In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Mkuu Pundit,

Ninajaribu kuielewa point yako wewe, Warioba na Butiku, lakini tatizo mnailazimisha kusimama at the wrong place, and time pia, kwa sababu kama ni Due Process Lowassa, sasa ana haki ya kwenda mahakamani tena njia ni nyeupe,

Mwanakijiji, anakwambia kuwa kwa misingi ya kisheria za kamati za bunge na uchunguzi, haikuwa lazima kwa hiii kamati kumhoji Lowassa, kwa sababu kwanza hakuwa the main principle wa uchunguzi, na kwamba kamati haikuona umuhimu wa kumhoji kwa kisheria za bunge ilikuwa sio lazima imuhoji yeye ili kukamilisha ripoti yake ya uchunguzi, kulingana na sheria za bunge.

Warioba na Butiku, hawalisaidiii taifa na maneno yao ambayo ukweli ni kwamba hawana idea of what they are talking about, kwa kuchanganya sheria kwenye siasa, Lowassa amejihukumu mwenyewe kwenye Court ya siasa, kwa kuikimbia Court of Public Opinion, lakini Bunge, na Mwakyembe, they have absolutely nothing to do na kujiuzulu kwa Lowassa na hii ripoti,

Slightly kama kuna ishu, Warioba na Butiku, walipaswa ku-question kwa nini rais alikubali kujiuzulu kwa Lowassa, kwa sababu legally ndio the only standing order kwenye hiii ishu, Lowassa, pamoja na kusema anajiuzulu bungeni, bado aliendelea na priviledges zote affordable kwa Waziri Mkuu, lakini hiii iliiisha the minute Rais aliposema amekubali kujiuzulu kwake ndipo the first thing akanyanga'nywa bendera kwenye gari, ngao ikang'olewa mbele ya gari, walinzi wakapungua na kubaki wawili, na ndani ya bunge akaanza kukaa nyuma anakostahili, sasa kama kuna wa kumlaumu na kutoka kwa Lowassa, kwanza ni yeye mwenyewe, na pili ni rafiki yake rais wetu,

At this time as a nation kwa kweli hatuyahitaji haya maneno ya kina Warioba na Butiku, na wewe pia Pundit, kwa sababu mnachojaribu kufanya ni kutuhadaa na maneno mengi ya kishule an kisheria, ambayo ukweli ni kwamba ni none applicable kwenye the ishu, sasa hivi wananchi tunatakiwa ku-move kwenye next phase ya hii ishu, yaaani Sheria, na wengine waliobaki ambao hawajatoka, sasa ni makosa kujaribu kutuvuruga wananchi na maneno mengi matupu kisiasa na kisheria, mimi sijawahi kusikia mtu anakimbia kazi yake kwa sababu ya ripoti ambayo ana hakika kuwa ni ya uongo na kwamba kabla ya kuiwasilisha hakupewa haki ya kuhojiwa, kama kweli Lowassa amejiuzulu kwa sababu hizi tu basi hakuwa competent enough in the first place kuwa Waziri Mkuu, wa taifa letu na ndio maana hata rais akakubali kuondoka kwake.

Warioba, Butiku, na Pundit, jamani mtuache wananchi tuendelee na kuwachambua wengine waliohusika ambao wanaweza kujificha na mijadala hewa kama huu, maana in the process kuna mjadala muhimu kisheria wa kwa nini Yona na Rostam, wako nje baada ya kukataa kwenda kwenye kamati? Otherwise Mkuu Pundit, tumekubali kwamba una elimu nzito sana na masuala ya journalism kama sio sheria, lakini ukweli ni kwamba kwenye kujiuzulu Lowassa, vyote havihusiki kabisaaa.

Ahsante Wakuu.
 
pm.jpg

Mzee Hapa Ni Wa Kiyanga Kinoma, Sasa Tuiweke Picha Hii Na Tumtazame Vipi Atakuwa Akiondoka.

zamani.jpg

Kumbe Hawa Jamaa Washkaji Kinoma? Jee Ataweza Kumuwajibisha? Au Ndio Yataenda Kishkaji Kishkaji?

pindaaapa.jpg

Mheshimiwa Kaanza Kubadilika Katinga Na Suti Naam Kesha Atapiga Rangi Ya Kunde Na Ile Mikunjo Mikunjo Utazani Utumbo Wa Ngozi Utaondoka Na Atakuwa Soft.
 
...................mimi sijawahi kusikia mtu anakimbia kazi yake kwa sababu ya ripoti ambayo ana hakika kuwa ni ya uongo na kwamba kabla ya kuiwasilisha hakupewa haki ya kuhojiwa, kama kweli Lowassa amejiuzulu kwa sababu hizi tu basi hakuwa competent enough in the first place kuwa Waziri Mkuu, wa taifa letu na ndio maana hata rais akakubali kuondoka kwake........................

