Jaji Warioba: Ripoti ya PAC ni dhaifu

Jaji Warioba: Ripoti ya PAC ni dhaifu

Huyu mzee nae na miaka yake 89 anatafuta kwa kutokea badala ya kupumzika!
 
Kama ni ya uongo kwa hiyo wewe unataka kusema nini sasa wote tulisikiliza na kuisoma,ni mtazamo wako na wake ila mimi naamini ni ya ukweli.
 
Huyu mzee nae na miaka yake 89 anatafuta kwa kutokea badala ya kupumzika!
Mkuu, soma vizuri, mwandishi ndio kamfuata ofisini kwake na kumtaka atoe comments zake, nimeona niweke record sawa, tukimlaumu kwa hilo tutakua tunamkosea mzee wa watu.
 
Warioba amesema ripoti dhaifu na kauonyesha udhaifu wake ila swala la uongo hakuzungumza ukweli pamoja na ufisadi uliofanyika pac ni kama iliwalenga baadhi ya watu na kuacha wengine ndio maana wengine tunashangaa kwanini gavana hakuguswa waliopokea pesa za stanibic hawasemwi
 
Alichosema Warioba ukikitazama kwa jicho la tatu kuna element ya watu kuwalinda wale "Wa kwao".
 
Haiingii akilini kumuacha gavana wa benki kuu bila kuwajibika kwa sakata hili; huu ni udhaifu mkubwa katika ripoti ya PAC!!
 
Report dhaifu au report ya uongo,

Mkuu,
Hii repoti ni dhaifu sana ambapo ndani yake ina element za uongo ndiyo naana wajuzi wa kanuni za bunge na taratibu za kisheria wanaichambua na kuichana chana kihoja.

Kwenye masuala ya Kanuni na sheria, hakuna emotions.

PAC wamelijongea suala hili wakiwa wamejaa ndani ya vifua vyao emotions huku wengine wakiwa wameishatoa hukumu kabla hata ya kusoma repoti ya CAG au kusikia maoni ya TRA na TAKUKURU.

Ndiyo maana hata mahakamani, pale mtu anapokutwa na makosa, mahakimu au mahaji huwa wanahitaji muda zaidi wa kufikiria kutoa adhabu ili kuepukana na emotions zinazotokea wakati wa uwasilishaji wa evidence na marumbano ya sheria.
 
Mods unganisheni huu uzi

Mkuu,
Unataka MOD's waunganishe wapi?.

Hutaki wanaJF waeleze mapungufu ya PAC katika kufikia mapendekezo yao?.

Haki na usawa ni pamoja na kusikia kila ambacho hupendi kukisikia.

Tuvumilie kwa sababu kama taifa tumeamua kufuata msingi wa usawa katika kusikia na kusikiliwa ili kufikia makubaliano au kukubali kutokubaliana.
 
Nimeridhishwa sana na uchambuzi wa Mzee Warioba. Haki ingeonekana imetendeka kama Watu wote hasa wale wote waliobeba Fedha taslimu kutoka stanibic banki. Hakuna hata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina. je haukuwepo na uwezekano wa kuilazimisha benki kisheria kuipatia PAC taarifa za waliolipwa ? Hasa ikitiliwa maanani kuwa kiwango cha fedha zilizotolewa ni zaidi ya bilioni 75. Kosa la Mkombozi benki hasa ni lipi? Kama mmiliki wa VIP engineering alikuwa mmiliki halali wa hisa 3, Je kuna mashaka kuhusu umuliki wa hisa hizo? Je kuna mashaka kuhusu uuzaji wa hizo hisa? Au kuna mashaka kuhusu bei aliyolipwa? Je, kuna mashaka kuhusu ukokotoaji wa kodi aliyotakiwa kuilipwa na VIP? Kama jibu ni ndiyo ni kiasi gani cha kodi kilichokwepwa?Ni lini muuuzaji akapata fursa ya kumhoji mnunuzi uhalali wa fedha anazolipa? Ni lini kasisi akahoji muumini uhalali wa zaka anazozitoa ? Taratibu za kutoza kodi viogozi wa dini kutokana na zaka umeanza lini ? Vigezo vya kodi hizi ni vipi?Hakika taarifa ya PAC imetolewa kwa ushabiki kwa faida ya nani? Ni udhaifu wa kawaida au kuna malengo ambayo hayajawa wazi?
 
