Inawezekana kupata kazi Serikalini kwa kutuma maombi pasipo kazi kutangazwa?

mweatu

Member
Jul 13, 2015
16
47
Ndugu wanajamvi, habarini za majukumu. Kutokana na wimbi la uhaba wa ajira na hasa ajira za Serikali, baadhi ya vijana wameonekana kukata tamaa juu ya ajira hizi za serikali.

Wengi huwa tunaomba kazi za serikali pale zinapotangazwa na hatujawahi kubahatika kuajiriwa.

Najaribu kufikiria kutuma MAOMBI ya kazi serikalini hata bila kazi kutangazwa.

Mwenye uzoefu wa kupata kazi kwa njia hii tafadhari tujuzane
 
Mkuu nafikiria kuomba Mfano TPDC, TIRDO, Wakala wa vipimo-WMA, Baraza la uhifadhi wa mazingira- NEMC, Mamlaka za maji eg MOROWASA, DAWASA n.k
 
Mkuu nafikiria kuomba Mfano TPDC, TIRDO, Wakala wa vipimo-WMA, Baraza la uhifadhi wa mazingira- NEMC, Mamlaka za maji eg MOROWASA, DAWASA n.a
Ajira serikalini lazima upite utumishi mkuu labda kama utakuwa unaomba Internship ndo upite TaESA au uende katika ofisi husika.
 
Ajira serikalini lazima upite utumishi mkuu labda kama utakuwa unaomba Internship ndo upite TaESA au uende katika ofisi husika.
Hilo nafahamu mkuu, ila kuna baadhi ya taasisi ambazo sijawahi kuona matangazo ya kazi zao utumishi. Ndiyo maana najiuliza kuwa kazi kwenye hzo taasisi zinapatikana kwa namna gani?
 
Kwa kuongezea kwa mwenye uzi:-
Jobless anaweza tuma maombi ya kufanya kazi kwa kujitolea katika Wizara ambayo inasimamia taaluma aloisomea? Kama ni Yes, utaratibu unakuaje?
 
Hilo nafahamu mkuu, ila kuna baadhi ya taasisi ambazo sijawahi kuona matangazo ya kazi zao utumishi. Ndiyo maana najiuliza kuwa kazi kwenye hzo taasisi zinapatikana kwa namna gani?
Ukiona hawatangazi jua kuna transfer ndani kwa ndani
 
Back
Top Bottom