Je hii ni sahihi kwa Wanandoa hasa wanaume?

Je hii ni sahihi kwa Wanandoa hasa wanaume?

Habari za weekend
wadau wa jukwaa hili...

Kuna dada mmoja alikuwa anatusimulia baadhi ya maisha yake ya ndoa. Moja
kati ya mambo yaliyonigusa ni hili...

"Sitaki kuamini kama nilipitishwa nyumbani kwetu kama kituo cha polisi"

Ilikuwa ni nyakati za sikukuu za mwisho wa mwaka, familia ile ilifunga
safari kwenda Kijijini kwao nwanaume kama ilivyo ada kwa makabila
fulani.

Ukitaka kufika kijijini kwao na yule mume ilikuwa lazima upite kijiji
cha na yule dada, basi safari ikaanza toka Mjini, haoooo wakafika
Kijijini kwao na yule dada. Basi mdada akafikiri huenda wanaweza kupita
hata kwa dakika chache wakaisalimia familia ya yule dada.

Thubutuuuu... Mume alinyoosha mguu wakapitiliza mpaka kwao, mdada kwa
busara akafikiri huenda wangelipita wakati wa kurudi, holaaaa!!! Kama
kawaida mume akanyoosha mguu...

Mwisho wa siku mdada akamtolea uvivu na kumuuliza kulikoni hata asipite
kuwasalimu wazazi, ndugu na jamaa hata kwa muda mfupi?? Yule mume
akamjibu MIMI NDIYE MWENYE MAMLAKA YA KUAMUA KUKUBALI AMA KUKATAA uende
ama usiende kwenu kusalimia. Labda tu kuwe na jambo la muhimu.

SWALI KWENU WANANDOA. Je alichokifanya ni haki?

Mzee Mtambuzi, Babu Dark
City
, Babu Asprin,
watu8, kabanga,
EMT na wanandoa wanaume, je hivi ndivyo
mnavyowa treat wake zenu???

Dada mkubwa AshaDii,
gfsonwin, cacico,
BADILI TABIA, Fixed
Point
, snowhite,
mrsleo na wanandoa wanawake je ukifanyiwa hivi
utachukua hatua gani??

Karibuni kwa mjadala....

mshenzi sana sory.kama si mkurya?
 
Last edited by a moderator:
Yani usipite hata kusalimia? nadhani unatania...

Kwa namna hiki kisa kilivyosimuliwa mimi sioni kama kuna kosa lolote...

Msimuliaji hajaonesha hata mahali pamoja kuwa wanandoa hao walipanga safari ya kwenda kwa wazazi wa binti...

Basi mdada akafikiri huenda wanaweza kupita hata kwa dakika chache wakaisalimia familia ya yule dada.
 
Nyinyi jamani mnaongea tu. Kweli upite kwenu vuuuu tena ukute umeona wazazi wako waleee, afu usishuke kuwasalimia, seriously?? Hivi kumbe kuolewa ni kukana wazazi wako? Sawa hawakuwa na plan ya kwenda kwa wazazi wa msichana, basi wangeshuka wasalimie tu afu waendelee na safari yao kama walivyoplan. Hivi inawezekana mumeo awa-ignore wazazi wako afu wewe ndo ukawachekee wazazi wake??
 
Ni nini maana ya ndoa?
 
Huyo mwanaume hajiamini...
Kwake yeye unyanyasaji ndio kipimo cha uanaume wake...ukichwa wake wa familia...

Mapenzi si kuburuzana...kwa mtindo huu lazima huyu mke atakuwa anapewa amri hata kitandani..
Mwanaume aso na discussion na mkewe atawezaje ku make love?

Jamani kwenye kuolewa msikubali kuolewa na mume asiyekusikiliza ...utajutraaaa....
Kuna wale hata kama kitu ni positive atapinga tu kisa mke ndio amekigusia wa kwanza...ni shiiidaa...

Ila nawahurumia sana wanaume wa hivi...kupata msaidizi ni sawa na kumsukuma mlevi...wake zao wana fall kirahisi kwa yeyote aliye kinyume na waume zao...

Mke anataka kusikilizwa bana...hata kama una miela vipi, kama huko rude imekula kwako...

Asante dada mkubwa... Nimepata kitu hapa!
 
Kuachana na na wazazi; baba na mama na kujenga familia mpya/ kuishi pamoja...

Na kwa definition hiyo basi hata kwa wazazi wa mwanaume hawakupaswa kwenda...

Hiyo ni maana ambayo haijakamilika...

Mwanamke anapoamua kuolewa maana yake ni kwamba anakubali kuhamishwa kutoka milki moja kwenda milki nyingine...

Gharama ya uhamisho huu huambatana na malipo ya mahari na kwa makabila au jamii nyingi hufanyika sherehe ya kumuaga binti...

Pia kwa tafsiri nyingine ni kwamba mwanamke anapoolewa baba wa mwanamke huwa anauza madaraka yake na kumkabidhi mwanaume anayeoa, na ndio maana wakati wa tukio la ndoa baba humtembeza bintiye na kumkabidhi mwanaume mbele ya kadamnasi...