FMES.....nakubaliana nawe huyu bwana hakuwa competent kabisa!!..........ingependeza zaidi kwa EL pale bungeni kama angepangua hoja moja baada ya nyingine.......halafu ajiuzulu!!!
 
Duh,
Jamani tuache utani mkuu wangu Pinda ana sura nzito kichizi!... eeeh bwana wee kama sura ingekuwa inazungumzia utendaji kazi basi huyu jamaa anaonekana hana mchezo... mtanisamehe nimeshindwa vumilia... yaani hapa nahaha akiniita ofisini kwake wala sintafika, nitajiuzuru JF mapemaa...
 
Mkandara umenivunja mbavu kwa kicheko!

Usimwogope sana, labda bado hajarelax na kupata pozi inayotakiwa pichani.

Ila mkuu ni gentleman na simple, hatishi kama picha zinavyomwonyesha.

Anapenda sana suti za mikono mifupi tangu akiwa naibu waziri.
 
Kithuku,

Nani kasema Lowassa kaonewa? Tatizo ni kwamba kwenye sheria, haki si muhimu tu kupatikana, bali pia ni muhimu haki kuonekana kuwa imepatikana.Beef yangu siyo juu ya incident, it is more about the process and principle.

Kwa hiyo ukifanya kazi na kutoa ripoti ya haki, lakini ambayo inaweza kuwa spinned kuwa haki haikutendeka, unaweza kuleta grounds za watu ku question kama haki imetendeka.

Ndiyo maana Lowassa anapata msemo hajahojiwa, kwa sababu kwa kutohojiwa amepewa nafasi ya ku-spin mambo kwamba hajatendewa haki.

Nilitaka Lowassa abanwe akose hata pa kutokea kirahisi rahisi kama hivyo.Ingewezekana kabisa speech ya kujiuzulu ya Waziri Mkuu ingekuwa ya kuwaomba msamaha Watanzania kwa ubadhirifu wake (kwa kukosa cha kutokea), au kungekuwa na perjury charges against Lowassa kwa kudanganya under oath.Mwakyembe kwa kutomhoji Lowassa amewanyima Watanzania any of those teo outcomes, instead Lowassa sasa yuko huru kama mbunge na mfanyabiashara.

Waendesha mashitaka wanapotaka kumfungulia mtuhumiwa kesi, hufanya uchunguzi na kukusanya ushahidi, ikiwa ni either pamoja na kumuhoji mtuhumiwa au bila kumuhoji mtuhumiwa.
Mahakama ni chombo cha kutoa haki lakini siyo Bunge.
Hii kamati iliundwa kuchunguza scandal ya Richmond na si kumchunguza Waziri mkuu.Sasa katika uchunguzi wao walialika watu wote wenye information wenye information kuhusiana na scandal hii.Pia walikuwa na hiari kumwita au kutomwita mtu yeyote kama waliona umuhimu upo,ili kufanikisha uchunguzi huo.Kama waliona hakuna haja ya kumwita Waziri mkuu kutoa maelezo ili kufanikisha uchunguzi huo walikuwa na hiari hiyo.
Kazi ya kamati haikuwa kum-clean au kum-implicate Waziri mkuu au mtu yeyote katika uchunguzi wao.
Kama EL anaona kawa implicated kwenye scandal ya Richard Monduli si kwa halali na kavunjiwa heshima na kuchafuliwa jina lake,sasa ndo ulikuwa wakati mzuri wa yeye kutafuta hahi yake kwa kwenda kuishitaki Kamati hiyo mahakamani.
 
According to the dataz kumbe toka skiu ya kwanza Muungwana, anaukwaa urais aliambiwa na wakuu wote wa CCM, ampe Pinda u-PM, yeye akagoma na kujfanya anajua zaidi, sasa hatimaye amekubali, baada tena ya kujaribu kubishana nao kuhusu idea yake ya kumpa tyson, ripoti ndiyo iliyoua kabisa na kumpa the original Pinda!
 
Duh,
Jamani tuache utani mkuu wangu Pinda ana sura nzito kichizi!... eeeh bwana wee kama sura ingekuwa inazungumzia utendaji kazi basi huyu jamaa anaonekana hana mchezo... mtanisamehe nimeshindwa vumilia... yaani hapa nahaha akiniita ofisini kwake wala sintafika, nitajiuzuru JF mapemaa...

Mkandara,

Lowassa ni handsome- ila ni mla rushwa na pia incompetent!

Sasa Pinda kama sura sii nzuri- unadhani Tunu angempenda? Halafu je uzuri wa mwanamme ni sura tu?

Nadhani uzuri wa Pinda tumuulize mama Tunu- yeye ndo anafahamu!

Hii sura ya Ufipa ndugu yangu- hapendwi mtu- ni mzee wa kazi!
 
Waendesha mashitaka wanapotaka kumfungulia mtuhumiwa kesi, hufanya uchunguzi na kukusanya ushahidi, ikiwa ni either pamoja na kumuhoji mtuhumiwa au bila kumuhoji mtuhumiwa.
Mahakama ni chombo cha kutoa haki lakini siyo Bunge.
Hii kamati iliundwa kuchunguza scandal ya Richmond na si kumchunguza Waziri mkuu.Sasa katika uchunguzi wao walialika watu wote wenye information wenye information kuhusiana na scandal hii.Pia walikuwa na hiari kumwita au kutomwita mtu yeyote kama waliona umuhimu upo,ili kufanikisha uchunguzi huo.Kama waliona hakuna haja ya kumwita Waziri mkuu kutoa maelezo ili kufanikisha uchunguzi huo walikuwa na hiari hiyo.
Kazi ya kamati haikuwa kum-clean au kum-implicate Waziri mkuu au mtu yeyote katika uchunguzi wao.
Kama EL anaona kawa implicated kwenye scandal ya Richard Monduli si kwa halali na kavunjiwa heshima na kuchafuliwa jina lake,sasa ndo ulikuwa wakati mzuri wa yeye kutafuta hahi yake kwa kwenda kuishitaki Kamati hiyo mahakamani.

HIvi hii kamati si ina kinga ya bunge na haiwezi kushtakiwa? naona ilikuwa jukumu lake ajipeleke mwenyewe mbele ya bunge ajieleze, ajisafishe, maana kamati ilitumwa na bunge. Lakini aliipuuza nafasi hiyo, kwa kuwa hakuwa na la kujitetea. Mbona Karamagi alijaribu kupangua baadhi ya hoja (shutuma) za kamati pale pale msalabani, japo enventually alivaa kitanzi?
 
Mzalendohalisi,
Mkuu usinielewe vibaya sikusema maswala ya handsome ila sura nzito ina maana sura yake haina kicheko ama kuonyesha furaha...Hayo mengine unayajua wewe kwani mimi sii mwanamke kujua kama jamaa ni handsome ama vipi!
Kifupi mjomba Pinda kaula lakini haonyeshi kitu chochote...sura blank, you can't read anything!!...Uswahilini tunasema sura ya FBI...
 
Mimi si mtaalam wa sheria lakini kidogo najitahidi kwenye siasa na ninavyofahamu there has to be a separation of power:
Executive ni Rais na serikali yake
Legislative ni Bunge
Judiciary ni mahakama

Sasa Bunge haliwezi kufanya kazi ya Mahakama, kamati ilifanya fact finding na ilipeleka Bungeni. Na kinachofuata ni discussion including kama hakutendewa haki na also kusikia utetezi wake. Lakini yeye kakimbia discussion.
Sasa issue hii Public prosecutor or Attorney General ndo anatakiwa kuipeleka mahakamani lakini kwa kuwa tumesikia Mwanyika kagoma kujiuzulu wanapalinda pale.
Lakini upinzani unaweza kufungua kesi mnajua, then kama hataitwa kujitetea anaweza kulalamika kwamba hakutendewa haki.
Kuhusu Warioba - kamati yake ilikuwa ni ya Rais ambayo ni tofauti na ile ya Mwakyembe. kwa hiyo nadhani ni vitu viwili tofauti.
 
wana JamboForums,
..nilitegemea bunge litaijadili ripoti ya mwakyembe. nilitegemea serikali itatoa msimamo wake kuhusu ripoti hiyo.

..waziri mkuu hata kama hakuhojiwa na kamati bado alipaswa kutoa utetezi wake ndani ya bunge. kama alikuwa na vielelezo zaidi ya vile vilivyotolewa na kamati ya mwakyembe basi Lowassa alipaswa kuvitoa ili wabunge na wananchi tupime nani mkweli nani muongo.

..binafsi nimeshangazwa sana na jinsi Lowassa alivyobwaga manyanga haraka haraka. ninavyomuelewa he rarely goes down without a fact. tuhuma na ushahidi wa kamati ulikuwa mzito na Lowassa akaona ni bora akubali yaishe.

..madai kwamba watuhumiwa hawakuhojiwa na Mwakyembe hayana msingi. watuhumiwa wote walikuwa na nafasi ya kujitetea ndani ya bunge.
 
Moe,

It is a bit unfair to call Pundit a stooge!

On Subject, Lengo la kamati lilikuwa ni kuichunguza mkataba wa Richmond. Uchunguzi huu ulifanyika kutumia Bunge na si Polisi ili kujua nafasi ya serikali na Tanesco katika sakata zima. Aidha Bunge lilichukua mamlaka ya kufanya uchunguzi baada yachombo cha kisheria cha upelelezi wa jinai na rushwa TAKUKURU kutoa majibu na matokeo ambayo si sahihi.

Bunge kama mhimili wa Serikali, lilikuwa na haki kuchunguza suala zima la Richmond na hivyo kwa maoni yangu, ni halali kusema lilikuwa likichunguza maamuzi ya Serikali Kuu kuipa RDC mkataba huo.

Hivyo basi, katika uchunguzi huu, Waziri Mkuu kama mkuu wa Serikali na mratibu wa shughuli zote za dharura anakuwa anachunguzwa.

Je alipaswa kutoa ushahidi kwa kamati ya Mwakyembe? baada ya kupitia nia ya kuundwa kwa kamati ya bunge, kupitia ripoti ya tume na maoni yetu, Edward Lowassa kama Waziri Mkuu au binafsi, alipaswa kujibu tuhuma hizi na kujitetea Bungeni na si kwenye kamati ya Mwakyembe. Yeye ndiye alikuwa mwamuzi na wa mwisho kuidhinisha mkataba. Yeye ni tofauti na Yona, Rostam, Fulgence Kazaura, Msabaha au Karamagi.

Bado yeye kama Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, anawajibu kulipa Bunge ufafanuzi wa kina wa kwa nini alitoa maamuzi mabovu kama hayo. Tunajua keshawajibika kama Waziri Mkuu, lakini hilo halimsaidii kwa maana wajibu wa kulinda nchi na mali zake kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 27 ni cha wananchi wote. Ama kwa mujibu wa katika kwa yeye kama Mbunge, mwakilishi wa wananchi, ana dhamana kubwa kulinda maslahi ya Taifa. La zaidi, Imani ya CCM pamoja na Ilani zake za 2005, amezikiuka.

Pamoja na hofu yangu ya awali kuwa kujiuzulu kwake atapata kibali cha kuondoka huru bila kuwajibika kwa Taifa na kujibu tuhuma, napenda kuwaomba wabunge wetu na CCM kufanya yafuatayo kwa Lowassa na wenzake(Hosea, Msabaha, Karamagi, Mwanyika) waliohusika na hili suala la Richmond.
  • Kwa kutumia madaraka yao, walivunja sheria za nchi na kushindwa kulinda ahadi za viapo vyao vya ubunge na uwaziri kuilinda Katiba na kulinda Taifa. Hili ni kosa la Jinai
  • Kwa ukosefu wao wa nidhamu katika kazi na kuwajibika, wamesaidia kuangamia kwa maslahi ya Taifa na usumbufu kwa Wananchi kwa kusaidia kwa kutumia madaraka yao Wahujumu wa Uchumi. Hili ni kosa la Uhujumu
  • Kwa kutumia madaraka yao, walionekana kuwa na nia za kuficha makosa yao na uhujumu ulitokea. Angalia tangu mchakato mzima wa RDC uanze, Edward Lowassa kwa kutumia madaraka yake na Edward Hosea, walipindisha ukweli na kutumia jitihada nyingi kuzorotesha uchunguzi wa kina wa suala hili la uhujumu. Hii ni hata suala hili lilipoletwa Bungeni kujadiliwa. Hili ni kosa la kuzuia mkondo wa sheria na haki ufanye kazi yake, kwa makusudi na kudhamiria kuficha makosa nauhujumu.
Tunaomba Mnyika wasilisha haya kwa wabunge wa chama chako. Wale wenye kuwasiliana na wabunge wa CCM, CUF, TLP na UDP mfanye hivyo. Mapendekezo yangu ni haya yatokee;
  1. Lowassa, Msabaha, Mwanyika, Karamagi na Hosea, wawajibishwe na Bunge kwa kutoa majibu kwa yote yaliyobainishwa kwenye ripoti hii wakiwa wamekula kiapo.
  2. Ikiridhia kuwa Uhujumu huu wa Taifa ulifanyika kutokana na Uzembe wa hali ya juu wa viongozi hawa na baada ya kuoanisha majibu yao, Bunge lipitie vifungu 68, 69, 70 na 71 na kutoa maamuzi kama watu hawa (Lowassa,Rostam, Msabaha na Karamagi) wana sifa za kuendelea kuwa Wabunge. Kama wameonekana wamekiuka miiko na viapo vyao na kushindwa kulinda katiba, basi wavuliwe Ubunge.
  3. Ikiridhia kuwa Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa TAKUKURU walishindwa kufanya kazi na kwa makusudi waliridhia UHUJUMU na nia ya Serikali (Lowassa, Msabahana Karamagi) kuficha ukweli, basi hawa pamoja na kufukuzwa kazi, hati zao za kuwa mawakili au wanasheria zifutwe.
  4. (this is wishful thinking though)Kamati Kuu ya CCM, ikipitia kanuni zake za maadili, Ilani za Uchaguzi na miongozo ya uongozi na kubaini kuwa Lowassa,Rostam, Msabaha na Karamagi walikiuka miiko ya Chama ya uongozi, basi wafukuzwe uanachama na kuwekewa pingamizi kwa miaka mitano.
Je Wabunge wetu na Raisi wetu watakuwa tayari kufanya hayo mapendekezo au yaleyale ya "yaliyopita si ndwele, tugange kwa yanayokuja"?
 
