kuwe na jambo la muhimu.
SWALI KWENU WANANDOA. Je alichokifanya ni haki?
Mzee Mtambuzi, Babu Dark City, Babu Asprin, Ankal Kaizer, watu8, kabanga, EMT na wanandoa wanaume, je hivi ndivyo mnavyowa treat wake zenu???
Dada mkubwa AshaDii, gfsonwin, cacico, BADILI TABIA, Fixed Point, snowhite, mrsleo na wanandoa wanawake je ukifanyiwa hivi utachukua hatua gani??
Karibuni kwa mjadala....

Last edited by a moderator: