TAMISEMI ongezeni muda wa kutuma maombi ya ualimu na afya

WEKKI

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
477
145
Ndugu zangu ningeomba tutumie huu Uzi kutoa maoni Kwa kuwaomba TAMISEMI kuongeza Muda wa watanzania kutuma maombi ya Kazi za ualim na Afya.

Kwanza muda uliotolewa no siku ambazo sio Chini ya 20 na yawezekana wengi wasiombe na kukosa Fursa ya Kuajiriwa(Kwa wale watoto wa maskini) ambao hawana plan yoyote ile.

Tunaomba Mama yetu ANGELA KAIRUKI uongeze Muda ili wafuassi wako wapate kupona. Sababu kubwa za Kuomba muda uongezwe no hizi hapa;
1. Ucheleweshaji wa Transcript na Leseni za MCT
Kwa ambao mmenda NACTE pale Kuna watu waliomba Transcripts za Kada ya Afya Kwa muda mrefu lakini Huwa zinacheleweshwa. Mtu analipa ili atumie Transcripts mkoani anaisubiri haimfikii anaamua Kufunga safar mpaka NACTE ili apatiwe anatumia siku Mbili Toka Mkoani mpaka Dar akifika pale tayari muda unakuwa umeisha kabisa au anapewa majibu ya subiri.

2. Ulazima wa kuwa na Leseni za MCT na Bodi nyingine kama Za Famasia na Uuguzi Kwa Nursing. Kama mnavyojua anayemaliza chuo Kwa Afya ili afanye kazi lazima awe na leseni. Hii wengi hawaipingi ila tatizo ni pale ambapo Leseni hizi zinachelewa. Mfano mtu kamaliza chuo 2020 ama 2021. Akishamaliza chuo anapaswa awe na leseni leseni kuipata sio Chini ya 400K yaani ada zake na Enrollment Fees. Kwa watanzania walio wengi kupata Laki nne ya kulipa ili apewe leseni kwanza ni Kizungumkuti. Pili Kwa wengine akishalipia Leseni haifiki Kwa wakati. Mfano hapo MCT Kuna mtu alilipia leseni Wiki Iliyopita Jumanne akaambiwa ndani ya Siku Tano itapatikana akaamua Kurudi Mkoani amekwishafika anaisubiri anaambiwa bado. Ina maana Mpaka Deadline inafika atakua hajaipata.

Kama mnavyojua wengi hufuatilia vyeti vyao pale ambapo kazii hutangazwa lakini Kuna yrasimu MKUBWA wa kupata vyeti haswa vya kitaaluma na ukitoa wiki mbili owe deadline ya kutuma maombi watu wengi wanaumia
Zipo sababu nyingi sana ambazo zinachelewesha watu kutokupata Documents zote za kuombea kazi.

Tunawoamba TAMISEMI kuongeza Muda hata wa wiki mbili au zaidi ili watu wapate Fursa ya Kuomba Kazi na kuijenga Nchi.
 
Huo muda wa maombi uliotolewa unatosha, mtu anapaswa kufuatilia vyeti na document nyingine punde anapomaliza masomo. Sasa umemaliza 2020 au 2021 hadi leo hivyo viambata huna, tatizo la nani hapo? Na utake upate mapema kwa kuwa ajira zimetolewa, huo ni uzembe wako.

Kama tatizo lilikuwa pesa huko nyuma. Leo umeitoa wapi?
 
Duuh, kweli wewe ni Sayansi piwa, umecharanga mwandiko wa kitabibu.

Hebu fikiria hili.

1. Kuna mtu hadi sasa hana hata namba ya nida.

2. Kuchukulia poa, mambo ya msingi.

3. Kuna mtu hapo unamtetea, lakini alipewa hela yote ya kupata vyeti au leseni na asifanye yanayohitajika

4. Zimamoto.

5. Serikali inajua watu wanavyo vyeti, lakini hiyo ni njia pia ya kupunguza jam, kazi chache ila watu wengi.
 
Huo muda wa maombi uliotolewa unatosha , Mtu anapaswa kufuatilia vyeti na document nyingine punde anapomaliza masomo.Sasa umemaliza 2020 au 2021 hadi leo hivyo viambata huna , tatizo la nani hapo?
Na utake upate mapema kwa kuwa ajira zimetolewa, huo ni uzembe wako .
Kama tatizo lilikuwa pesa huko nyuma ..leo umeitoa wapi???.
Kuna watu walimaliza Vyuo 2020 na 2019 lakini mpaka Sasa hawajafikiwa na Transcripts. Hebu nenda pale NACTE Mikocheni uone watoto wa Maskini wanavyohaha kupata Transcripts. Kuna watu wamesubiri vyeti hvyo zaidi ya Mwaka. Wakipiga simu mtu anaambiwa subiri. Muda uongezwe
 
Duuh, kweli wewe ni Sayansi piwa, umecharanga mwandiko wa kitabibu.

Hebu fikiria hili.

1.Kuna mtu hadi sasa hana hata namba ya nida.

2.Kuchukulia poa, mambo ya msingi.

3.Kuna mtu hapo unamtetea, lakini alipewa hela yote ya kupata vyeti au leseni na asifanye yanayohitajika

4.Zimamoto.

5.Serikali inajua watu wanavyo vyeti, lakini hiyo ni njia pia ya kupunguza jam, kazi chache ila watu wengi.
Leseni ya MCT au ya Ufamasia pamoja na kuwa na. Malipo Kuna ambao hawana hata nauli ya kuzifata. Sisi tunajiuliza kama Mtu kamaliza chuo Mwanza Kwanini RMO wa Mkoa ndo
 
Watu ni wengi kuliko nafasi zilizotangazwa halafu eti unatoa hoja za kuongeza muda,umewaza vema kweli wewe?
Hata wangetoa siku tatu,zilikua zinatosha ilimradi mtandao uko vizuri.

Hoja zako zote ni dhaifu, watu ni wengi, hao ambao hawajakamilisha, wasubiri nafasi nyingine.

Ntawasilisha.
 
Kuna watu walimaliza Vyuo 2020 na 2019 lakini mpaka Sasa hawajafikiwa na Transcripts. Hebu nenda pale NACTE Mikocheni uone watoto wa Maskini wanavyohaha kupata Transcripts. Kuna watu wamesubiri vyeti hvyo zaidi ya Mwaka. Wakipiga simu mtu anaambiwa subiri. Muda uongezwe
Sasa kama mtu kamaliza 2019 na kaanza kufatilia hiyo transcript hajapata hadi leo unataka muda wa ku apply uongezwe kwa kiasi gani? Uongezwe kwa miaka mingapi?

We jamaa kataa kubali, mnapenda Sana zimamoto. Mmeanza kufuatilia vyeti baada ya tangazo la ajira
 
Ndugu yangu Kama transcripts ingekuwa inatoka Chuoni Moja Kwa moja hapakuwa na tatizo. Lakini unavyosema transcripts itoke NACTE Dar unatarajia nini? Hivi unajua Kuna watu wamemaliza vyuo na washasahau mpaka namba ya Mtihani wa Form 4. Hivi unajua Kuna watu hata shilingi laki Moja ya Kwenda Dar hawana.? Hivi unajua kuwa Unaweza chukua Transcripts na ikawa kama pambo kutokana na Ajira kuchekeweshwa?

Kuna mambo mengi sana ambayo watu wanakutana nayo shukuru Mungu ulisoma Kozi ambayo Cheti unapata Chuoni na hauhtaji leseni ama kufata Transcripts Mikocheni.
 
Ndio maana Hii Nchi watu wanabeba mihela wakijua kuwa watanzania wengi hawawezi wafanya lolote na watawanyamazia. Mtu anaibua hoja ambayo watanzania wengi wanakutana nazo unaibuka huko eti sio lazima uajiriwe.. Points zote ambazo mtu anatoa ni Uhuru wake na ni kilio Cha walio wengi na haujalazimishwa kuandika Hapa. Wakati mwingine ni vyema kukaa Kimya kuliko kuongea ukkonekana mjinga
 
We ni poor brain ndomaana watu wanabeba mihela na wakijua Kuna watu watakuja na kauli za kuwatetea. Nacte,MCT na Wizara ya elimu wanapaswa wabadili mfumo wao sio Kwa Ajira Bali Kwa Kila kitu
 
Maombi ya kazi kuwa na deadline nacho ni kigezo.
Hoja yako ya leseni nadhani tangia unasoma unalijua hilo. Ni vizuri kujiandaa kuanza kujiandaa mapema.
 
Maombi ya kazi kuwa na deadline nacho ni kigezo.
Hoja yako ya leseni nadhani tangia unasoma unalijua hilo. Ni vizuri kujiandaa kuanza kujiandaa mapema.
Isshue ya Leseni imeletwa juzi. Haikuwepo. Shida sio kujua shida no urasimu wa upatikanaji
 
Kuna watu wako Dodoma kule, hamtaki kuwatumia kwa masuala ya haraka kama ya huko MCT, mnakuja humu kusumbua. Akina Dodoma messengers wana kazi gani kule,msiwapigie wawaharakikishie michakato na utumwaji wa nyaraka zenu?

Ngoja siku ziyoyome muone,mwisho wa siku aje Luhaga Mpina, ashike urais, afanye Kama JPM, azuie kuajiri, ndipo ambapo mtamkumbuka huyu mama, na kulaumu uzembe wenu.
 
Wewe kama hukuandaa vitu vyako mapema usiandike ujinga humu,
Kwanza kupata Nacte transcript haichukui hata week tatu wewe useme ukweli umeanza kushugulikia vitu baada ya ajira kutangazwa
Hauko serious na mambo yako

Utajijua
 
Mm naona wafunge tu hata Leo kuna demu ni mwalimu wa phy na chem aliomba siku ya kwanza kabisa mpaka Leo shule alizoomba ipo hivi

Shule ya kwanza wapo 2

Shule ya pili na ya tatu yupo yeye tu

Shule ya nne wapo 5

Shule ya tano wapo 3

Alafu kuna sehemu English wapo watu 756
 
Back
Top Bottom