Jaji Warioba: Ripoti ya PAC ni dhaifu

Warioba apigilia msumari escrow




Posted Jumanne,Decemba2 2014 saa 8:56 AM

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.



Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.

Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.

“Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015.”

Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.

“Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu,” alisema.

Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.

“Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?”

Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... “Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?”

Waliopata mgawo

Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.

“Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

“Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki,” alisema.

Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika... “IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.

“Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.

“Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani.”

Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.

“Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida,” alisema.

Source; Mwananchi 2/12/2014

Sisi tunaomuamini huyu Mzee naona kama vile tutaanza kupoteza uelekeo.
 
Kwa hiyo Profesa Muhongo yupo sahihi? kwa nini Warioba hukujitokeza mapema kulisema hili?

Prof Muhongo ni muongo hayuko sahihi. Ili kujua nani anamiliki how much ni mpk re-calculation ifanyike. Kusema pesa zote ni za IPTL si sahihi pia (nimekusamehe hapa mzee warioba) kwani ni sawa na kusema kuwa hakukuwa na disputes btn tanesco na iptl ambayo ni wrong pia.
 
Kwa maoni ya Warioba kunahitajika kufanywe ajwari ,ili Zito na wenzake wajipange upya ,na zaidi ipatikane suluhu ya kutoonewa mtu na kuachwa mtu ,kila mtu abebe mzigo wake kwa haki.

Mambo ya kutoana kafara ili wengine wasalimike wakati huo umepitwa ,haki itendeke vinginevyo Zito nae achunguzwe kwa kukwepa na kuwakwepa wengine kama alivyodai Mh.Warioba ,utamhusishaje Waziri mkuu kwamba mambo akiyajua wakati Wizara ya fedha nayo hukuitaja wala kuihusisha isipokuwa madagaa wachache wasio na mapezi ya kuwavukisha kina kikubwa chenye mawimbi.

Zito achunguzwe,inaonekana kuna watu amewalinda.
 
Mikwara tuu; nchi hauwezi kusambaratika wala nini. Baadhi ya watu wanatumia excuse hiyo kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.Kama waliomleta Seth tayari wanajulikana nchi itasabaratikaje wakati wahusika wanajulikana? Kuna lipi jipya ambalo watu hawajui kuhusiana na Escrow?

In the modern era of technology na kupashana habari horizontally rather than vertically (ambavyo tulizoea huko nyuma) huwezi kusema kuwa nchi itasambaratika kwa kusambaa kwa habari. Kwa sababu tayari watu wengi wanajua in and out ya Escrow na wahusika wote na kilichotokea.

Kwa maana nyingine the problem is not about not having the information, but not acting on that information. Watu wana info zote; sema zinawafanya wajisikie sad for what is going on. They aren't angry yet.

As Malcolm X once said "Usually when people are sad, they don't do anything. They just cry over their condition. But when they get angry, they bring about a change." Ninachotaka kusema ni kuwa watu wanawajua wahusika almost wote. But they are just sad of what is happening.

They are not angry yet and, hence, they aren't about to bring any change. Ndo maana hata ukisoma maandiko ya watu juu ya hili sakata, wengi wanaonyesha kusikitika juu ya kilichotokea. They arent' angry.

But if you are sad you would like to keep things as they are. Just few things to fix na mambo yatakuwa fine as usual. Lakini kama ukiwa na hasira and really want to bring about change, then hutajali kama nchi itasambaratika. What you really want is change and change only, not repair the damn thing which have caused you loads of problems.

Ni sawa na a married woman aliyezaa na mumewe. Mume hasn't been performing well for a number of years now. He has left the woman unsatisfied. She is sad, but not angry with her husband kutomfikisha atakapo. She may want to stay with him by fixing the problem with him, but next next day she is all over him b'se he has done exactly the same thing he promised that he won't.

She is indecisive. She can't decide what to do. She doesn't know what will happen if she breaks up with him. She is scared to be alone. Will she find a man out there? She isn't sure. She has got kids to take care of na hii inamwongezea wasiwasi.

