In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Nitoeni ushamba jamani kabla sijakurupuka hapa.

Hivi, hii tume (ref: case husika), iliundwa KUSHTAKI/PROSECUTE ama KUPELELEZA tu?

Nisaidieni jamani, sheria imenipiga chenga.
 
wana JF
issue ya natural justice imekuwa blown out of proportion. kwa kawaida natural justice huwa ni rule of procedure katika administrative tribunals (baraza or quasi judicial bodies) ambapo mamlaka husika kabla haijatoa maamuzi ( decision ) yanayoweza kuwa na athari mbaya kwa mtumishi basi wanatakiwa wamsikilize na pia mtumishi ajiridhishe kwamba hawakuwa na upendeleo ( rule against bias). mtumishi ambaye anaona kaonewa anaweza kuiomba mahakama ifanye mapitio (judicial review) ili kuona kama baraza lilifuata misingi ya natural justice.

now coming to our 'friend' lowassa.

1. kamati teule ya bunge ( parliamentary select committee) haikumuita lowassa kwa vile huko nyuma, kuna precedent ambapo spika alitoa maelekezo kwamba kwa uzito wa wadhifa wake, lowassa asiitwe mbele ya kamati. hakuna recodi kwamba lowasa alisisitiza naye ahojiwe kinyume na maagizo ya spika!wakati huo aliona hiyo issue imetulia!

2. Pili kuna ushahidi wa kutosha kabisa kimaandishi kwamba lowassa amehusika kuweka shinikizo kuipa contract richmond siyo lazima ahojiwe yeye binafsi ili kujua ukweli.

3. kamati teule ya bunge haikutoa maamuzi (decision ) bali bali imefanya finding na kupendekeza hatua kadhaa kuchukuliwa and mark you....there was no concrete suggestion related to lowasa. walimuacha ajikaange na mafuta yake mwenyewe. (here natural justice does not apply).

4. katika mabunge mengine ya commonwealth, mhusika anaruhisiwa kupinga ripoti ya kamati teule ( can appeal challenging an adverse finding of the select committee ) . ripoti ya richmond iliwasilishwa kwanza kwa viongozi wakuu serikalini akiwemo lowassa kabla ya kusomwa bungeni. at no time lowassa alisisitiza ahojiwe. instead yeye na marafiki zake akina chenge baada ya kujua kilichomo kwenye ripoti wakawa wanajitahidi kuizima isisomwe bungeni! lakini as the wise saying goes 'siku ya kufa nyani, miti yote huteleza!!

5. mojawapo ya mapendekezo yaliyosahaulika na kamati ya mwakyembe ni kuona kwamba lazima viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakae pembeni kwanza wakati kamati inaanza kazi yake. hii itatoa mwanya kwa kamati kufanya kazi yake kwa uhuru bila kuzingatia wadhifa wa mtu, na pia watendaji walio chini wataweza kutoa taarifa na ushirikiano kwa kamati bila woga. kumekuwepo na ushahidi wa kughushi nyaraka ili kuchafua ushahidi (re utaratibu wa kimasjala), watu wazima na akili zao kusema uongo katika tume ili kumlinda mkubwa haya yote yamejidhihirisha katika ripoti ya mwakyembe. Je lowassa angehojiwa si ndio angevuruga kabisa?

6. lowassa yeye issue yake ni ku-clear jina lake. lakini yeye kama waziri mkuu, alikuwa na miaka miwili ya kuhakikisha kwamba madudu aina ya richmond hayatokei. sasa baada ya taifa kupoteza billion 200 and still counting ndiyo anaanza kulia? wakati taasisi ya kuzuia rushwa ilipotoa clean bill....hakulalamika aliona wamefanya kazi super! kikwete naye akasema ni uzushi, kelele za wapinzani hazimyimi usingizi! sasa yako wapi?

8. Taarifa ya CAG imeonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tuwa 2006, serikali ya tanzania na taasisi zake zilipoteza shs billioni 700...katika mahesabu haya richmond haimo. Je lowassa kama waziri mkuu amemuwajibisha nani? ama mkaguzi mkuu wa serikali naye anapika majungu?

7. lowassa alikuwa ana occupy a political post. he was not a civil servant or an empoyee of the cilic service. therefore hana haki ya msingi kwamba lazima asikilizwe kabla ya 'kuachichwa ngazi' . kama mawaziri wengine yeye ni mteule wa rais and he serves at the pleasure of the president, who can dismiss him without giving him a hearing! na hawezi kulalamika kwamba rais hakumsikiliza. kikwete alikuwa na nafasi ya kukataa barua ya kujiuzuru kwa lowassa hadi lowassa asikilizwe. Why didnt he choose that option especially kwa vile lowassa kasema waziwazi bungeni kwamba ripoti ya tume ni uongo na uzushi wa maadui zake wa kisiasa?

8. dr mwakyembe has impeccable credentials in constitutional law na tunaimani kwmba in their wisdom kamati ilishabaini kwamba taifa halitapata hasara kwa kutomsikiliza lowassa. he made himself irrelevant. kama lowassa anaona kaonewa the road is clear for him to challenge the findings of the select committee. tuone kama atakuwa na jeuri hiyo. (rafiki zake waliokumbwa na kashfa ya benki kuu, mpaka leo hakuna hata mmoja aliyefungua kesi mahakamani licha ya kutishia kufanya hivyo.) kulikoni?

Aluta continua!
 
wana JF
issue ya natural justice imekuwa blown out of proportion. kwa kawaida natural justice huwa ni rule of procedure katika administrative tribunals (baraza or quasi judicial bodies) ambapo mamlaka husika kabla haijatoa maamuzi ( decision ) yanayoweza kuwa na athari mbaya kwa mtumishi basi wanatakiwa wamsikilize na pia mtumishi ajiridhishe kwamba hawakuwa na upendeleo ( rule against bias). mtumishi ambaye anaona kaonewa anaweza kuiomba mahakama ifanye mapitio (judicial review) ili kuona kama baraza lilifuata misingi ya natural justice.
Aluta continua!

Mkuu salaam
Nakubaliana nawe 100% kwa namna ulivyoangusha vipengele na details hapa. Ila kuna kitu kimoja ambacho sijakielewa labda nina matatizo ya lugha. Katika mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe lilitumika neno WAWAJIBISHE, au WAWAJIBIKE. Hii ina maana gani?? au kujiuzulu na kukaa pembeni ndiyo kuwajibika?

Na ninapinga kwa nguvu zote wale wanaompongeza Lowasa kwa kujiuzulu, wanataka ionekane kama ni jambo la kawaida ili kuosha akili za watanzania kuwa jamaa si fisadi ila ametajwa tu. Ninadhani hapa kuna turufu inataka kuchezwa na CCM, Ndugu yangu Zitto upo?? natumaini Manyika umenisoma. Pia kwa nini CCM haijatoa tamko la kuunga au kukanusha??
IPO NAMNA HAPO SI BURE!
 
Waingereza walikuja na concept ya responsibility kwa maana ya kwamba kiongozi aliyepewa dhamana ya umma ni 'uungwana akiwajibika' kwa makosa/uzembe ama uliosababishwa na yeye mwenyewe ama na wale walio chini ya uangalizi wake.

hawakuishia hapo. walipanua wigo wa hii concept ya uwajibikaji na kuja na 'collective responsibility' has ikilihusu baraza la mawaziri. iwapo uamuzi wa baraza la mawaziri umepelekea madhara, hata kama mtekelezaji ni wizara moja wapo....baraza zima linawajibika.

sasa tukija kwa mheshimiwa lowassa. let us assume kwamba hakuhisika wala kunufaika vyovyoe vile na richmond. Question is 'ofisi ya waziri mkuu' ilihusika! Question is 'wasaidizi wa waziri mkuu walihusika'. inamaana hadi dr slaa na zitto kabwe wanapata habari za ufisadi wa richmond, yeye lowassa kama waziri mkuu, akiwa kila siku anapata 'intelligence briefing' hilo alikuwa halijui?

kwa maana nyingine yeye kama msimamizi alikuwa amelala usingizi mnono! sasa amekuja kuzinduka usingizini, 200 tsh billion down the drain anasema hakusikilizwa? give me a break!!!
 
Wakuu,
Nimefurahishwa sana na michango yenu hapa. Nakubaliana na wengi wenu mliochangia hapa kwamba siku za mtu kuhujumu uchumi halafu akaacha kazi au kubadilishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine zimepita. Mhujumu uchumi lazima achukuliwe hatua za kisheria na pesa warudishiwe wananchi. Hilo pekee litasaidia kupunguza ufisadi.

Kwa kipindi kirefu nimekuwa najiuliza kwanini viongozi wetu hawaogopi kuiba? Kwanini uwizi hauishi? Moja ya majibu ni kwamba hamna accountability. Pili wezi hawachukuliwi hatua za kisheria. Na tatu wale wanaoiba wanaachiwa wabaki na mapesa yao. What do you have to loose if you know you can steal $3 million,quit your job, and nothing will happen? Ndugu zangu hii system haitakwisha kamwe kama hamna mabadiliko.

Wahujumu uchumi kama wakina Lowassa na kundi lake kubwa lazima wafukuzwe kazi, wataifishwe mali zao, na watiwe ndani. Hilo litakuwa fundisho kubwa kwa viongozi wa baadaye na nina uhakika litapunguza uwizi.
 
Mie nashangaa watu pamoja na yeye Lowassa kudai kuwa hakutendewa haki kwa sababu hakuhojiwa. Hii kamati kazi yake ilikuwa ni kuchunguza uhalisia wa Richmond pamoja na taratibu zote zilizotumika katika sakata hiyo. Hata hivyo kwa jinsi nilivyoielewa ile ripoti ni kuwa ile kamati ya Mwakyembe ilitoa nafasi kwa yeyote aliyekuwa na info juu ya Richmond pamoja na evidence kuhudhuria mahojiano nao. Na kuna wengine walijulikana kuwa walikuwa na info lakini hawakutaka kwenda na ikabidi waitwe kwa summons. Kama ijulikanavyo kwa Tanzania, mtu mzito kama PM kuhojiwa na kamati is really hard lakini kama Lowassa angekuwa na nia njema na nchi na wakati huo akijua kuwa alikuwa na evidence kibao kwa nini hasingekwenda kwa hiari yake mwenyewe kwenye hiyo kamati na kueleza alichojua yeye???????? Nafikiri alikuwa bado na ile dhana kuwa "ALIYEKO JUU MSUBIRI ATASHUKA" Siku hizi hiyo dhana haipo tena, dhana iliyopo sasa hivi ni "ALIYEKO JUU MFUATE HUKO HUKO" Sasa uchunguzi umefanyika na kum-implicate EL na kundi lake kwenye hiyo sakata. Dhumuni la kamati ilikuwa si kuhukumu na ndiyo maana ilitoa ONI kwa PM kuangalia cha kufanya kwa kutumia busara zake. Yeye Lowassa kakimbilia ku-resign kwa maelezo butu kuwa nia ni uwaziri Mkuu. Analilia haki haikutendeka, sawa hakuhojiwa lakini kuna Memo pamoja na barua alizoandika kutoa directs kwa Karamagi na wengineo, naamini meo na barua ziliambatanishwa kwenye ripoti hivyo yeye ndo anatakiwa atoe maelezo ya hivyo vi-memo na barua. Haki yake bado haijapotea kabisa, bado ana muda mzuri wa kusikilizwa. Hii sakata bado haijaisha na sehemu nzuri ya yeye kujieleza au kutafuta haki yake ni MAHAKAMANI. Kadai kuvunjiwa heshima, kudhalilishwa na mengineyo hadi kufikia kuachia ngazi. So the best way hapa ni kwenda MAHAKAMANI kum-clear. Ana haki kikatiba kufungua mashitaka dhidi ya kamati ya Bunge kumdhalilisha kama alivyodai yeye mwenyewe. Pamoja na kwamba mie ni MAIMUNA wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini naamini hata ndani ya Bunge unaweza kupata haki yako kama Kamati yake haikukutendea haki. Kwa hiyo huyu PM-MWATHIRIKA bado anayo nafasi ya kujitetea, vinginevyo ningemshauri hata huo Ubunge nao angeachia ingawa hilo ni suala la yeye na wananchi wa jimbo la Monduli.
 
