Naomba kuuliza, maana mimi siyo mtaalam wa sheria. Kuna paragraph moja kwenye report inasema kwamba iwapo Msabaha, Mwakapugi na Balozi Kazaura wangemtaja EL kwamba anahusika basi Kamati ingeweza kumhoji kwa kiapo.
Juzi Dr. Mvungi alisema kwamba kitendo cha kamati kumhoji EL akiwa PM ilikuwa ina amount kwenye situation ya impeachment kitu ambacho ni cha kikatiba zaidi. Swala la kura ya kutokuwa na imani na PM lazima kuwe na grounds za kueleweka. Kwa hiyo Kamati haikuwa na nguvu ya kumwita kumhoji ili kupata maelezo ya upande wake. Hapa inabidi watu wajiulize, je, ni kwanini Msabaha na Balozi Kazaura walikubali kusema "bangusilo" wakiwa nje ya kiapo na hawakusema wakiwa kwenye kiapo? Nadhani hapa kuna fumbo kubwa sana na vigogo hao hawakutaka kuleta balaa ya impeachment na walidhani kwamba kwa kufanya hivyo wangekuwa wanamtetea PM!
Conclusion ya Kamati iko wazi, imesema ushahidi wa mazingira, mawasiliano, na kiburi cha Wizara ya Nishati na Madini vina m-implicate EL. Paragraph iko hapa:
Kwa hiyo mimi naona tu kwamba Mzee EL alikuwa anatafuta mwanya wa kutokea ili aonekane ameonewa. Afterall atakuwa anaona amekufa kiume, lakini ningeona amekufa kiume zaidi iwapo angepangua hoja moja baada ya nyingine na finally akasema kwamba kwa kuwa amechafuliwa sana na report ya tume anaamua kubwaga manyanga. Hakujibu hata hoja moja na pia hata alipobanwa na Selelii akafuta claims nyingi na ikabaki moja kwamba ni mstari mmoja tu wa kwamba RDC ni mradi wa EL na RA. Lakini hao si maneno ya Kamati, bali ni maneno ya Balozi Kazaura na Mzee wa Bangusilo. Msabaha kwenye uteteji wake hakukanusha kutamka maneno hayo, so kuituhumu Kamati kwamba ilimsingizia bado naona ni kichekesho. Alitakiwa ambane Msabaha na Kazaura kama kweli RDC ni mali yake!