Iwe heri kwako Bro Mabeste katika ndoa yako

Iwe heri kwako Bro Mabeste katika ndoa yako

Mbona huyu kawaida sana
Kaka yetu amepata jiko bora bhana 😃 Namba C kabsa
1742845913188.jpg
 
Mnasema


Mmesema anateswa na mademu, halafu tena mnamwita mgumu. Endeleeni kututania.
Kwani wagumu hawateswi na mapenzi mkuu!? Moyo wa mtu kichaka!
 
Hongera sana kwa kuanza ukurasa mpya wa maisha, tazama mbele brother na endelea kusamehe na kusahau yale ambayo yalitokea kipindi ulipojitoa kwa ajili ya Lisa. Karma is a bitch! Nature itakulipia bro wala usisumbuke na yaliyopita, waswahili wanasema YALIYOPITA SI NDWELE tazama mbele kuna maisha unatakiwa kuishi duniani.
View attachment 3273112

Nadhani kila Mtanzania anafahamu kisa chako wewe na aliyewahi kuwa Mke wako, nyakati za furaha pamoja na nyakati mbaya. Ila usione ajabu kupata watanzania wengi wakikuzungumzia kama mfano bora sana, wapo ambao wamekupa jina la GENTLEMAN, wapo wanaokuita MSAMARIA na kuna wengine walikwenda mbali na kuona kuwa haukupaswa kujitoa kiasi kile kwa mwanamke ambaye hakuwahi kuwa na upendo wala hisia kwako.
View attachment 3273113

Nina imani shemeji yetu ni mtu wa kipekee sana kwako, pamoja na familia yako, naweza kusema kuwa una bahati ya kipekee kwa sababu hayupo kwenye vichwa vya habari sio Facebook, Tiktok wala Instagram, ni kupitia picha zenu za harusi watu ndo wamemuona shemeji kwa mara ya kwanza kuwa ndo Mrs. Mabeste.
View attachment 3273114

Mbali na hayo kuna idadi kubwa ya watu kutoka nyumbani Tanzania, Kenya, Uganda na mataifa mengi tunatamani kuona ukirejea kwenye fani ya muziki, japo tuendelee kusikia sauti yako.

HONGERA SANA KWA KUJIPATIA JIKO BORA KAKA MABESTE.
Dogo jinga sana
 
Heri kwao... hopefully amegraduate kutoka uvulana kwenda uanaume.
Akawe baba mzuri kwa watoto wake wa kufikia
 
Mtoa mada punguza muwasho... huyo Lisa ana maisha yake na hana shida na mtu....
Mkumbushe tu kijana wako huko akawe mwanaume haswa na pia awalee vizuri hao mabinti wa mwanaume mwenzie
 
hii sio namba C hii ni namba A kabisa mhh hata kama ni kuchagua wife material hii level ya namna hii hapana
😆 😂 😆 😂 😆 kikubwa amani buda, halafu manzi ni wakawaida tu hata sio mbaya jamani, ukitegemea yupo hivyo bila manyamanyama after 2 kids....
 
Mtoa mada punguza muwasho... huyo Lisa ana maisha yake na hana shida na mtu....
Mkumbushe tu kijana wako huko akawe mwanaume haswa na pia awalee vizuri hao mabinti wa mwanaume mwenzie
Au sio
 
Back
Top Bottom