Je hii ni sahihi kwa Wanandoa hasa wanaume?

Je hii ni sahihi kwa Wanandoa hasa wanaume?

Weeee! Xmass wapi na easter wapi? Tena huyu kaka alikosea mimi ningebadiri na njia - kama ni njia badala ya kupitia Bamaga - sinza kwenda Urafiki nikiwa natoka Viktoria/moroko, ningepitia Mwenge - Ubungo-Urafiki ili nisipitie ukweni Sinza Madukani,

Labda kama umeoa jiwe ambalo utalibeba popote!
 
ok, nadhani nimeeleweka vibaya kwako, sikuwa na maana kuwa waliotajwa wameomba ila wale waliochukia baada ya kutotajwa kwenye thread.. embu refer kwa hawa members wawili hapo juu
dagii, slim5


Mkuu Firstborn kama charminglady hajanitaja ktk uzi wake, na mimi nikasema sichangii kwa kuwa hajanitaja, na amejitetea vzr tu, kuwa wanandoa ambao hajatutaja ktk uzi wake HATUJUI (ubinafsi-kujuana kuanzia ktk ajira mpk jukwaani), sasa wee inakuuma nini mkuu?
Kwani hapo kuna tatizo gn mpk tushambuliane?

Mwenewe mleta uzi kawataja anaowajua, mbn hapo hamna tatizo!

Ulazima wa kuwataja aliowataja anaujua yy mwenyewe!
 
Last edited by a moderator:
EMT umeshamaliza kila kitu blaza,,,,,sina cha kuongeza hapo maana nilikuwa nafikiria hivyo hivyo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Firstborn kama charminglady hajanitaja ktk uzi wake, na mimi nikasema sichangii kwa kuwa hajanitaja, na amejitetea vzr tu, kuwa wanandoa ambao hajatutaja ktk uzi wake HATUJUI (ubinafsi-kujuana kuanzia ktk ajira mpk jukwaani), sasa wee inakuuma nini mkuu?
Kwani hapo kuna tatizo gn mpk tushambuliane?

Mwenewe mleta uzi kawataja anaowajua, mbn hapo hamna tatizo!

Ulazima wa kuwataja aliowataja anaujua yy mwenyewe!

Ukiona mtu anamshambulia mleta mada badala ya kuchangia mada ujue kuna uwalakini... Uliona heading na ukafungua mada ili kujua kilichomo. Kama ulikwazika kwa vile hukutajwa shaurilo!

Kilichkuleta hapa sio kutajwa bali na mada husika!
 
Habari za weekend wadau wa jukwaa hili...

Kuna dada mmoja alikuwa anatusimulia baadhi ya maisha yake ya ndoa. Moja kati ya mambo yaliyonigusa ni hili...

"Sitaki kuamini kama nilipitishwa nyumbani kwetu kama kituo cha polisi"

Ilikuwa ni nyakati za sikukuu za mwisho wa mwaka, familia ile ilifunga safari kwenda Kijijini kwao nwanaume kama ilivyo ada kwa makabila fulani.

Ukitaka kufika kijijini kwao na yule mume ilikuwa lazima upite kijiji cha na yule dada, basi safari ikaanza toka Mjini, haoooo wakafika Kijijini kwao na yule dada. Basi mdada akafikiri huenda wanaweza kupita hata kwa dakika chache wakaisalimia familia ya yule dada.

Thubutuuuu... Mume alinyoosha mguu wakapitiliza mpaka kwao, mdada kwa busara akafikiri huenda wangelipita wakati wa kurudi, holaaaa!!! Kama kawaida mume akanyoosha mguu...

Mwisho wa siku mdada akamtolea uvivu na kumuuliza kulikoni hata asipite kuwasalimu wazazi, ndugu na jamaa hata kwa muda mfupi?? Yule mume akamjibu MIMI NDIYE MWENYE MAMLAKA YA KUAMUA KUKUBALI AMA KUKATAA uende ama usiende kwenu kusalimia. Labda tu kuwe na jambo la muhimu.

SWALI KWENU WANANDOA. Je alichokifanya ni haki?

Mzee Mtambuzi, Babu Dark City, Babu Asprin, Ankal Kaizer, watu8, kabanga, EMT na wanandoa wanaume, je hivi ndivyo mnavyowa treat wake zenu???

Dada mkubwa AshaDii, gfsonwin, cacico, BADILI TABIA, Fixed Point, snowhite, mrsleo na wanandoa wanawake je ukifanyiwa hivi utachukua hatua gani??

Karibuni kwa mjadala....