Mkuu Mabbyjr: tafadhali edit ujumbe wako ili uweke aya (paragraphs), ututendee haki tuweze kusoma bila kufikicha macho tafadhali.
 
Hivi ule "ushahidi" wa maandishi alioutoa Lowassa kwanini tume haikuutia kwenye ripoti? au basi walau ku acknowledge tu kwamba uliletwa lakini haukuwa na maana or something of that nature...

Hivi Sitta "alipomnong'oneza Lowasa kama ana "ushahidi" wowote hiyo peke yake haikuwa ni kama juhudi za ku i undermnine kazi ya kamati?

Kuna mambo makubwa kwenye sakata hili ambayo hayaja wekwa wazi...
 
Nitoeni ushamba jamani kabla sijakurupuka hapa.

Hivi, hii tume (ref: case husika), iliundwa KUSHTAKI/PROSECUTE ama KUPELELEZA tu?

Nisaidieni jamani, sheria imenipiga chenga.

Mkuu Lizy,

Kamati iliundwa ichunguze, na hatimaye itoe mapendekezo. Katika kufanya kazi hiyo, ilipewa hadidu za rejea kama nguzo kuu za kufanyia kazi hiyo.
 
Hivi ule "ushahidi" wa maandishi alioutoa Lowassa kwanini tume haikuutia kwenye ripoti? au basi walau ku acknowledge tu kwamba uliletwa lakini haukuwa na maana or something of that nature...

Hivi Sitta "alipomnong'oneza Lowasa kama ana "ushahidi" wowote hiyo peke yake haikuwa ni kama juhudi za ku i undermnine kazi ya kamati?

..

Ted Lowa alichemsha sana ile barua eti ushahidi. Selelii, makamu mwenyekiti alimjibu: "Isingewezekana kuiweka kama ushahidi kwenye ripoti barua ambayo ilitumwa kwa spika 28.1. 2008, yaani mwezi mzima baada ya ripoti kukamilishwa na kukabidhiwa kwa spika."

Na akamweleza kuwa wasingeweza kuopachika, kwa kuwa huo si mchezo unaofanywa na kamati, "kama imezoeleka mahali kwingine lakin sisi hatuwezi kufanya hivyo."

Si hivyo tu, bali alisema hata kama wangeupata mapema, wasingeutumia, kwa kuwa ushahidi walioupata ulitosha...walijiridhisha.Ted macho chini, uso mwaaa...Nikashangaa sana, hivi hakuna mshauri angemkataza utetezi wa kiinga vile kweli? Maana kwa namna fulani alijiumbua sana juu ya hiyo document kutaka iwe sehemu ya ushahidi.

Kuna mambo makubwa kwenye sakata hili ambayo hayaja wekwa wazi.
 
Hivi ule "ushahidi" wa maandishi alioutoa Lowassa kwanini tume haikuutia kwenye ripoti? au basi walau ku acknowledge tu kwamba uliletwa lakini haukuwa na maana or something of that nature...

Hivi Sitta "alipomnong'oneza Lowasa kama ana "ushahidi" wowote hiyo peke yake haikuwa ni kama juhudi za ku i undermnine kazi ya kamati?

Kuna mambo makubwa kwenye sakata hili ambayo hayaja wekwa wazi...

Chief Masatu,

That is a very good point that you brought up and honestly I never thought of it until now. Did the Speaker showed dishonesty and went against the law when he whispered something to Lowassa?

To me he had undermined the Select Committee and he should also be held accountable! To be fair, did anyone whispered to Ballali when Ernst & Young folks were about to submit the report to CAG? Does anyone in the government whispers in the ears of many Tanzanians who get in legal trouble before they are sent to jails because of some petty theft? Shame on the speaker, who, apparently, is a learned legal scholar!
 
Spika alikuwa anataka kupiku na kujiwekea nguvu za kimwinyi. Aangalie zitamtokea puani hivi karibuni!
 
Pundit,

Ni muhimu kutofautisha masuala ya kitaalamu na siasa. Mh Lowasa alipigwa dongo la kisiasa! "Legal processes" .... Mapendekezo yaliyotolewa na kamati yaangaliwe kwa mantiki hiyo.

By the way, siasa inatawaliwa na rules gani??... za aliyeko madarakani
 
huyu jamaa ni mwizi anataka nini tena, amekuwa na harakati nyingi sana za hapa na pale za kujisafisha lakini hakuna kitu, yeye atulie watu wamemchoka.
 
Jf
hatuna muda mchafu kujadili uchafu wa wazi kama huu
kama njaa yako ni yako usitushirikishe kwenye dhambi hii
 
Jana baada ya kamati ya Bunge kumaliza kutoa ripoti ya richmond na kueleza pamoja na mambo mengine kuwa kuwajibika kwa viongozi wa kisiasa kumetosheleza nilikutana na watu ambao walikuwa wakijutia chuki waliyoijenga kwa aliyekuwa waziri mkuu bw. Lowasa na kusema kuwa kumbe ni kweli issue ilikuwa ni uwaziri mkuu na mengine yote yalikusanywa tu, nikajiuliza inaama lowasa alifanyiwa fitna?
 
Hata mimi nadhani ndivyo ilivyo,maana sasa kinachoonekana ni unafiki mtupu.
 
kama nchi hii ingekuwa ina sheria zinazowabana viongozi, wasiweze kuwa miungu mtu, ningemchagua Lowassa, lakini until then, bora muungwana mwenzetu, singependa kurudia ya awamu ya tatu ya kulazimishwa kuuza kila kitu kwa seli kama vile vina taka kuexpire. Hadi eti mikataba ya madini lazima isigniwe mapema la sivyo kitatudodea!!

jamani! kweli tumetoka mbali!

Mnakumbuka wale Tanesco walivyokataa kufungulia mlango netgroup solutions FFU wakaja wakawatoa kwa nguvu na matokeo yake?

Mnakumbuka jinsi TTCl ilivyouzwa na kumegwa na celtel kuingia kinyemela na matokeo yake!?

Mnakumbuka jinsi Songosongo ilivyoibuka upya na matokeo bei za umeme zinapanda badala ya kushuka?

Mengi mno tulikubali kwa kushinikizwa na kukosekana kwa sheria na watekelezaji wa sheria hizo, nidhamu za woga ndio zinazosumbua nadhani.

Si kama Pinda anavyosema eti wataalamu wa kuingia mikataba hatuna. si kweli hata kidogo.
jamani nampenda Lowassa lakini namuogopa mie!!
 
Bugurunkwamnyamani,

Jamaa ni mwizi, period! Haitaji hata kulizwa this is now general knowledge to everybody in TZ. Kama ana cha kujitetea si angesema pale bungeni kila mtu akasikia na kujisafisha. Hotuba yake haina hata chembe ya kujitetea ukichulia kuwa alishaona ripoti tofauti na wenzake waliohojiwa kichwakichwa. Yeye kutuambia kuwa hakutendewa haki kwa kutokuhojiwa haitusaidii sisi wala yeye mwenyewe. Anachotakiwa kufanya ni kujisafisha kitu ambacho ameshindwa. Naomba majibu ya maswali yafuatayo:
1. Mbona sasa alikuwa kimbelembele kujaribu kuzuia ripoti isiwasilishwe bungeni?
2. Mbona alijaribu kuwatisha mawaziri na kuwanga'ang'aniza waitetee ripoti ambayo hata hawajaiona.
3. Mbona alitamka hadharani kuwa serikali ilikuwa ina nia nzuri kwenye swala la Richmond.
4. Atwambie kama ni kweli ripoti hii aliisikia na kuiona siku ile iliposomwa.

Kama huyu fisadi alijuwa kuwa hana makosa kwanini katika hotuba yake aliwatisha wenzie kuwa '' Tukianza kuumbuana hakuna atakayepona". Hii inaashiria kuwa alitegemea kuwa wenzie wangemtetea kama walivyozoea lakini badala yake wakamuacha azame ikiwa pamoja na Jakaya mwenyewe!!! Lowassa alikuwa anatoboa mtumbwi baharini akiwa na wenzie kwenye ngalawa ikabidi WAMTOSE!!!
 
Back
Top Bottom