Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 13,044
- 25,790
Mastory ya bey
My people,
Kama ukipewa nafasi ya kuwa kitu kimoja tu maishani basi chagua kuwa mkarimu, ukarimu huleta mapenzi ya watu kwako,ukarimu humgeuza adui yako kuwa rafiki yako,ukarimu ndio ubinadamu wenyewe
Unaweza kuamua kuwa mtu wa kwanza kuwasalimia watu mara pale unapokutana nao, haikugharimu kitu chochote sana sana unavutia mapenzi kwako
Kuna kipindi fulani niliongazana na fundi fulani ambaye ni mgeni mazingira ya kwetu,aisee alinifundisha kitu,alikuwa anasalimia kila mtu ambaye anakutana nae,tena anasalimia kwa tabasamu kabisa,nilimkubali sana yule fundi
Unaweza kumfanya mtu atabasamu kwa sababu yako,hakika hilo ni jambo jema sana,siku zote wafanye watu wafurahie uwepo wako maishani mwao,iwe kazini,kwenye burudani,na popote pale ambapo utakuwa na watu pamoja
Unaweza kumlipia mtu nauli ya basi au kumnunulia kinywaji,kwako wewe unaweza ona ni jambo dogo lakini kwa mtendewa ni jambo kubwa sana kwake ambalo linabakia kwenye kumbu kumbu zake siku zote
Unaweza kumpisha mama mjazito kwenye siti ya daladala au mzee,au ukampakata mtoto mdogo ambaye mlezi wake amesimama kwenye daladala
Unaweza kumuelekeza mtu aliyepotea njia au kumfahamisha sehemu fulani ambayo anataka kuelekezwa
Kikubwa kadri ya uwezo wako jitahidi kuwa mkarimu kwa watu unao wajua na usio wajua,na hata kwa upande wa imani tunafahamishwa kwamba hakika watu wenye ukarimu wana thawabu zao kwa Mola wao
Siku zote jitahidi na azimia kuwa mwangaza kwa watu wengine
Ni hayo tu!