Hayo mambo inategemea mnaishi vipi, na mwanaume anakuchulia vipi na wewe umempa mamlaka ya kukutawala kwa kiasi gani, kwa kweli jinsi nnavyoishi na mume wangu hathubutu, kama kitu sitaki ni sitaki na kama nataka ninataka
 
Kuna mambo mengi sana hatuyajui kuhusu hiyo story though kama ilivyo, inaweza kuwa haki kutegemeana na mazingira. All in all mume yupo sawa coz it seem hayo hayakuwa makubaliano ya mwanzo wa safari na tatizo nililoliona, sor to say, wake wengi hujisahaulisha kuwa mume naye ameondoka kwao na makazi ya wanandoa ni yenu pia kwa asilimia 100.

Huwa mnafikiri ni nyinyi tu mliotoka kwenu, wanaume hutoka kwao pia kujenga himaya binafsi. Mwisho, alipotaka kupita si kwao(mke) bali ni kwa wazazi wa mke ambao pia ni wazazi wa wote mke na mume.


Ni mtazamo binafsi.
 
kuwa kichwa cha nyumba haimaanishi mambo yote mazuri basi mwanzilishi ni lazima awe mwanaume........

hapo ukijaribu kutafakari kwa kina utagundua kuna matatizo sana kwenye mawasiliano ndani ya hiyo ndoa....... na mimi hisia zangu zinanituma huyo mwanamke ndiyo tatizo siku hizi tunawaita mzigo.

Mkuu, kuna wanawake wengi sana, ambao kwa hapa mmewatwisha jina la mzigo, ambao huepusha shari kwa kukaa kimya kama mama anayetajwa kwenye mada hii. Na ninachokiona kwa baba huyu ni 'ubabaism' zaidi kuliko issue ya mawasiliano na hata kilichowekwa hapa kama kutokutoa taarifa kabla kwa wakwe kabla ya kuwatembelea.

Na kwa mwanaume huyu, lazima maamuzi yake mengi hayatakuwa upande wa mkewe kwa mantiki hiyo hiyo ya kuwa mkewe mzigo.
 
Huyo mume wa kumpiga biti hivyo atakuwa lofa/zoba/boya/duanzi...........

mimi mwanamke hanitishii au hawezi kupimana ubavu na mimi , ni bora makubaliano ya kiupendo yale ambayo uswahilini wanasema ni limbwata hapo kwangu shwari tu.

inategemea kama umeoa mke au kijakazi kama ni mke wala hakuna shida ya kupimana ubavu mtaelewana vizuri kwenye mambo yenu kwa kuwa mke ni partner na si adui. na hakuna haja ya kutishana na binadamu mwenzako wkt kuna aliyejuu yetu wote na mwenye uwezo wa kutufanya chochote.
 
Unachezea ndoa¿ unachezea mume¿ labda kama tulipendana mlimani¿

Mume sio Mungu cha muhimu mume aheshimiwe na mke apendwe. Mungu ndio sio wa kumchezea maana adhabu yake ni kali sana. Ndoa, mke na hata wazazi wote wanatoka kwa Mungu so waheshimiwe wote hapo. ukiheshimu mke au mme na ndoa utapata baraka za muumba lakini ubabe hutaki wazazi wasalimie sio busara.
 
Kwani sababu ya safari ilikuwa ni kwenda kuona wakwe?

najua si yakuona wakwe, ila ukizingatia wanapita karibu na wakwe kuna ubaya gani usisimame na kusalimia kisha unaendelea na safari zako, wewe niambie kaka watu8 waweza fanya hivyo kweli kama alivyofanya mshikaji...?
 
Last edited by a moderator:
najua si yakuona wakwe, ila ukizingatia wanapita karibu na wakwe kuna ubaya gani usisimame na kusalimia kisha unaendelea na safari zako, wewe niambie kaka watu8 waweza fanya hivyo kweli kama alivyofanya mshikaji...?

Kwa kadiri ya maelezo aliyoyaleta mleta mada nami ningeliweza kufanya hivyo...unless hii stori iongezewe maneno zaidi na mleta mada!!!
 
Hayo mambo inategemea mnaishi vipi, na mwanaume anakuchulia vipi na wewe umempa mamlaka ya kukutawala kwa kiasi gani, kwa kweli jinsi nnavyoishi na mume wangu hathubutu, kama kitu sitaki ni sitaki na kama nataka ninataka

Mh..una msimamo mkali sana!!
 
Wewe ndo umejibu la maana kabisa


kiufupi kabla ya ndoa inabidi muambiane mambo ya msingi ambayo hayatatatiza ndoa yenu
mfano masuala ya faimili zote mbili kwa ujumla/ idadi ya watoto na mengineyo zaidi
inabidi ajiulize je yeye akifanyiwa hivyo kwa binti zake atafurahi? Anyway huyo dada naye atakuwa amemzoesha mimi wa kwangu nilimwambia clear
kabisa kabla ya ndoa kwamba alinitoa kwa wazazi na si juu ya mti so kama xmas naenda kwao easter ni kwetu zaidi ya hapo hakutaendeka kokote.
 
Back
Top Bottom