Jaji Warioba: Ripoti ya PAC ni dhaifu

win8

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
926
500
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.

Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.

“Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015.”

Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.

“Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu,” alisema.

Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.

“Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?”

Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... “Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?”

Waliopata mgawo

Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
give credit were credit is due

the basis of PAC report is from respectively CAG and TAKUKURu reports

if there's any weakness why blame it on PAC

warioba wants us to believe he's the only one in Tz who can do a job better lol

huyu babu kenge kweli

What credit ....................!? The guys have failed the Nation!!

If there were no enough evidences why sniffing around trying to implicate innocent people. They should have told CAG and PCCB that their evidences were baseless instead of pushing for things which were not there ................. what they were trying to do was character assassination instead. Those dudes had their own motives which we should be asking ourselves .................... what!?

I will say it again and again, if CAG and PCCB reports had no concrete evidences smart people could have seen that and told the nation the whole truth instead of trying to put the nation in a stand still!!

We should all agree these guys are not as smart as think ............... That should be their biggest lesson. And people should stop overrating these dudes ................. they will take us nowhere!! Their time is yet to come!!
 
Mpanzi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
785
500
Nani kakudanganya?

Nionavyo, ndiyo kwanza yameanza. Kumbuka hilo.

“Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.

“Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani. (Judge Warioba)
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,265
2,000
give credit were credit is due

the basis of pac report is from respectively cag and takukuru reports

if there's any weakness why blame it on pac

warioba wants us to believe he's the only one in tz who can do a job better lol

huyu babu kenge kweli

pcca bado wanafanya uchunguzi.cag kazi yake ilikuwa mbovu na haijitoshelezi,walishndwa kuonesha pesa za nani.pac walitakiwa kuona mapungufu yote na kulieleza bunge.hata hvyo ilikuwa mapema kufanya hitimisho na kuhukumu, ilitakiwa isubiriwe full report ya pcca.tukubali,hapa ajenda alikuwa muhungo,maswi,werema na tiba.hii ni hujuma na bunge linatumiwa vibaya na wafanyabiashara,ufanyike uchunguzi.
 
nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,274
2,000
Katika michango yangu mingi kwenye hili swala la Escrow nimezungumzia sana kuwa hawa jamaa wamesurvive kwa vile repot ya PAC ilikuwa too weak. Pamoja na ushahidi kuwa overwhelming kuliko wa Richmond bado walishindwa kuja na report ya nguvu. Hiyo report ilikuwa ndiyo uwezo wao pamoja na kukesha. Niliwashangaa kuwakaribisha watu kama wakina Kingwang'ala badala ya design za akina Mwakyembe. Nawaelewa walitaka kupandisha profile yao kuwa vijana wanaweza but it backfired big time. FF aliiona mapema akatahadharisha watu lakini only few people understood her. Halafu kuna tu kesho atakuja dai eti Zitto ni presidential material ....................what a joke!!

Kumbuka PAC walikuwa wanafanyia kazi ripoti ya CAG na TAKUKURU sio kma ile ya akina Mwakyembe. Pengine PAC wangepewa jukumu zima la kuchunguza kashfa ile basi mambo mengi yangeibuka.
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
Ha ha ha ha ha haaaaaah, mkuu wengine wanachangia kwa kukurupuka bila kuangalia maudhui ya thread

Nakubaliana na wewe 100 %!! Kuna watu humu jamvini mpaka wanatia wasiwasi .................. sijui walisomea wapi!! Kwa mtu mwenye uelewa wala hatakiwi kusoma contents za hilo gazeti kwa kuwa title iko very clear.
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,559
2,000
Palikuwa na hoja ya msingi sana mwanzo wa hili sakata kama ilivyotolewa na Kafulila, Alipoingia Zitto na timu yake ya PAC, na hasa ile report yao, ilionyesha kabisa report inabagua nani wa kutoka/kuwajibishwa na nani wa kuachwa

Nilizungumzia triangle ya Zitto, Mkono na Mengi, kabla ya Prof Muhongo hajajibu zile hoja za PAC na watu wengi walishindwa kunielewa na bado hawataweza kuilewa hiyo Triangle, kwa kifupi Report ya PAC imeandikwa kwa kufuata behind agenda za Mengi. kwa kutumia uwezo wake wa kifedha na vyombo vyake vya Habari Mengi ndio kainfluence sana hiyo Report ya PAC

Tiangle na wengine waliokuwa pembezoni wanataka sana kuimiliki Wizara ya Nishati na MAdini, ndio wizara pekee ambayo watu walikuwa wanapiga pesa isiyokuwa na control, pamoja na mapungufu yake ya hapa na pale, Prof Muhongo na timu yake ya watendaji wameleta mabadiriko makubwa sana ndani ya hiyo Wizara, watu sasa wanashindwa kupenyeza Mirija yao na njia pekee ya kuimiliki hiyo wizara ni kumtoa Prof Muhongo na watu wake ili watu waendelee na michezo yao michafu

Hili Sakata la ESCrOW bado halijaisha
 
samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,551
2,000
Tusisahau wajumbe 19 wa PAC walikua MaCCM.. anyway unaweza kumtoa Filikunjombe hapo wanabaki 18, report lazima ingezingatia uchama
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,321
2,000
yaani kwa jinsi navyo ona mara nyingi unavyocomment it is 100 % ni msukule wa kisiasa,, misukule ya kisiasa huwa very limited katika uwezo wa ku accept maoni ya wengine hasa kinzani

Hongera sana kwa kuliona hilo mkuu, ila tu kwa kukusaidia ni ww na wanalumumba wenzako ndio wenye utahira huo
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
Kumbuka PAC walikuwa wanafanyia kazi ripoti ya CAG na TAKUKURU sio kma ile ya akina Mwakyembe. Pengine PAC wangepewa jukumu zima la kuchunguza kashfa ile basi mambo mengi yangeibuka.

Mkuu amini nakwambia, it would not have made any difference!! Hapo ndiyo uwezo wao ulipoishia .................. kama wangekuwa smart enough wangeliona weakness wa hizo reports. Kazi yao haikuwa kusoma reports na kuzisummarize .................... walitakiwa kuwahoji wahusika na kama kuna ushahidi waliuhutaji wangeliuomba!! They had all the powers but they did not know what to do more!!
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,265
2,000
nilishawahi kusema na narudia tena, delivery ya PAC ilikua below standard, ilikua ya kitoto mnoo, nilitegemea nisimame kwenye kiti lakini ilikua kama kawimbo tu kakunilaza, hamna kitu pale, zito jitahidi kua mwandishi mzuri wa hotuba,

WATU WACHACHE HUMU WENYE AKILI KAMA WEWE.SOMETIMES HUWA NAWAKUBALI WANAMEMBA KUWA NI GREAT THINKERS LAKINI WAKATI MWINGNE NAWAONA KAMA BAADHI WANA JAZIBA SANA!HUWEZI KUWA RATIONAL UKIRUHUSU AKILI YAKO IKATAWALIWA NA JAZIBA.NI KWELI REPORT ILIKUWA SHALLOW,ORGANIZATION MBAYA,PRESENTATION MBOVU.AKILI NDOGO ILITUMIKA.
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,321
2,000
Hivi mtaendelea kudanganyika na usafi bandia wa Mbowe mpaka lini?ZZK na Mbowe wote wanahusishwa na kadhia hii ya ESCROW, Kufa kwa kashfa ya ESCROW ndiyo kupona kwake kisiasa!

Nani kawalinda akina mbowe dola hii ya bongo, acha bange
 
NINAHASIRA

Member
Nov 5, 2010
58
0
Katika michango yangu mingi kwenye hili swala la Escrow nimezungumzia sana kuwa hawa jamaa wamesurvive kwa vile repot ya PAC ilikuwa too weak. Pamoja na ushahidi kuwa overwhelming kuliko wa Richmond bado walishindwa kuja na report ya nguvu. Hiyo report ilikuwa ndiyo uwezo wao pamoja na kukesha. Niliwashangaa kuwakaribisha watu kama wakina Kingwang'ala badala ya design za akina Mwakyembe. Nawaelewa walitaka kupandisha profile yao kuwa vijana wanaweza but it backfired big time. FF aliiona mapema akatahadharisha watu lakini only few people understood her. Halafu kuna tu kesho atakuja dai eti Zitto ni presidential material ....................what a joke!!

Yah ni ukwe;i mtupu! point kaka!
 
kidole007

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
3,094
2,000
What credit ....................!? The guys have failed the Nation!!

If there were no enough evidences why sniffing around trying to implicate innocent people. They should have told CAG and PCCB that their evidences were baseless instead of pushing for things which were not there ................. what they were trying to do was character assassination instead. Those dudes had their own motives which we should be asking ourselves .................... what!?

I will say it again and again, if CAG and PCCB reports had no concrete evidences smart people could have seen that and told the nation the whole truth instead of trying to put the nation in a stand still!!

We should all agree these guys are not as smart as think ............... That should be their biggest lesson. And people should stop overrating these dudes ................. they will take us nowhere!! Their time is yet to come!!

try to use a bit of common sense which is not common

the allegations themselves were enough to hold AG and his compatriots accountable, so many fraud involved under their respective offices ; illegal money laundry, tax ovation to mention few

where is they're innocence's

PAC did what was to be done its now up to Govt
 
Gwalihenzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
5,126
2,000
nilishawahi kusema na narudia tena, delivery ya PAC ilikua below standard, ilikua ya kitoto mnoo, nilitegemea nisimame kwenye kiti lakini ilikua kama kawimbo tu kakunilaza, hamna kitu pale, zito jitahidi kua mwandishi mzuri wa hotuba, ulichemsha.
Wewe unafikiri kwa tumbo, huna lolote la maana unaloweza kusema likaeleweka!
 
nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,274
2,000
Mkuu amini nakwambia, it would not have made any difference!! Hapo ndiyo uwezo wao ulipoishia .................. kama wangekuwa smart enough wangeliona weakness wa hizo reports. Kazi yao haikuwa kusoma reports na kuzisummarize .................... walitakiwa kuwahoji wahusika na kama kuna ushahidi waliuhutaji wangeliuomba!! They had all the powers but they did not know what to do more!!

Huo mda usingepatikana kuwahoji watu wote, wewe kumbuka figisu figisu zilizokuwa zimeshaanza mambo yangeharibikia njiani maana na bunge lilikuwa linamaliza muda wake so jamaa wamejitahidi kiasi chake lakini kumbukeni chanzo cha haya yote ni pale state house
 
Gwalihenzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
5,126
2,000
Warioba apigilia msumari escrow
Posted Jumanne,Decemba2 2014 saa 8:56 AM

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.

Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.

"Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015."

Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.

"Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu," alisema.

Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.

"Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?"

Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... "Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?"

Waliopata mgawo

Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.

"Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

"Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki," alisema.

Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika... "IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.

"Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.

"Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani."

Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.

"Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida," alisema.

Source; Mwananchi 2/12/2014
 
Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,129
2,000
warioba+px.jpg

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA

Dar es Salaam
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.

Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.
"Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015."

Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.
"Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu," alisema.

Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.
"Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?"
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... "Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?"

Waliopata mgawo
Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.
"Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

"Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki," alisema.

Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika... "IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.
"Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.

"Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani."
Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.

"Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida," alisema.

CHANZO: MWANANCHI|Jumanne Decemba 2, 2014
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
try to use a bit of common sense which is not common

the allegations themselves were enough to hold AG and his compatriots accountable, so many fraud involved under their respective offices ; illegal money laundry, tax ovation to mention few

where is they're innocence's

PAC did what was to be done its now up to Govt

You are the one who is failing to use common sense here .................... unfortunately, you can't see that either!!

We're not talking about allegations here, we needed evidence up front. They could be thieves and we all agree that but they needed to prove that beyond that. All what happened was the result of the peer pressure from the public that's why the Bunge has to come up with something. In case they felt they did not have enough time they could have asked for more ............... in short your defense does not add up!!
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,820
2,000
Kumbuka PAC walikuwa wanafanyia kazi ripoti ya CAG na TAKUKURU sio kma ile ya akina Mwakyembe. Pengine PAC wangepewa jukumu zima la kuchunguza kashfa ile basi mambo mengi yangeibuka.

Kwa nini walishindwa kuona mapungufu kwenye hizo report!!??

Tatizo walichokifanya wameendana na emotions za public. Walichukwa wanataka kufanya ni kuplease public and perhaps to gain out of it ................ politically!! It's backfired!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom