Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,438
1,387
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-

1. SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe ni raia wa Tanzania;
ii. Awe amehudhuria na kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au tayari amerudi Uraiani;
iii. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
iv. Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
v. Awe na Kitambulisho cha Taifa au Nambari ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
vi. Awe na siha njema ya mwili na akili iliyothibishwa na Daktari wa Serikali,
vii. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
viii. Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
ix. Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
x. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
xi. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 23, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 26 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
xii. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
xiii. Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la Ajira.

2. MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE

Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:

Masijala, Udereva, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Tathmini na Uperembaji (Monitoring & Evaluation), Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa AC, Uhusiano, Cyber Security, Brass band, Mtunza Nyumba (House keeping), Mtunza Bustani (Garderner) na Mpiga chapa (Printer).

3. NAMNA YA KUFANYA MAOMBI: Mwombaji anatakiwa kuwasilisha barua ya Maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono wake ikiwa na namba ya simu inayoweza kupatikana muda wote. Pamoja na barua ya maombi ya ajira, mwombaji anapaswa kuambatisha nakala ya nyaraka zifuatazo:-

i. Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; ii. Cheti cha kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU). Kwa waombaji waliopo Makambini, barua zao zipitie kwa Wakuu wa Kambi husika; iii. Cheti cha Kuzaliwa; iv. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; v. Cheti cha Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na Shahada; vi. Vyeti vingine vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Stashahada na Astashahada (kama anavyo); vii. Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi; viii. Wasifu wa Mwombaji (CV), ix. Picha Tano (05) za Pasipoti zenye rangi ya Bluu bahari.

4. MAOMBI YA AJIRA YATUMWE KUPITIA ANUANI ZIFUATAZO:

a) Kwa Waombaji walioko Tanzania Bara watume kupitia kwa:


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, 4
Barabara ya Mwangosi,
UZUNGUNI,
S. L. P. 1181,
DODOMA

b) Kwa Waombaji walioko Zanzibar watume kupitia kwa:

Kamishna wa Uhamiaji,
S. L. P. 1354,
ZANZIBAR

5. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 12 Januari, 2024.

TAHADHARI
(i) Hakuna maombi yatakayopokelewa nje ya utaratibu ulioainishwa katika kifungu Namba 4 hapo juu.

(ii) Mwombaji yoyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

Limetolewa na:

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI, MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI - DODOMA. Tarehe; 30 Disemba, 2023
 

Attachments

  • TANGAZO LA AJIRA 2023.pdf
    193.3 KB · Views: 15
Sisi tulioenda kwa mujibu wa sheria pia tunaruhusiwa kuomba ?. Maana vyuma mtaani vimekaza vibaya mno
 
Afu sijaelewa wanaposema passport size 5 , wanamaanisha nini yani katika maombi yako ndani ya bahasha uweke na picha za passport size 5 ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom