Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 356
- 707
Leo nilipata nilipata nafasi ya kutafakari habari kutoka Njombe kutoka katika mitandao ya kijamii
Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika ujumbe ambao alikuwa anatoa alilielezea kisa cha kijana mmoja ambaye alipewa kazi ya kukusanya maparachichi kutoka kqa wakulima na mfanyabiashara wakiasia.
Mfanyabiashara huyo alimpa mtaji wa kiasi cha Tshs 100 Milioni kwa ajili ya kuanza kazi ya kukusanya maparachichi kijana huyo mara baada ya kupewa mtaji huo badala ya kukusanya parachichi alipotea na fedha za watu na hakuna alichofanya na pesa za watu.
Habari hiyo ilinishikitisha sana, kutokana na jinsi mtu anavyoweza kupoteza kesho yake kaa tamaa ya leo.
Mungu akitaka kukutoa kiwango kimoja kwenda atakuingiza kwenye mtihani na miongoni mwa mitihani ambayo Mungu anatoa kwa watu wake ni mtihani wa uaminifu
Unaposoma habari za Daniel katika kitabu cha Daniel, Daniel alifanikiwa kuwa kiongozi katika nchi ya ugeni sio kwa sababu alikuwa na akili sana kuliko wengine hapana Daniel aliwazidi wenzake kitu kimoja tu ambacho ni uaminifu
Mfalme alifanya tathimini ya utendaji kazi wa watumishi wake na akabaini kwamba hakuna mwaminifu kama
Daniel katika kazi watumishi wake akampandisha cheo.
Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Danieli 6:4_4.
Umesoma habari za Yusufu mwana wa Yakobo, Yusufu kilichomsaidia kuwa Waziri Mkuu katika nchi ya Misri ni uaminifu wake
Yusufu wakati anafanya kazi kwa Potifa alikutana na mtihani wa uaminifu juu ya mke wa potifa, kijana mwingine angeona kuwa ndio fursa ya kufanikiwa kwa kutembea na mke wa bosi wake, lakini Yusufu akaona huu ni mtengo kutoka kwa Mungu aksema maneno aya
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? Mwanzo 39:9
Yusufu alimwabia yule mama sijui kama alimwelewa? yule mama aliona kwakuwa wako wawili hakuna mtu atakaye toa siri kwa mumewe, lakini Yusufu aliona wako watatu ndio maana akasema nifanyaje ubaya huu mkubwa ni mkose Mungu?
Je unapokuwa pekee yako au umepewa fedha utakuwa mwaminufu au utahamua kupotea na fedha za watu
Mtu yoyote ambaye sio mwaminifu ni mtu ambaye hajui kesho yake, Yusufu akiwa kijana mdogo aliota ndoto ya kwamba hiko siku hatakuwa waziri mkuu na ndoto hiyo hakuiacha
Tunapokuwa watoto kila mmoja anakuwa na ndoto yake na zingine tunapewa na watu , unasikia huyu mtoto atakuwa mtumishi wa Mungu au huyu mtoto atakuwa mfanyabiashara mkubwa
Zile ndoto ambazo tunakuwa nazo utotoni wengi hatuzifati na tunaingia katika vishawishi vya shetani
Mungu pekee ndiye aliyekupangia maisha bora na ya mafanikio pekee na sio shetani na kazi ya shetani ni kukutengenezea mazingira ili umkose Mungu na Mungu asikusaidie
Yule kijana wa parachichi alipata kazi ya kubadirisha maisha yake , inawezekana kila siku alikuwa anamwomba Mungu amsaidie kuwa na kipato cha uhakika cha kubadirisha maisha yake na familia yake na Mungu ni mwaminifu akamleta mfanyabishara wa kumsaidia lakini kutokana na tamaa kijana akapoteza baraka zake
Habari kama hizi sio mara ya kwanza kuziskia ziko nyingi mtu anapewa duka kufanya kazi ya kuuza duka la mtu badala ya kufanya kazi kwa uhaminifu unakuwa wakwanza kumwibia na kupelekea mweye duka kufirisika au kushindwa kuendelea na biashara
Unaposhindwa kuwa mwaminifu kwa mali za watu Mungu hawezi kukupa ya kwako
Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.Luka 19:17
Uaminifu unajengwa , uaminifu sio kitu kinashuka kutoka mbinguni hapana uaminifu ni tabia ambayo inajengwa, ili uwe mwanifu kwa vitu vikubwa kuwa mwaminifu katika kidogo
Umepewa kazi na mtu fanya kazi kwa uaminifu hata kama malipo ni madogo
Kuna katabia kwa watu kutumia kigezo kwa kuwa kazi ina malipo madogo basi ni lazima nisiwe mwaminifu hapana kama unaona malipo ni madogo omba kuongezewa, kama haujapata tafuta sehemu nyingine
Na mara nyingi kazi ambayo inakuwa na kipato kidogo inakuwa na ushawishi sana na inawezekana ayo mazingira ya kazi yanaweza kuwa ni sehemu ya mwajiri kutafuta mtu mwaminifu kwa ajili ya kumpa majukumu makubwa zaidi ukashidwa huo mtihani kwa tamaa ndogo
Siku zote kumbuka neno hili
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Luka 16:10
Tengeneza uhaminifu katika vitu vidogo na makubwa yatakuja kwako, Yusufu angefeli mtihani wa uhaminifu leo hii tusingekuwa na habari ya Yusufu kama waziri mkuu kwa sababu alishinda
Popote unapoaminiwa kufanya kazi iwe kazi ya kumtumikia Mungu au kazi ya kaisari hakikisha unafanya kazi kama unafanya kwa Bwana
Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu. Wakolosai 3:23