Jaji Warioba: Ripoti ya PAC ni dhaifu

Prof Muhongo ni muongo hayuko sahihi. Ili kujua nani anamiliki how much ni mpk re-calculation ifanyike. Kusema pesa zote ni za IPTL si sahihi pia (nimekusamehe hapa mzee warioba) kwani ni sawa na kusema kuwa hakukuwa na disputes btn tanesco na iptl ambayo ni wrong pia.

Nauliza, ikiwa Re-calculation ingefanyika kati ya Tanesco na IPTL je, Utekelezaji wa maamuzi hyo ungetumika...Retrospective au Retroactive? Maana kama ungeanza kutumika Retrospective Pesa ya UMMA ipo katika ESCROW Acc. ikiwepo ya TANESCO, na TRA. Kama maamuzi yangeanza kutumika Retroactive Basi pesa katika Escrow Acc. siyo ya UMMA labda kodi ya TRA.
 
Katika michango yangu mingi kwenye hili swala la Escrow nimezungumzia sana kuwa hawa jamaa wamesurvive kwa vile repot ya PAC ilikuwa too weak. Pamoja na ushahidi kuwa overwhelming kuliko wa Richmond bado walishindwa kuja na report ya nguvu. Hiyo report ilikuwa ndiyo uwezo wao pamoja na kukesha. Niliwashangaa kuwakaribisha watu kama wakina Kingwang'ala badala ya design za akina Mwakyembe. Nawaelewa walitaka kupandisha profile yao kuwa vijana wanaweza but it backfired big time. FF aliiona mapema akatahadharisha watu lakini only few people understood her. Halafu kuna tu kesho atakuja dai eti Zitto ni presidential material ....................what a joke!!

With due respect mwanajamvi, kulinganisha report ya PAC na ile ya Mwakyembe ni sawa na kulinganisha embe na papai kwavile tu yote ni matunda. Siyo sahihi. Ya Mwakyembe ilikuwa kamati teule kwa ajili ya kufanya uchunguzi na uchambuzi, wakati ya PAC ilikuwa kupitia report ya CAG kwa niaba ya bunge!!
 
Unawezaje kuwatenganisha MWANANCHI NA ZITTO KABWE? Mimi naamini Raia Tanzania ndiyo wameandika ukweli wa aliyoyaema WARYOBA.
 
Nani kawalinda akina mbowe dola hii ya bongo, acha bange

Hivi kwa akili yako kabisa unaamini Mbowe ni tishio kwa Watawala,On the contrary wanamtumia kufanikisha mipango yao mingi.Mbowe na watawala (CCM) wanakula na kunywa pamoja usiku halafu anajifanya kutupigania sisi wanyonge wakati wa mchana.Usisahau pia kwamba Mbowe ni mfanyabiashara if you know warram mean!
 
Wakuu katika hali ya kushangaza Jaji Warioba ameikosoa ripoti ya kamati ya hesabu za serikali (PAC) na kusema kwamba haikutenda haki imewajumuisha watu wasiokuwa na makosa waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo na Katibu mkuu wa wizara hiyo E Maswi na kuwaacha watu waliokuwa na makosa na ambao walipaswa kuwajibika Wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.Ni wazi ripoti hiyo ya PAC ilitengenezwa kisiasa,Naomba fuatilia maelezo yafuatayo ya Jaji Joseph Warioba

Dar es Salaam
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.

Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.
"Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015."

Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.
"Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu," alisema.

Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.
"Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?"
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... "Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?"

Waliopata mgawo
Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.
"Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

"Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki," alisema.

Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika... "IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.
"Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.

"Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani."
Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.

"Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida," alisema.


CHANZO: MWANANCHI|Jumanne Decemba 2, 2014
 
Ahsante Baba Warioba kwa kusema ukweli na kukuweka huru, hapa inazidi kujidhihirisha ni kwa namna gani Kamati ya PAC ilivyotumika kuwapiga na kuwashambulia Mawaziri watendaji kwa shinikizo la pesa za kina Regnald Mengi, Nimrod Mkono na Edward Lowassa.

Shame on you Zitto Kabwe, Filikunjombe and your company
 
Ni kweli. Ripoti ile imewaehalilisha sana wabunge.
Ilikuwa ni ripoti ya MENGI kumsulubu Mhjongo, ripoti ya UKAWA kutaka kumrudisha ZITTO kundini na ZITTO kutaka huruma ya UKAWA, ripoti vita ya KANDA YA KASKAZINI vs KANDA YA ZIWA
 
Ahsante Baba Warioba kwa kusema ukweli na kukuweka huru, hapa inazidi kujidhihirisha ni kwa namna gani Kamati ya PAC ilivyotumika kuwapiga na kuwashambulia Mawaziri watendaji kwa shinikizo la pesa za kina Regnald Mengi, Nimrod Mkono na Edward Lowassa.

Shame on you Zitto Kabwe, Filikunjombe and your company
Ila kiukweli RAIS hawezi kubariki ujinga wa akina mengi, nchi haiwezi kuendeswa na remote ya wafanyabiashara matajiri
 
With due respect mwanajamvi, kulinganisha report ya PAC na ile ya Mwakyembe ni sawa na kulinganisha embe na papai kwavile tu yote ni matunda. Siyo sahihi. Ya Mwakyembe ilikuwa kamati teule kwa ajili ya kufanya uchunguzi na uchambuzi, wakati ya PAC ilikuwa kupitia report ya CAG kwa niaba ya bunge!!

Mkuu siyo kwamba tunalinganisha hizo report mbili (PAC na Mwakyembe). Nilichosema ni weakness kubwa walioionyesha katika report yao. They are too naive .............. !! Kama kulikuwa na mapungufu kwenye report ya CAG wao walitakiwa wayaone hayo na kuyawasilisha bungeni au kumuhoji CAG. Naamini wangekuja bungeni na kusema report imekuja na A, B, C lakini tumegundua kuna mapungufu fulani hivyo tunaomba muda kutavuta evidence zaidi au kuwahoji watu fulani kwanza, nafikiri bunge na wananchi wangekubali kuvuta subira. Perhaps ingeweza kuwapa mwanya wa tume kama ya Mwakyembe kuundwa. Where they went wrong ni kutuaminisha kuna kesi ambayo haikuwa na backing ya kutosha. Ndiyo maana in the end wao wenyewe walikubaliana na ushauri wa mtu kama Chenge ambaye ni muhusika kwa namna fulani. Ukitaka kuona how weak they were angalia kwa nini mapendekezo yao yote yamebadilishwa!!??

By the way, hivi akina Chenge and the likes ambao walikuwa kwenye mgao wa Ruge walihojiwa na PAC ............... if not why??
 
Ilikuwa ni ripoti ya MENGI kumsulubu Mhjongo, ripoti ya UKAWA kutaka kumrudisha ZITTO kundini na ZITTO kutaka huruma ya UKAWA, ripoti vita ya KANDA YA KASKAZINI vs KANDA YA ZIWA

Kwa mtu mwenye akili ndogo kama kuku anaeumwa kideri kuwaza haya ni sawa! Ila pole sana ungekuwa umepungikiwa damu ningejitolea lakini umepungukiwa akili nakuhurumia!
 
Ripoti na michango ya wabunge ingesisitiza Ikulu na Rais walivyohusika kwenye huu wizi. Nadhani hao ccm wangesahau hata wazo la kutaka kumuokoa Waziri mkuu.
Ipo siku wezi wetu tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Hakika Pinda na Mr. Dhaifu siku yenu ipo jikoni.
 
Ahsante Baba Warioba kwa kusema ukweli na kukuweka huru, hapa inazidi kujidhihirisha ni kwa namna gani Kamati ya PAC ilivyotumika kuwapiga na kuwashambulia Mawaziri watendaji kwa shinikizo la pesa za kina Regnald Mengi, Nimrod Mkono na Edward Lowassa.

Shame on you Zitto Kabwe, Filikunjombe and your company

Ni kweli mkuu mm nachompendea warioba huwa anasimamia ukweli katika hili Prof Muhongo na wenzake wanakandamizwa kisa vitalu vya gesi
 
Raia Tanzania, leo jumanne trh 02/12/2014

WARIOBA: RIPOTI YA ZITO DHAIFU, NGELEJA KAHUSIKAJE ESCROW?

Waziri mkuu na makamu wa pili wa rais wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema ripoti ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) chini ya Kabwe Zitto kuhusu akaunti ya tegeta Escrow ilikuwa dhaifu, yenye kuendeleza tabia ya kulindana.

Zaidi ya hapo, Jaji Warioba alisema kwa namna fulani Bunge la Jamhuri ya Muungano limeingilia uhuru wa mihimili mingine kutokana na maazimio yake.

Akizungumza na Raia Tanzania ofisini kwake jijini Dar es salaam, Jaji Warioba alisema ripoti ya PAC imeacha maswali kadhaa bila majibu.
"Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza, taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya fedha na tatu ni yale yanayohusu Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema katika mjadala wa sakata la Escrow Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa licha ya kwamba ndio wahusika wakuu wa hasara inayojulikana.

" Katika mawasiliano yote (kuhusu utoaji fedha Escrow) Waziri mkuu walimuingiza kwa kusema alikuwa akipata nakala za barua lakini wizara ya Fedha ilihusika katika mawasiliano na wameachwa" alisema Warioba.