Kamati ya Richmond haikukosea kutomhoji Lowassa-Dk. Mvungi

2008-02-09 08:38:06
Na Sharon Sauwa

Mwanasheria na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi amesema Kamati ya Bunge ya Uchunguzi wa mkataba wa Richmond, haikupaswa kumhoji aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hili, jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Mvungi alisema malalamiko aliyoyatoa Bw. Lowassa na baadhi ya wabunge, kuwa hakutendewa haki na kamati hiyo kwa kutopewa nafasi, yanatokana na kutofahamu sheria.

Alisema kimsingi kama mawaziri waliohusika katika sakata hilo, wangekula kiapo na kusema tuhuma hizo zinamkabili Waziri Mkuu, hapo sheria inasema anapaswa kuitwa na kujieleza.

Alisema kinyume cha hapo basi sheria inamtaka, Waziri Mkuu kupewa nafasi mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujieleza.

``Kama wangekula kiapo (mawaziri) na kutoa tuhuma hizo chini ya kiapo, basi hapo kamati inapaswa kumwita na kumpa nafasi ya kujeleza kwa sababu wana ushahidi wa jambo hilo,`` alisema Dk. Mvungi.

Alisema alipopatiwa nafasi ya kuzungumza Bungeni, ilitakiwa Bw. Lowassa kuitetea Serikali yake na mawaziri wake wasiadhibiwe badala ya kutoa malalamiko kuwa hakupewa nafasi ya kujieleza.

``Hakuitumia nafasi hiyo kuitetea Serikali yake kwa sababu tuhuma hazielekezwi kwake binafsi, zinaelekezwa kwa mawaziri wake,`` alisema.

Mbali na hivyo, mawaziri hao wawili ndio walikuwa na nyaraka mbalimbali zinazohusiana na uchunguzi wa sakata hilo na Bw. Lowassa alibaki kuwa kama kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni na msimamizi wao tu.

Aliongeza kuwa, ``Dk. Harrison Mwakyembe, mimi sina wasiwasi naye kabisa kwanza katika wataalam bora wa katiba anaongoza, alichokifanya ni sahihi kabisa kwanza alimlinda asituhumiwe yeye binafsi,`` alifafanua.

Alisema endapo tuhuma hizo zingeelekezwa kwa Bw. Lowassa binafsi, hali ingekuwa mbaya kwa sababu ingebidi baada ya kujieleza Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye.

Kauli hiyo imekuja siku mbili baada ya Bw. Lowassa, kulalamika mbele ya Bunge kuwa kamati hiyo haikumpa nafasi ya kujieleza.

Hata hivyo, Bw. Lowassa na mawaziri wa Madini na Nishati, Bw. Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, walijiuzulu kwa nyakati tofauti wakati wakichangia hoja hiyo.
 
Ikiwa Abdul Jumbe na Sefu Hamadi walipoteza si madaraka tuu bali hata uanachama na kuwekwa ndani kwa "uhaini" kwa nini iwe vigumu kuwaweka ndani Lowassa na wenzake kwa "Uhujumu"?
 
HIli siyo gumu hivyo kuelewa. Tunapotaka utawala wa sheria ni lazima tujue gharama yake kwani sheria ni msumeno. Hatuwezi kwa sababu ya hisia, passion au kitu kingine kuamua kufanya kitu even if kitu hicho si kibaya kwa sababu ya kujiridhisha sisi.

