JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mastory ya bey​


Habar za kutwa nzima ya leo,ni usiku mwingine tena tunakutana katika kijiwe chetu

Leo nawapa siri ya kuupa ubongo wako code ambayo itaufanya ubongo wako ufanye kile ambacho unataka kifanyike au ubongo ufanye

Let me break this way for proper understanding,neno Asante au samahani ni code ambazo zimerithishwa kwenye ubongo wetu toka tukiwa watoto,hivyo tumeufundisha ubongo kwamba ukisikia neno Asante inaleta ridhiko la nafsi kwa yule anayeambiwa

Na tumeufundisha ubongo kwamba neno samahani linatumika kusawazisha mambo na kuyaweka sawa,ndio maana kama mtu akikuuudhi au kukukera akikwambia samahani chap tu hasira zinashuka na hali ya utulivu inatokea au inatawala

Nimetoa hiyo mifano miwili ambayo sote tunaijua ikiwa ni sehemu ya coding katika bongo zetu

Sasa unaweza kutafuta code maalumu halafu ukaufundisha ubongo maana ya hiyo code na baada ya muda fulani ikaleta matokeo

Bey anatumia code hii PERIOD kumaliza uzia kichwani kwake au kuyafutilia mbali mawazo ambayo yana mgasi gasi

Huwa kama jambo linanikera na nataka nimalizane nalo huwa nasema period hata ndani ya nafsi yangu kisha inakuwa imeisha hiyo
Mfano " jambo hili sitaki kuliwaza tena period" hapo nakuwa kama nimeweka mhuri wa moto kumaliza jambo hilo

Au kama napata stress kuhusiano na jambo fulani basi hujiambia AM OKAY na chap nakuwa sawa

Sasa haya mambo haya tokeo over night tu chap,bali inachukua muda kwa kutengeneza utaratibu wa kujiambia au kusema code fulani kwa kipindi fulani baada ya muda ubongo wako utaitambua code husika na kukufanyia kazi ile unayoitaka

Mfano huu ni sawa na hizi positive affirmations ambazo huwa nazileta hapa,ukizisoma mara kwa mara baada ya muda zinabadilisha namna unavyoyawaza na kuyaangalia mambo mbali mbali katika maisha yako

Ni muda muafaka Sasa kutengeneza code zako.
 
Back
Top Bottom