Yafuatayo ni maelezo ya kina ya Jaji Warioba:

IPTL NI MZIGO

"Nataka nizungumzie mchakato wa Escrow, kwanza, IPTL imekuwa mzigo kwa nchi kwa muda mrefu tangu kampuni hiyo ilipoundwa, imekuwa na matatizo mengi. Katika kipindi hicho nchi imepoteza fedha nyingi kupitia kesi zilizotokana na IPTL ".

Nimesikia kwenye bunge kampuni moja ya wanasheria imelipwa sh.bilioni 62 lakini haikuwa peke yake, katika kesi hizo kulikuwa na gharama za TANESCO kwa kuwa walikuwa wakipeleka watu na kulikuwa na gharama za serikali, kwa hiyo fedha zilizotumika kwa migogoro hii ni nyingi.

"Katika utendaji wenyewe kulikuwa na matatizo, kwa hiyo nadhani ni jambo jema kwa sababu ya tatizo lililotokea lizungumzwe kwa undani ili kumaliza matatizo ya IPTL, tusiendelee nayo na gharama zake kwa nchi..
Kwa hiyo kulipeleka bungeni ilikuwa ni jambo zuri na limezungumzwa na ninaamini baada ya mchakato huu tutafika mahali tumalize matatizo ya IPTL na kuendelea na shughuli zingine za uchumi" alisema Warioba.

MAMBO MATATU MUHIMU

Warioba alisema hadi suala la IPTL linafikishwa bungeni na kisha kupatikana kwa maazimio ya Bunge kuna mambo matatu yameongoza mjadala:

La kwanza, ni wananchi, wananchi walikuwa na hamu ya kusikiliza mjadala Hui na kuona matokeo yake ni nini. Yalipokuwa yakitokea matatizo kama vile ya umeme, walikuwa wakilalamika kwa kuwa walitaka wafuatilie kwa ukaribu sana.

Hili kwa kiwango kikubwa naweza kusema ni kama vile imani ya wananchi kwa uongozi, hivyo kwa kila jambo linalotokea likiwahusu viongozi, wananchi wanakuwa makini kuona ni nini kitatokea. Hivyo bunge lilipokuwa likizungumza walijua kwamba wananchi wanatarajia kutatokea uamuzi mzito na si mazungumzo tu.

La pili, ni kwamba tunazungumza wakati huu ni kama wahisani wamesimamisha misaada kwa serikali na hata katika mjadala wengine walitaja hilo, kwamba limetuletea matatizo nchi sasa haipati misaada, kwa hiyo walipozungumza walijua kuwa wahisani walitaka waone matokeo ya hilo.

La tatu, nadhani ni siasa kwa kiwango kikubwa. Tunaingia katika kipindi cha uchaguzi, kwa hiyo vyama vinatafuta mambo ya kampeni kwa pande zote mbili, chama tawala na vyama vya upinzani. Nina hakika hili litaendelea kuwa jambo litakalozungumzwa wakati wa kampeni, kwa hiyo mazungumzo yote, huo ndo ulikuwa msingi wake.

FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI?

Mazungumzo yalivyokwenda utaona kubwa ambalo ndilo msingi wa uamuzi uliofanywa na bunge ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa mali ya umma na ndivyo wananchi wamefanywa waamini hilo lakini hakuna palipothibitishwa kuwa ni za umma. Msingi wa Escrow ni kwamba pande hizi mbili hazikuwa zikikubaliana kuhusu capacity charge, hivyo kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana waliona wawe na utaratibu, kwanza waendelee kushauriana wao wenyewe au kwenye mahakama ya nje; lakini kwa kipindi hicho kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana, iliafikiwa kuwe na mpango wa kuweka fedha mpaka watakapofikia makubaliano. Katika kipindi chote hicho IPTL ilikuwa ikitoa huduma, kwa hiyo kwa vyovyote vile ilikuwa na haki ya kulipwa capacity charge watakapokubaliana.

Hivyo kilicho cha uhakika katika fedha zile ni kwamba, zipo za capacity charge, hawakufika mahali waseme ni kiasi gani, lakini kwa kuwa sasa wanakwenda kuchunguza nina hakika mwisho itaonekana sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa ni za capacity charge", alisema warioba.

Hata hivyo, wananchi wamefanywa waamini kwamba fedha zote zilikuwa ni za umma, hilo ni mwelekeo wa kisiasa. Ni sawa wamefikia hapo, kama wameamua kwa msingi huo, wanasema kuna watu ni lazima wawajibike kwa hasara ambayo nchi imepata.

VIPORO VYA MASWALI

Jaji Warioba alisema mchakato huu wa IPTL na akaunti ya Escrow umeacha maswali kadhaa.:

" Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza , taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya ya Fedha na tatu ni yale yanahusu Wizara ya viwanda na biashara.