Hii imesababishwa na kuishi na mume wake kwa miaka mingi. He has been the only man in her life . She doesn't know how other men test like and she is afraid of testing them, just in case they end up testing like him. May be, they may want her just for sex, whilst she wants more in the relationship.

Lakini inaweza kufikia siku ambayo huyo mwanamke ataamka na kunusa kikombe cha cappuccino na kumwambia mumewe, enough is enough. My husband, you were magnificent, thank you very much for what you have done to me, including these children, but please we have to move on. We have got to have change.

It will be a heartbreaking divorce, but a divorce that has to be. Akishafikia stage hiyo, i.e. kuwa na hasira na ndoa yake hataogopa kama ndoa itasambaratika. Atasema potelea mbali liwalo na liwe. I have had enough. Na sitegemei mwanaume aka chama kuishi ninavyotaka. Au siyo everlenk?

Laiti watz wengi wangekuwa na mtazamo huu!
 
Last edited by a moderator:
Yale majina hayawezi kutolewa, familia ya Mkulu inatuhumiwa kuchukukua kwa niaba ya. ...., Pinda sio rahisi akapona kwenye hiyo orodha maana kuna tetesi kuwa Hizo pesa ndo zilimpa kiburi cha kuingia kwenye mbio za urais. Ndio maana hayo majina hayawezi kuonekana hata kwenye database ya benki husika.
 
Bado mimi naamini MENGI REGINALD ndiyo karufikisha hapa. Tutamkumbuka sana MUHONGO
 
Yale majina hayawezi kutolewa, familia ya Mkulu inatuhumiwa kuchukukua kwa niaba ya. ...., Pinda sio rahisi akapona kwenye hiyo orodha maana kuna tetesi kuwa Hizo pesa ndo zilimpa kiburi cha kuingia kwenye mbio za urais. Ndio maana hayo majina hayawezi kuonekana hata kwenye database ya benki husika.
Mbona WARYOBA kawabeba sana kwenye issue ya Katiba Mpya, mnashindwa nini kumuelewa kihusu ESCROW? Hakufurahishwa na ambavto majambazi ya kaskazini yalivyoungana kumchafua MHONGO.
 
CCM wanapata shida sana na huyu Mzee mpaka anawanyima usingizi - Go Warioba Mungu atakulipa!:wave:
 
Hili sakata Ni refu sana.......kama hii Nchi ingekuwa na uadilifu madhubuti hata Ikulu isingesalimika.
 
DAMU NI NZITO KULIKO MAJI, WARYOBA ametambua NDUGU zake wa Mara hawajatendewa haki na akina MBOWE, MNYIKA, OLESENDEKA(WOTE KUTOKA KASKAZINI). TUJIPE MOYO ndugu yangu Waryoba, bado tuna nafasi ya kuona ndugu zetu wanatendewa haki
 
CCM wanapata shida sana na huyu Mzee mpaka anawanyima usingizi - Go Warioba Mungu atakulipa!:wave:
Warioba ni mzee aliyekosa busara. Ila kwa hili kuna mahala namuunga mkono. Ile ripoti ya PAC ilikuwa inawalenga watu fulani. Ndo maana wakamuingiza na Maselle kwa makosa yasiyojulikana
 
alipokuwa dalali katikaa ofisi ya UMMA

Hilo kaonesha wazi kuwa hakufanya huo udalali na RITA ndiye alikuwa msimamizi wa shughuli za IPTL na ndiye aliwakutanisha mnunuzi na muuzaji wa hisa miaka kadhaa kabla ya Muhongo hajawa Waziri.

Tuwe wakweli, RITA hawajapinga hilo popote.
 
Warioba ni mzee aliyekosa busara. Ila kwa hili kuna mahala namuunga mkono. Ile ripoti ya PAC ilikuwa inawalenga watu fulani. Ndo maana wakamuingiza na Maselle kwa makosa yasiyojulikana
Weston Songoro -Join Date : 17th February 2014 - Wewe ukaye ukijua sio saizi ya Warioba kaa kimya!
 
Back
Top Bottom