Kama mapungufu ya sheria yapo, huo ni mjadala mwingine, lakini Kamati ilichofanya au kutofanya was within its scope. Rais kama Rais hawezi akaamka sasa hivi na kuamua kulivunja Bunge na kuunda serikali mpya n.k Hata Rais akijiuzulu mwenyewe sasa hivi Bunge linaendelea kuwepo.

Jamani, sheria ni sheria hata kama hatuipendi. Kwanini tusililia Balali naye apewe nafasi ya kujitetea na asingetimuliwa Ugavana bila ya kusikilizwa? Si Rais Kikwete alisema alipohojiana na VOA kuwa kama kuna kitu anakijutia ni kumtimua jamaa mmoja huko nyuma bila ya uthibitisho.

Sasa uthibitisho utoke wapi zaidi ya Mahakamani au Rais alikuwa na uwezo wa kutengua uteuzi wa Balali bila kupitia mahakama au kumsikiliza? Yaani tuhuma za Ernst and Young (chombo cha kukodiwa) zinaweza kumfukuzisha mtu?

Hayo ni rhetorical questions kwani majibu yake nayajua...
 
Moe,

It is a bit unfair to call Pundit a stooge!

On Subject, Lengo la kamati lilikuwa ni kuichunguza mkataba wa Richmond. Uchunguzi huu ulifanyika kutumia Bunge na si Polisi ili kujua nafasi ya serikali na Tanesco katika sakata zima. Aidha Bunge lilichukua mamlaka ya kufanya uchunguzi baada yachombo cha kisheria cha upelelezi wa jinai na rushwa TAKUKURU kutoa majibu na matokeo ambayo si sahihi.

Bunge kama mhimili wa Serikali, lilikuwa na haki kuchunguza suala zima la Richmond na hivyo kwa maoni yangu, ni halali kusema lilikuwa likichunguza maamuzi ya Serikali Kuu kuipa RDC mkataba huo.

Hivyo basi, katika uchunguzi huu, Waziri Mkuu kama mkuu wa Serikali na mratibu wa shughuli zote za dharura anakuwa anachunguzwa.

Je alipaswa kutoa ushahidi kwa kamati ya Mwakyembe? baada ya kupitia nia ya kuundwa kwa kamati ya bunge, kupitia ripoti ya tume na maoni yetu, Edward Lowassa kama Waziri Mkuu au binafsi, alipaswa kujibu tuhuma hizi na kujitetea Bungeni na si kwenye kamati ya Mwakyembe. Yeye ndiye alikuwa mwamuzi na wa mwisho kuidhinisha mkataba. Yeye ni tofauti na Yona, Rostam, Fulgence Kazaura, Msabaha au Karamagi.

Bado yeye kama Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, anawajibu kulipa Bunge ufafanuzi wa kina wa kwa nini alitoa maamuzi mabovu kama hayo. Tunajua keshawajibika kama Waziri Mkuu, lakini hilo halimsaidii kwa maana wajibu wa kulinda nchi na mali zake kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 27 ni cha wananchi wote. Ama kwa mujibu wa katika kwa yeye kama Mbunge, mwakilishi wa wananchi, ana dhamana kubwa kulinda maslahi ya Taifa. La zaidi, Imani ya CCM pamoja na Ilani zake za 2005, amezikiuka.