" Hasara inayotajwa kwa uhakika ilikuwa inahusu kodi inayotokana na mauzo ya hisa na hiyo si strictly ya Escrow ni kodi ya mauzo ya hisa , kwa namna ya capital gains tax na stamp duty. Wanaohusika hasa ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na pia wizara ya viwanda kwa maana ya Brela.

"Katika mjadala huu inaonekana kama wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa na huko ndiko yametokea matatizo ya hasara inayojulikana. Nimesoma taarifa ya PAC, wakifika kwenye wizara ya fedha, wanasema PAP kwa kushirikiana na maofisa wadogo wa TRA walofanya dhambi hii, sasa ni kama wanataka kuilinda Wizara ya Fedha. Katika mawasiliano yote Waziri Mkuu walimuingiza kwa kusema alikuwa akipata nakala za barua kakini Wizara ya Fedha ilihusika kabisa katika mawasiliano na wameachwa.

Brela wamefanya uzembe kwamba, unaweza kuandikisha kampuni na watu wakatia saini na majina hayapo, unaona kulikuwa na kasoro lakini haikuguswa. Kwa hiyo licha ya kuwa wameamua kuchagua watu waliohusika, inaonekana walikwenda mahali pamoja na huku kwingine wamewalinda.

Wamewalinda viongozi wa wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda, wakati vitendo vilivyosababisha hasara ya kodi kupatikana vimetendwa katika wizara hizi. Nijachouliza hapa ni kwa nini hawakutajwa, kuna element ya kulindana.

La pili linaloonekana kwamba kuna kulindana ni kwamba, waliopokea fedha kutoka kwa Rugemalira (James) wote wametajwa. Akaunti ya Rugemalira imetajwa katika benki ya mkombozi na hao wametuhumiwa lakini wanaohusika na fedha zilizotolewa stanbic bank , ambazo kamati inasema zilichukuliwa kwenye mifuko ya rambo, lumbesa na kwenye magunia, hawakutaja ni nani alichukua.

"Kwa sababu kama wanajua zilichukuliwa kwa njia hiyo, lazima watakuwa wanajua ni nani alichukua. Hivyo ni kwa nini hao waliochukua upande huu hawakutajwa? Unaaanza kuwa na maswali kuwa hapa kuna dalili za kulindana na wameendelea hivyo na kutoa uamuzi.

"Umuzi ule ni kama wa mahakama, bunge limekaa na kuamua kwamba fedha hizi na hasa alizolipa Rugemalira zilikuwa chafu na wote waliopokea fedha hizo walizipokea zikiwa chafu, hivyo na wao waadhibiwe. Wana ushahidi gani? Hawakuwasikiliza wale watu. Unasema kuna askofu amepewa fedha umuhukumu kwamba alijua kuwa ni fedha chafu, kuna jaji hapa alipata fedha unasema alijua ni fedha chafu, kuna Waziri alichukua fedha unasema alijua kuwa ni chafu, lakini hawakuwasikiliza.

" Kwa hiyo, wamehukumu bila kuwasikiliza na wamependekeza hatua za kuchukua. Baadhi yao wamesema wachukuliwe hatua za kinidhamu na wengine walipe kodi. Najiuliza kama askofu amepewa fedha, unasimama kwenye bunge unasema ajiandae kulipa kodi, najiuliza hivi ni mara ya kwanza kwa wao na watu wengine kupata fedha za aina hii? Mbona viongozi hao hao wanatoa misaada tena mikubwa na mahali pengi, mamilioni hatujasikia wakisema waliopewa walipe kodi.

" Hivi tuna uhakika gani kwamba hizi site zinazochangwa ni halali? Kwanini hawa ndio walipe kodi lakini zinazotolewa na wanasiasa husemi zilipiwe kodi.
Nadhani bunge halikutumia madaraka yake sawasawa. Unamwambia rais aunde tume ya kuwachunguza majaji walipata fedha, anaunda tume kwa msingi gani?

"Kwa sababu sheria inasema yakiwapo malalamiko kuhusu jaji, rais ataunda tume. Sasa hapa bunge linampelekea malalamiko gani yatakayomfamya aunde tume. Bunge lina ushahidi gani kwa sababu halikuwasikiliza ili kusema kuna malalamiko? Hilo nadhani bunge limeingilia mambo yasiyolihusu, ingekuwa haki kwamba hujatamka hatua gani zichukuliwe wangepata maelezo kutoka kwa wote wanaohusika ndipo ubaini kama kuna shaka ndipo uchukue hatua.....

Na Ester Mvungi, Dar es salaam
 
NDIYO WARYOBA ajue sasa kwamba hao washirika wake hawana nia njema na taifa hili.
 
Back
Top Bottom