Raia Tanzania, leo jumanne trh 02/12/2014

WARIOBA: RIPOTI YA ZITO DHAIFU, NGELEJA KAHUSIKAJE ESCROW?

Waziri mkuu na makamu wa pili wa rais wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema ripoti ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) chini ya Kabwe Zitto kuhusu akaunti ya tegeta Escrow ilikuwa dhaifu, yenye kuendeleza tabia ya kulindana.

Zaidi ya hapo, Jaji Warioba alisema kwa namna fulani Bunge la Jamhuri ya Muungano limeingilia uhuru wa mihimili mingine kutokana na maazimio yake.

Akizungumza na Raia Tanzania ofisini kwake jijini Dar es salaam, Jaji Warioba alisema ripoti ya PAC imeacha maswali kadhaa bila majibu.
"Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza, taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya fedha na tatu ni yale yanayohusu Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema katika mjadala wa sakata la Escrow Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa licha ya kwamba ndio wahusika wakuu wa hasara inayojulikana.

" Katika mawasiliano yote (kuhusu utoaji fedha Escrow) Waziri mkuu walimuingiza kwa kusema alikuwa akipata nakala za barua lakini wizara ya Fedha ilihusika katika mawasiliano na wameachwa" alisema Warioba.

Yafuatayo ni maelezo ya kina ya Jaji Warioba:

IPTL NI MZIGO

"Nataka nizungumzie mchakato wa Escrow, kwanza, IPTL imekuwa mzigo kwa nchi kwa muda mrefu tangu kampuni hiyo ilipoundwa, imekuwa na matatizo mengi. Katika kipindi hicho nchi imepoteza fedha nyingi kupitia kesi zilizotokana na IPTL ".

Nimesikia kwenye bunge kampuni moja ya wanasheria imelipwa sh.bilioni 62 lakini haikuwa peke yake, katika kesi hizo kulikuwa na gharama za TANESCO kwa kuwa walikuwa wakipeleka watu na kulikuwa na gharama za serikali, kwa hiyo fedha zilizotumika kwa migogoro hii ni nyingi.

"Katika utendaji wenyewe kulikuwa na matatizo, kwa hiyo nadhani ni jambo jema kwa sababu ya tatizo lililotokea lizungumzwe kwa undani ili kumaliza matatizo ya IPTL, tusiendelee nayo na gharama zake kwa nchi..
Kwa hiyo kulipeleka bungeni ilikuwa ni jambo zuri na limezungumzwa na ninaamini baada ya mchakato huu tutafika mahali tumalize matatizo ya IPTL na kuendelea na shughuli zingine za uchumi" alisema Warioba.

MAMBO MATATU MUHIMU

Warioba alisema hadi suala la IPTL linafikishwa bungeni na kisha kupatikana kwa maazimio ya Bunge kuna mambo matatu yameongoza mjadala:

La kwanza, ni wananchi, wananchi walikuwa na hamu ya kusikiliza mjadala Hui na kuona matokeo yake ni nini. Yalipokuwa yakitokea matatizo kama vile ya umeme, walikuwa wakilalamika kwa kuwa walitaka wafuatilie kwa ukaribu sana.

Hili kwa kiwango kikubwa naweza kusema ni kama vile imani ya wananchi kwa uongozi, hivyo kwa kila jambo linalotokea likiwahusu viongozi, wananchi wanakuwa makini kuona ni nini kitatokea. Hivyo bunge lilipokuwa likizungumza walijua kwamba wananchi wanatarajia kutatokea uamuzi mzito na si mazungumzo tu.

La pili, ni kwamba tunazungumza wakati huu ni kama wahisani wamesimamisha misaada kwa serikali na hata katika mjadala wengine walitaja hilo, kwamba limetuletea matatizo nchi sasa haipati misaada, kwa hiyo walipozungumza walijua kuwa wahisani walitaka waone matokeo ya hilo.

La tatu, nadhani ni siasa kwa kiwango kikubwa. Tunaingia katika kipindi cha uchaguzi, kwa hiyo vyama vinatafuta mambo ya kampeni kwa pande zote mbili, chama tawala na vyama vya upinzani. Nina hakika hili litaendelea kuwa jambo litakalozungumzwa wakati wa kampeni, kwa hiyo mazungumzo yote, huo ndo ulikuwa msingi wake.

FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI?

Mazungumzo yalivyokwenda utaona kubwa ambalo ndilo msingi wa uamuzi uliofanywa na bunge ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa mali ya umma na ndivyo wananchi wamefanywa waamini hilo lakini hakuna palipothibitishwa kuwa ni za umma. Msingi wa Escrow ni kwamba pande hizi mbili hazikuwa zikikubaliana kuhusu capacity charge, hivyo kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana waliona wawe na utaratibu, kwanza waendelee kushauriana wao wenyewe au kwenye mahakama ya nje; lakini kwa kipindi hicho kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana, iliafikiwa kuwe na mpango wa kuweka fedha mpaka watakapofikia makubaliano. Katika kipindi chote hicho IPTL ilikuwa ikitoa huduma, kwa hiyo kwa vyovyote vile ilikuwa na haki ya kulipwa capacity charge watakapokubaliana.

Hivyo kilicho cha uhakika katika fedha zile ni kwamba, zipo za capacity charge, hawakufika mahali waseme ni kiasi gani, lakini kwa kuwa sasa wanakwenda kuchunguza nina hakika mwisho itaonekana sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa ni za capacity charge", alisema warioba.

Hata hivyo, wananchi wamefanywa waamini kwamba fedha zote zilikuwa ni za umma, hilo ni mwelekeo wa kisiasa. Ni sawa wamefikia hapo, kama wameamua kwa msingi huo, wanasema kuna watu ni lazima wawajibike kwa hasara ambayo nchi imepata.

VIPORO VYA MASWALI

Jaji Warioba alisema mchakato huu wa IPTL na akaunti ya Escrow umeacha maswali kadhaa.:

" Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza , taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya ya Fedha na tatu ni yale yanahusu Wizara ya viwanda na biashara.

" Hasara inayotajwa kwa uhakika ilikuwa inahusu kodi inayotokana na mauzo ya hisa na hiyo si strictly ya Escrow ni kodi ya mauzo ya hisa , kwa namna ya capital gains tax na stamp duty. Wanaohusika hasa ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na pia wizara ya viwanda kwa maana ya Brela.

"Katika mjadala huu inaonekana kama wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa na huko ndiko yametokea matatizo ya hasara inayojulikana. Nimesoma taarifa ya PAC, wakifika kwenye wizara ya fedha, wanasema PAP kwa kushirikiana na maofisa wadogo wa TRA walofanya dhambi hii, sasa ni kama wanataka kuilinda Wizara ya Fedha. Katika mawasiliano yote Waziri Mkuu walimuingiza kwa kusema alikuwa akipata nakala za barua kakini Wizara ya Fedha ilihusika kabisa katika mawasiliano na wameachwa.

Brela wamefanya uzembe kwamba, unaweza kuandikisha kampuni na watu wakatia saini na majina hayapo, unaona kulikuwa na kasoro lakini haikuguswa. Kwa hiyo licha ya kuwa wameamua kuchagua watu waliohusika, inaonekana walikwenda mahali pamoja na huku kwingine wamewalinda.

Wamewalinda viongozi wa wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda, wakati vitendo vilivyosababisha hasara ya kodi kupatikana vimetendwa katika wizara hizi. Nijachouliza hapa ni kwa nini hawakutajwa, kuna element ya kulindana.

La pili linaloonekana kwamba kuna kulindana ni kwamba, waliopokea fedha kutoka kwa Rugemalira (James) wote wametajwa. Akaunti ya Rugemalira imetajwa katika benki ya mkombozi na hao wametuhumiwa lakini wanaohusika na fedha zilizotolewa stanbic bank , ambazo kamati inasema zilichukuliwa kwenye mifuko ya rambo, lumbesa na kwenye magunia, hawakutaja ni nani alichukua.

"Kwa sababu kama wanajua zilichukuliwa kwa njia hiyo, lazima watakuwa wanajua ni nani alichukua. Hivyo ni kwa nini hao waliochukua upande huu hawakutajwa? Unaaanza kuwa na maswali kuwa hapa kuna dalili za kulindana na wameendelea hivyo na kutoa uamuzi.

"Umuzi ule ni kama wa mahakama, bunge limekaa na kuamua kwamba fedha hizi na hasa alizolipa Rugemalira zilikuwa chafu na wote waliopokea fedha hizo walizipokea zikiwa chafu, hivyo na wao waadhibiwe. Wana ushahidi gani? Hawakuwasikiliza wale watu. Unasema kuna askofu amepewa fedha umuhukumu kwamba alijua kuwa ni fedha chafu, kuna jaji hapa alipata fedha unasema alijua ni fedha chafu, kuna Waziri alichukua fedha unasema alijua kuwa ni chafu, lakini hawakuwasikiliza.

" Kwa hiyo, wamehukumu bila kuwasikiliza na wamependekeza hatua za kuchukua. Baadhi yao wamesema wachukuliwe hatua za kinidhamu na wengine walipe kodi. Najiuliza kama askofu amepewa fedha, unasimama kwenye bunge unasema ajiandae kulipa kodi, najiuliza hivi ni mara ya kwanza kwa wao na watu wengine kupata fedha za aina hii? Mbona viongozi hao hao wanatoa misaada tena mikubwa na mahali pengi, mamilioni hatujasikia wakisema waliopewa walipe kodi.

" Hivi tuna uhakika gani kwamba hizi site zinazochangwa ni halali? Kwanini hawa ndio walipe kodi lakini zinazotolewa na wanasiasa husemi zilipiwe kodi.
Nadhani bunge halikutumia madaraka yake sawasawa. Unamwambia rais aunde tume ya kuwachunguza majaji walipata fedha, anaunda tume kwa msingi gani?

"Kwa sababu sheria inasema yakiwapo malalamiko kuhusu jaji, rais ataunda tume. Sasa hapa bunge linampelekea malalamiko gani yatakayomfamya aunde tume. Bunge lina ushahidi gani kwa sababu halikuwasikiliza ili kusema kuna malalamiko? Hilo nadhani bunge limeingilia mambo yasiyolihusu, ingekuwa haki kwamba hujatamka hatua gani zichukuliwe wangepata maelezo kutoka kwa wote wanaohusika ndipo ubaini kama kuna shaka ndipo uchukue hatua.....

Na Ester Mvungi, Dar es salaam

Sitakuwa nimetenda haki kama nikimlaumu Warioba na mwandishi wa taarifa hii. Hata hivyo kwa maoni yangu Warioba naye amekwenda mbali mno kuiona taarifa ya PAC Kuwa ilikuwa na udhaifu. Kwa haraka nilidhani huenda wahusika wengi ni vijana wake wa Nyumbani. Hata hivyo katika taarifa nzima kuna jambo moja tunalokubaliana sote nalo ni kuwa kuna TATIZO.

Sipashwi kulaumu kwa kuwa kwa upande mwingine vi vizuri kusikiliza na kuyapima maoni yaliyo tofauti na yangu, Lakini nina hakika Mzee Wetu mpendwa warioba anafahamu fika kuwa, hatua Elfu moja zinaanza na moja. Huenda hapo ameenda mbali sana kuelezea udhaifa katika mazingira ambayo sote tunajua jinsi kamati ilivyokuwa imebanwa. Kwanza viongozi wa kamati ilibidi wapongezwe na mzee Warioba kwa kuwa ni bado vijana wadogo ambao kisiasa si vizuri kuwakatisha tamaa. Ni kweli kamati imefanya zero??? Hapana Mnyonbd mnyongeni haki yake apewe.

Ni vizuri Warioba alivyosema kuna mambo ya kuendelea kuyatazama BRELLA na Wizara ya Mambo ya Ndani. Nadhani Mzee wangu warioba hajatenda haki kutolisemea jambo kubwa ambalo huenda likawa tatizo zito, Ninafikiri tu, Je: IPTL Imeuzwa. Inawezekana imeuzwa na inawezekana haijauzwa. Kama haijauzwa ni nani atawajibika kurudisha fedha zilizokuwa BOT Kwa IPTL. Tumeambiwa hakuna PAP, Hakuna majina, hii inatosha kutueleza kuwa Benki kuu imetapeliwa. Kwangu mimi hilo ni tatizo kubwa zaidi ambalo ninamsihi Warioba alizungumzie bayana. Mzee Warioba haoni kuwa kitendo cha Stanbic Bank ya Makaburu kuruhusu kutoa fedha kwa mabilioni kwenye sandalusi, fedha ambazo si za Seti, ili kuzichakachua na kuonesha Seti kanunua hisa ni Tatizo??

Ndugu zangu, tunajifunza nini katika tatizo hili kuhusu Mahakama kujaribu kulizuia Bunge, Serikali kutoa kauli tofauti, Turejee Kauli na hotuba ya Mhongo ya Masaa mawili, kauli ya Mwigulu, Kauliya Mwandosya, Kauli ya Wazira, Kauli ya Makamu Mwenyekiti kamati PAC ambaye ni Mwana CCM. Hapa kuna mengi ya kujifunza lakini moja kubwa ni kuwa, Kamati imefanya kazi Nzuri. Mbona Warioba enzi zake hazikuwa na matukio ya aina hii?? Leo tuna serikali ngapi? Msemaji wa serikali ni nani? Wananchi tuichukue kauli gani au ipi kuwa ndiyo ya Serikali.

Naomba kwa heshima na taadhima niyaweke maneno kinywani mwa Warioba kuwa alisema: Kun TATIZO, ndiyo maana ninaunga mkono maazimio ya Bunge kuwa, Uchunguzi uendelee na ukamilishwa na serikali ili hatua stahiki zichukuliwe kwa taasisi, shirika, kampuni, asasi na mtu yoyote ambaye atabainika kuwa amehusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la Escrow.
 
napata tabu sana kujua iweje gavana wa benki kuu hatajwi. napata tabu kujua kamishna wa mashirika ya umma katika wizara ya fedha hatajwi. napata tabu kujua waziri wa fedha hatajwi katika sakata hili.

iweje list ya stanbic haitajwi wala haizungumzwi kabisa tuseme ukweli washupaliaji wakuu wameogopa kupokonywa uanachama kama wangewataja hawa wa stanbic.
 
Nimeridhishwa sana na uchambuzi wa Mzee Warioba. Haki ingeonekana imetendeka kama Watu wote hasa wale wote waliobeba Fedha taslimu kutoka stanibic banki. Hakuna hata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina. je haukuwepo na uwezekano wa kuilazimisha benki kisheria kuipatia PAC taarifa za waliolipwa ? Hasa ikitiliwa maanani kuwa kiwango cha fedha zilizotolewa ni zaidi ya bilioni 75. Kosa la Mkombozi benki hasa ni lipi? Kama mmiliki wa VIP engineering alikuwa mmiliki halali wa hisa 3, Je kuna mashaka kuhusu umuliki wa hisa hizo? Je kuna mashaka kuhusu uuzaji wa hizo hisa? Au kuna mashaka kuhusu bei aliyolipwa? Je, kuna mashaka kuhusu ukokotoaji wa kodi aliyotakiwa kuilipwa na VIP? Kama jibu ni ndiyo ni kiasi gani cha kodi kilichokwepwa?Ni lini muuuzaji akapata fursa ya kumhoji mnunuzi uhalali wa fedha anazolipa? Ni lini kasisi akahoji muumini uhalali wa zaka anazozitoa ? Taratibu za kutoza kodi viogozi wa dini kutokana na zaka umeanza lini ? Vigezo vya kodi hizi ni vipi?Hakika taarifa ya PAC imetolewa kwa ushabiki kwa faida ya nani? Ni udhaifu wa kawaida au kuna malengo ambayo hayajawa wazi?

Mkuu,
Ninakubaliana na wewe.

Haya ndiyo maswali ambayo mapendekezo ya PAC yanatufanya tuulize huku wengine tukiwa tunadhani kama repoti ya PAC haikulitendea haki taifa.

Repoti ya PAC ilijikita kwenye cherry picking na kukomoana badala ya kutibu chanzo na matokeo ya tatizo.
 
Sasa ulitegemea nini wakati kijakazi chake Judge Werema ameguswa na wizi wa mabillion.

Katika michango yangu mingi kwenye hili swala la Escrow nimezungumzia sana kuwa hawa jamaa wamesurvive kwa vile repot ya PAC ilikuwa too weak. Pamoja na ushahidi kuwa overwhelming kuliko wa Richmond bado walishindwa kuja na report ya nguvu. Hiyo report ilikuwa ndiyo uwezo wao pamoja na kukesha. Niliwashangaa kuwakaribisha watu kama wakina Kingwang'ala badala ya design za akina Mwakyembe. Nawaelewa walitaka kupandisha profile yao kuwa vijana wanaweza but it backfired big time. FF aliiona mapema akatahadharisha watu lakini only few people understood her. Halafu kuna tu kesho atakuja dai eti Zitto ni presidential material ....................what a joke!!

Hili nalo jipya......lkn kiukweli hata mimi nilishangaa Waziri wa fedha kutoguswa na hili sakata.

Inaelekea wewe ndiyo unazeeka bila kufahamu, usimsingizie mzee wa watu kajiangalie kwenye kioo vizuri ...................... the point is very clear watuhumiwa wamesurvive kwa sababu report ya Zitto ilikuwa too weak .............Period!!! Whether you like it or not, that's the truth!!


Waungwana, hata mimi ningeandika ripoti ya PAC, kuna watu ningewaruka makusudi kabisa ili wahusika wakuu waangamie. Angalieni mjadala ulivyoendeshwa. Ilifikia wakati likawekwa kama ni CCM na UKAWA. Baadaye tena ukabila ukaanza kujitokeza. Akina Mwijage wakaanza kutetea bila kueleza ni kwa nguvu gani. Ukiwa unawawinda akina Muhongo, Maswi, Tibaijuka na wengine wahusika wakuu, lazima umkwepe Rais wa nchi ambaye pia kuna dalili kubwa kabisa kwamba ndo chanzo cha haya yote.

Sasa pale bungeni kama PAC ingekomaa na kusema kila kitu pamoja na jina la Rais, fikilia wabunge wa CCM wangefanya nini? Tuliona kabisa kila Pinda alipoguswa takribani mawaziri wote walisimama, kwa kujua kwamba wanakosa uwaziri!

Sasa tuendelee ili baadaye tuelewe nani alisahaulika au aliachwa.
 
Ana pointi wazee.

Haswa,
Capital gain na Stamp duty. Hawa jamaa walikuwa wameshasepa nayo. Faini na Riba lazima wapigwe.

Mwenye majina ya walio-beba na viroba atuwekee hapa. Hapo ndio mtakoma kuwa na Raisi Jizi na Njaa kali.
 
Na asipokuwa pointi

Ni pale anapokazania eti kwa misingi gani walipe kodi? Kodi ni kitu kidogo sana kwanza, kama viongozi waandamizi hawakutakiwa wapokee rushwa. Na wamejihusisha na utakasaji wa fedha. Hiyo misingi anayodai mizuri sana ndio imeifanya mijitu, miviongovi imekuwa hovyo kabisa.

Kuna saa inafikia, kama kule Taharir Misri, mambo ya kanuni sijui misingi inakuwa inawalinda zaidi vigogo kuliko wananchi wa kawaida hivyo lazima itumike nguvu nyingine.
 
Back
Top Bottom