Pamoja na hofu yangu ya awali kuwa kujiuzulu kwake atapata kibali cha kuondoka huru bila kuwajibika kwa Taifa na kujibu tuhuma, napenda kuwaomba wabunge wetu na CCM kufanya yafuatayo kwa Lowassa na wenzake(Hosea, Msabaha, Karamagi, Mwanyika) waliohusika na hili suala la Richmond.
  • Kwa kutumia madaraka yao, walivunja sheria za nchi na kushindwa kulinda ahadi za viapo vyao vya ubunge na uwaziri kuilinda Katiba na kulinda Taifa. Hili ni kosa la Jinai
  • Kwa ukosefu wao wa nidhamu katika kazi na kuwajibika, wamesaidia kuangamia kwa maslahi ya Taifa na usumbufu kwa Wananchi kwa kusaidia kwa kutumia madaraka yao Wahujumu wa Uchumi. Hili ni kosa la Uhujumu
  • Kwa kutumia madaraka yao, walionekana kuwa na nia za kuficha makosa yao na uhujumu ulitokea. Angalia tangu mchakato mzima wa RDC uanze, Edward Lowassa kwa kutumia madaraka yake na Edward Hosea, walipindisha ukweli na kutumia jitihada nyingi kuzorotesha uchunguzi wa kina wa suala hili la uhujumu. Hii ni hata suala hili lilipoletwa Bungeni kujadiliwa. Hili ni kosa la kuzuia mkondo wa sheria na haki ufanye kazi yake, kwa makusudi na kudhamiria kuficha makosa nauhujumu.
Tunaomba Mnyika wasilisha haya kwa wabunge wa chama chako. Wale wenye kuwasiliana na wabunge wa CCM, CUF, TLP na UDP mfanye hivyo. Mapendekezo yangu ni haya yatokee;
  1. Lowassa, Msabaha, Mwanyika, Karamagi na Hosea, wawajibishwe na Bunge kwa kutoa majibu kwa yote yaliyobainishwa kwenye ripoti hii wakiwa wamekula kiapo.
  2. Ikiridhia kuwa Uhujumu huu wa Taifa ulifanyika kutokana na Uzembe wa hali ya juu wa viongozi hawa na baada ya kuoanisha majibu yao, Bunge lipitie vifungu 68, 69, 70 na 71 na kutoa maamuzi kama watu hawa (Lowassa,Rostam, Msabaha na Karamagi) wana sifa za kuendelea kuwa Wabunge. Kama wameonekana wamekiuka miiko na viapo vyao na kushindwa kulinda katiba, basi wavuliwe Ubunge.
  3. Ikiridhia kuwa Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa TAKUKURU walishindwa kufanya kazi na kwa makusudi waliridhia UHUJUMU na nia ya Serikali (Lowassa, Msabahana Karamagi) kuficha ukweli, basi hawa pamoja na kufukuzwa kazi, hati zao za kuwa mawakili au wanasheria zifutwe.
  4. (this is wishful thinking though)Kamati Kuu ya CCM, ikipitia kanuni zake za maadili, Ilani za Uchaguzi na miongozo ya uongozi na kubaini kuwa Lowassa,Rostam, Msabaha na Karamagi walikiuka miiko ya Chama ya uongozi, basi wafukuzwe uanachama na kuwekewa pingamizi kwa miaka mitano.
Je Wabunge wetu na Raisi wetu watakuwa tayari kufanya hayo mapendekezo au yaleyale ya "yaliyopita si ndwele, tugange kwa yanayokuja"?

Rev Kishoka

Ujumbe utafika.

Nina maswali na masuala kadhaa ya kuchagiza huu mjadala-

1. Ofisi ya Waziri Mkuu ikiitwa kutoa ushahidi- waziri mkuu hajaitwa?

2. Kwanini Lowassa alikimbia kabla ya kujibu hoja? Si alikuwa msemaje wa kwanza? mbona ametoa malalamishi mafupi tu ambayo hata alishindwa kuyathibitisha? Aliita kamati imesema uwongo na kutumia magazeti ya udaku! Bahati yake Spika aliamua kufunika kombe manake. Na kwa kweli kile kipindi cha mapumziko ya mchana kilifanya watu wajipange. Jioni ilikuwa show nzuri tu, laiti kama ile asubuhi mambo yangeendelea tungekuwa tunasema mengine hivi sasa.

3. Bunge lijadili; wale mashahidi waliokwepa kuja kutoa ushahidi ambao ni wabunge wajadiliwe- waulizwe maelezo yao hadharani, wajieleze bungeni. Wasisingizie tena kuwa safarini/

4. Yale maelezo ya Bangusilo yaliyotolewa pembeni nje ya oath, yahojiwe na kuthibitishwa bungeni. Msabaha si mbunge bado? Kazaura naye aeleze aliposema ni mradi wa wakubwa alimaanisha nini. Hawa nao kwa maoni yangu wameidanganya kamati. Wamesema uwongo chini ya kiapo na kuusema ukweli pembeni!

5. Suala aliloibua Dr Slaa kwamba kuna tuhuma nyaraka za Richmond zimebadilishwa BRELA kwamba wamiliki wanaotajwa sio wamiliki waliosajiliwa awali ni serious allegation. Bunge lazima lijadili wakina RICHMOND wenyewe wajulikane.

6. Mengine hayo ya mabadiliko ya kisheria, kimuundo, hatua za kinidhamu na za kisheria yanajieleza yenyewe. YATEKELEZWE.

Nitatafuta wasaa niichambue ripoti yote kwa kina. Bado bunge linawajibu wa kujadili ripoti kwa kina. Uteuzi wa baraza jipya usiwe kisingizio cha kuacha mjadala wa kisingizio kuwa ni watu wapya. Alhamasi na ijumaa moto uwake kama kawaida.

JK kwanini asiruhusu ripoti kamili ya EPA nayo ikaenda bungeni? Kama hofu ni kuharibu ushahidi kabla ya hatua za kimahakama kwamba watuhumiwa watajificha mbona hii ya Richmond ilikuwa na sura hiyo hiyo lakini imeenda?

By the way, audit report ya taasisi ya umma toka lini ikawa siri hata kwa wabunge?

Scandal ya BOT ikijadiliwa tena kwa uwazi na kwa kina katika maeneo yote sitashangaa kama JK atalazimika kuwaondoa tena baadhi ya mawaziri wapya wengine atakaowateua kesho!

JJ
 
Rev Kishoka

Ujumbe utafika.

Nina maswali na masuala kadhaa ya kuchagiza huu mjadala-

1. Ofisi ya Waziri Mkuu ikiitwa kutoa ushahidi- waziri mkuu hajaitwa?

2. Kwanini Lowassa alikimbia kabla ya kujibu hoja? Si alikuwa msemaje wa kwanza? mbona ametoa malalamishi mafupi tu ambayo hata alishindwa kuyathibitisha? Aliita kamati imesema uwongo na kutumia magazeti ya udaku! Bahati yake Spika aliamua kufunika kombe manake. Na kwa kweli kile kipindi cha mapumziko ya mchana kilifanya watu wajipange. Jioni ilikuwa show nzuri tu, laiti kama ile asubuhi mambo yangeendelea tungekuwa tunasema mengine hivi sasa.

3. Bunge lijadili; wale mashahidi waliokwepa kuja kutoa ushahidi ambao ni wabunge wajadiliwe- waulizwe maelezo yao hadharani, wajieleze bungeni. Wasisingizie tena kuwa safarini/

4. Yale maelezo ya Bangusilo yaliyotolewa pembeni nje ya oath, yahojiwe na kuthibitishwa bungeni. Msabaha si mbunge bado? Kazaura naye aeleze aliposema ni mradi wa wakubwa alimaanisha nini. Hawa nao kwa maoni yangu wameidanganya kamati. Wamesema uwongo chini ya kiapo na kuusema ukweli pembeni!

5. Suala aliloibua Dr Slaa kwamba kuna tuhuma nyaraka za Richmond zimebadilishwa BRELA kwamba wamiliki wanaotajwa sio wamiliki waliosajiliwa awali ni serious allegation. Bunge lazima lijadili wakina RICHMOND wenyewe wajulikane.

6. Mengine hayo ya mabadiliko ya kisheria, kimuundo, hatua za kinidhamu na za kisheria yanajieleza yenyewe. YATEKELEZWE.

JJ

mkuu, make sure kina zitto wanaask kwa mkataba wa dowans kuvunjwa asap. hakuna cha mahakama kwa sababu dowans ni kampuni ya uongo na owners tunawajua wote.

richmond llc = dowans = edoros
 
mkuu, make sure kina zitto wanaask kwa mkataba wa dowans kuvunjwa asap. hakuna cha mahakama kwa sababu dowans ni kampuni ya uongo na owners tunawajua wote.

richmond llc = dowans = edoros

Rostam aulizwe bungeni; Dowans ni kampuni ya nani? Mbona P.O Box na email ya Kampuni yake ya Caspian imetumiwa na Dowans? Na kwanini wafanyakazi wengine kwa mujibu wa ripoti wanafanya kazi katika kampuni zote mbili?

Tanzania itumie tu ule msingi wa kisheria wa 'nyaraka hii sio yangu' katika kuukana huo mkataba na kutaka refund. Tatizo letu ni kuwa tunafanya usanii hata kwenye masuala ya kitaifa.

Kabla ya kutafuta chenji yetu ya Richmond/Dowans tumuulize kwanza Kikwete kile 'chajuu' cha RADA si aliahidi kitarudishwa? Sasa mbona wakina Mramba na Mkapa wanakwenda kupunzika bila 'soo' hilo kumalizika? Tutaamini vipi kwamba hili la sasa litafikishwa mpaka mwisho?

JJ
 
........................5. Suala aliloibua Dr Slaa kwamba kuna tuhuma nyaraka za Richmond zimebadilishwa BRELA kwamba wamiliki wanaotajwa sio wamiliki waliosajiliwa awali ni serious allegation. Bunge lazima lijadili wakina RICHMOND wenyewe wajulikane......................

John

hiyo namba 5 yako......ni NZITO SANA.......................na kijana aliyehusika ana Jumba pale Chang'ombe na Segerea pia zote ni za kifahari........fuatilia wakati wa sherehe ya ufunguzi kibosile/vibosile gani alikuwepo/walikuwepo......halafu utaniambia hii ishu ilivyo complicated.........MAFIA STYLE!!!..........halafu wanajifanya kuwa ni wafanyabiashara as a cover up!!!
 
Back
Top Bottom