Msaada: Mtoto wa miaka miwili kukosa usingizi wakati wa usiku

Unforgettable

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
5,273
11,773
wapendwa za asubuhi,poleni na hongereni kwa majukumu ya familia zenu na ya kuijenga nchi nimekuja kwenu kuomba ushauri/msaada wa mtoto wa kiume umri miaka 2 na miezi 4 kukosa usingizi wakati wa usiku.

Mtoto ni mtundu na anapilikapilika nyingi mchana hivyo wakati wa usiku unategemea alale mapema lakini wapi inaweza fika mpaka saa 6 jicho jeupe na akitaka kulala anatumia nguvu sana kiasi cha kuomba maji kila baada ya mda mchache baada ya kujipigapiga kichwa kifuani kwako huku akijisukuma mfano wa kujibembeleza hata kwa lisaa na zaidi ili aweze kulala

Hili limekuwa changamoto hata kwa mzazi anaemlea sababu akianza kujisukuma anataka awe amekupanda juu yaani hakuna kulala,hivyo naombeni ushauri kwa wazazi/walezi,madaktari au yeyote aliyewahi kukutana na changamoto kama hii naombeni ushauri.Nafuatilia comments

Muwe na siku njema.
 
Peleka huyo mtoto shule aanze pilika na wenzie. Saa moja asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni akirudi na hana ham tena.

saa 2 usiku mpaka saa 4 ni kumsomesha a e i o u mpaka akili itamkaa sawa.

niamini hii ndio tiba mbadala.

Huu ushauri ukikufaa unaweza kunipa hata elfu 15 ya maji mtaani hali tete
 
Jifunze malezi. Unaposema mtoto mtundu inamaanisha hakuna malezi hapo, kama unamkataza mtoto kufanya jambo halafu anaendelea kufanya na unamchekea kisha unasema ni mtundu tafuta anayejua kulea akusaidie usije ukampoteza mtoto kimaadili. Charaza mtoto kwani mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
 
Miaka miwili anatakiwa acheze itakua utundu tu wa kitoto sio ubishi wala ukorofi. Fimbo hazisaidii mkuu. Na tatizo lake la kuleta uzi hapa ni usingizi sio utundu
Jifunze malezi. Unaposema mtoto mtundu inamaanisha hakuna malezi hapo, kama unamkataza mtoto kufanya jambo halafu anaendelea kufanya na unamchekea kisha unasema ni mtundu tafuta anayejua kulea akusaidie usije ukampoteza mtoto kimaadili. Charaza mtoto kwani mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
 
Jifunze malezi. Unaposema mtoto mtundu inamaanisha hakuna malezi hapo, kama unamkataza mtoto kufanya jambo halafu anaendelea kufanya na unamchekea kisha unasema ni mtundu tafuta anayejua kulea akusaidie usije ukampoteza mtoto kimaadili. Charaza mtoto kwani mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
hakuna sehemu nimesema nimeshindwa kulea/au namchekea mtoto ila nilichomaanisha ni michezo anayo yakutosha hivyo kama mzazi unategemea ikifika jioni mtoto awe amechoka alale mapema ila yeye halali hata kwa kiboko halali mpk nimekuja hapa ujue kachezea sana mboko mpk nimeona its too much
 
Jifunze malezi. Unaposema mtoto mtundu inamaanisha hakuna malezi hapo, kama unamkataza mtoto kufanya jambo halafu anaendelea kufanya na unamchekea kisha unasema ni mtundu tafuta anayejua kulea akusaidie usije ukampoteza mtoto kimaadili. Charaza mtoto kwani mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
Junior hacharazwi
 
itakuwa anawazuia kufanya mambo yenu na shemelaaaa haaaaaaaaaaaaaaa🤣 wengine wanasema mmoja wenu alikuwa na utundu huoo🤣

mzoeshe kusali kwa pamoja na kisha kuzima taaa huku mkijifanya mmelalaaaa
 
itakuwa anawazuia kufanya mambo yenu na shemelaaaa haaaaaaaaaaaaaaa wengine wanasema mmoja wenu alikuwa na utundu huo...
hapana mkuu wasiwasi wangu ni namna anavyotumia nguvu kupata usingizi.

3997982746_7f1b917078.jpg
 
hapana mkuu wasiwasi wangu ni namna anavyotumia nguvu kupata usingizi View attachment 2134744
Ukipata matibabu utuletee mrejesho.
Ninae wa miaka minne kasoro yupo hivyo tuilishampa dawa za usingizi hazikusaidia mpaka tumeamua kumtizama. Akiwahi kulala ni SAA tano, awe alilala mchana au hakulala, awe alienda shule au hakwenda yaani usingizi ni wa kutumia nguvu.
Na usipomuimbia na kumlaza kifuani atakesha mpaka SAA kumi ndio alale fofofo.
Ukimlazimisha kulala anajifunika analala halafu anakuvizia umesinzia anaamka anaendelea na shughuli zake humo ndani, atachoraaaa, ataandikaaaa, ataimbaaa, mwenyewe anakuambia anafanya mtihani wa ufundi, tunamuita injinia maana kwa kukorokocha yuko vizuri sana.
 
yaani na huyu wangu ni hivihivi sema yeye mpk aupate huo usingizi sasa atakaa hiyo style hapo juu ajisukumesukume kwenye kifua chako mpk jasho limtoke aombe maji
 
Back
Top Bottom