Sasa mila nyingi za kiafrika zipo hivi, mwanamke akishaolewa hana ruksa ya kurudi kwa wazazi wake isipokuwa awe amepewa kibali maalumu kinachoambatana na taarifa kabla...

Pia mwanaume hapaswi kwenda ukweni pasipo taarifa yoyote rasmi kwa wakwe zake...

Mimi ninachoona hapa ni huyo dada kutokuongea mapema na mume wake ili safari zote mbili zipangwe kwa kufuata protokali...
 
Si mke kukatazwa kwenda kwao kusalimia.kama vile akiolewa ndio ntolee??

Mbona katika maandishi yako hapo juu haioneshi hivyo?

Kwa namna ulivyoandika hapo juu haya ndio yalikuwa matamshi ya mume...

Yule mume akamjibu MIMI NDIYE MWENYE MAMLAKA YA KUAMUA KUKUBALI AMA KUKATAA uende ama usiende kwenu kusalimia

Sasa hebu nikuulize, je si kweli kuwa mume ndiye mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa....?
 
Du kwani ndoa ni utumwa au makubaliano vipi umfanye mwenzio mtumwa lol undugu wa mimi na wewe tumejuana kila mmoja ana meno 30 kisa kunizuia wazazi wangu siku mapenzi yakiisha sikubaliani na hilo hata kidogo mume nitasema alikuwa wangu lakini wazazi wangu ni wangu lazima niwape umuhimu
 
Hiyo ni maana ambayo haijakamilika...

Mwanamke anapoamua kuolewa maana yake ni kwamba anakubali kuhamishwa kutoka milki moja kwenda milki nyingine...

Gharama ya uhamisho huu huambatana na malipo ya mahari na kwa makabila au jamii nyingi hufanyika sherehe ya kumuaga binti...

Pia kwa tafsiri nyingine ni kwamba mwanamke anapoolewa baba wa mwanamke huwa anauza madaraka yake na kumkabithi mwanaume anayeoa, na ndio maana wakati wa tukio la ndoa baba humtembeza bintiye na kumkabidhi mwanaume mbele ya kadamnasi...

Sasa mila nyingi za kiafrika zipo hivi, mwanamke akishaolewa hana ruksa ya kurudi kwa wazazi wake isipokuwa awe amepewa kibali maalumu kinachoambatana na taarifa kabla...

Pia mwanaume hapaswi kwenda ukweni pasipo taarifa yoyote rasmi kwa wakwe zake...

Mimi ninachoona hapa ni huyo dada kutokuongea mapema na mume wake ili safari zote mbili zipangwe kwa kufuata protokali...

We jamaa umeongea mambo ya maana sana, hiki kizazi cha tamthlia na whatsap wanadhani ndoa ni kama kwenda kwa jirani kucheki muvi,sasa yeyote unaweza kurudi kwenu fasta kucheki kama maharagwe yamekaukia maji!

Na ndio maana ndoa zinawasumbua sana!
 
Huyo mwanaume ni mbinafsi tu na si muungwana.... inawezekana hana hata heshima kwa wakweze au mkewe

Ila mume umleavyo ndivyo atakavyokutreat...
 
Mimi naona jamaa yuko sahihi maana kama walikuwa hawajapanga kupita ukweni ingekuwa pia siyo vyema kuwashitukiza wakwe kwa ugeni usio na taarifa. Vip waibuke pale wakute nyumbani hakuna mtu? Mwanamke ndiye mwenye kosa. Kama angetaka kwenda kusalimia basi angemwambia mmewe mapema.
 
Nakwambia...huyu ameshajiandaa na ndoa ndoano...
Ningekuwa mimi asingepita kwetu...aaahhh
Kama noma na iwe noma...onyesha makucha asubuhi kweupe usisubiri jua kuzama...

Sijui ndio kujishusha wanakokusema...
Na wanajuaga kweli kuchagua mke wa kuoa...wanajua nani anakubali kuonewa...

Huyo mwanaume ni mbinafsi tu na si muungwana.... inawezekana hana hata heshima kwa wakweze au mkewe

Ila mume umleavyo ndivyo atakavyokutreat...
 
Wanawake(baadhi) tunalilia ndoa na kusahau mambo mengine ya msingi
Huyo mke si ajabu kukuta kabla hajaolewa alijua ubabe na kiburi cha mwanaume.....akaamua kuingia hivyo hivyo tena (inawezekana) kwa kujivisha utiifu na "u-hewala bwana" badala ya kuset grounds zake mapemaaaaaaaaaa

Hivi inagharimu nini kusalimia wakwe zake kwa muda wa dakika 20? Hilo nalo mpaka mwanaume uambiwe? Huyo mwanaume kichwa chake ni roboti hakina ubongo wa kufikiria?

Na ana bahati kwa mke alonae la sivyo..........

Back
Top Bottom