?𷠽
𷠽𴰼󞐊
*THE VALENTINE DAY*
____________________________

Historia na asili ya siku hii ni *Mt Padre Valentino Shahidi wa dini* huko Italia.

Mkuu wa dola ya kirumi alipiga marufuku vijana wa kiume kuoa kusudi muda wo wote wawe tayari kuitwa kwenda vitani.

Hivyo Vijana wakawa wanafanya mahusiano na wasichana kiholela bila kufunga ndoa, jambo ambalo Padre Valentino aliona ni kinyume cha maadili ya maisha ya kikristo.

Akawa anawahamasisha na kuwafungisha ndoa vijana hao kwa siri.

Hata hivyo mpango huo ukavuja na habari ikamfikia mkuu wa dola ya kirumi kwa vile ilifanyika kinyume na maagizo yake.

Padre Valentino alikamatwa kwa amri ya mkuu wa dola ya kirumi, mkuu huyo alimshinikiza padre Valentino aikane dini kama njia ya kuepuka na adhabu ya kifo kwa sababu ya kuvunja amri ya mfalme.

Padre alikubali kuchagua kifo kuliko kuikana imani ya dini yake na kwa ajili ya utetezi wa maadili ya maisha ya ndoa badala ya vijana kuishi na vimada tu.

Padre Valentino aliuawa kama shahidi wa dini na mtetezi wa maisha ya ndoa, February 14 katika kalenda ya maisha ya watakatifu ni siku ya kumbukumbu yake.

Kutokana na kanisa kuweka siku hiyo ya February 14 kuwa kumbukumbu ya wanandoa kutokana na jitihada za Padre Valentino, walimwengu wameitafsiri kama siku ya wapendanao bila kuzingatia mapenzi ni ya kindoa au la.

Ukweli ni siku ya wanandoa kujikumbusha na kurudia ahadi za maisha ya ndoa na kwa vijana na wasiofunga ndoa ni kuhamasisha kufunga ndoa na sio vinginevyo.

Tusome maisha ya Mtakatifu Padre Valentino shahidi, kuna mengi sijayaandika hapa tutajifunza ya muhimu kwa maisha ya umuhimu wa ndoa.

_*VALENTINE DAY SIO SIKU YA WAPENDANAO KWA DHANA YA KIDUNIA BALI NI SIKU YA WANANDOA NA KUHAMASISHA MAISHA YA NDOA*_

 
20190213_185145.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom