In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
837
Naona JF kama kawaida yetu tumeingia na vigele gele wakati ukweli ni kuwa MWAKYEMBE kama mwanasheria anajua fika kuwa kulikuwa na umuhimu wa kumhoji mtuhumiwa mkuu katika hili skendo bwana LOWASSA lakini hakufanya hivyo

Huu si uzushi wala nini na LOWASSA mwenyewe alisema hilo katika hotuba yake

sasa guys lets take a back seat and look at huyu MWAKYEMBE na kamati yake walikuwa wanajaribu kuficha nini ? huwezi kuendesha mambo haya based on emotions na kwangu naamini kuwa one is innocent till proved otherwise na in this case Lowassa hakutendewa haki. Simpendi na sina ulazima wa kumpenda lakini haki yake mpeni


HOTUBA YA KUJIUZULU YA LOWASSA:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.

Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni
"Natural Justice".


Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.


Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri.
Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.


Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.


Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.

Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".


+++++++++++++++++++++

KAMATI YA MWAKYEMBE NAYO:


Kamati Teule inapendekeza yafuatayo:

(1) Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) haina nguvu ya kutosha ya kuiwezesha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Ununuzi wa Umma unaboreshwa kwa kuongeza ushindani wa ukweli na uwazi na hivyo kuipa Serikali thamani halisi ya pesa zake. Kamati Teule inapendekeza kwamba sheria hii ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale Sheria na Kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.

(2) Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni taasisi ya ununuzi (procurement entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na taarifa zake kuwasilishwa Bungeni.

(3) Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme. Kamati Teule inatoa rai kwa Serikali kuwa mikataba yote hii ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

(4) Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme. Kamati Teule inaitaka Serikali kutathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi, na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na Kampuni kubwa ya Kimataifa ya Pratt & Whitney na utambulisho wa Mzungu mmoja kwa jina la John Perun kama mwakilishi wa Pratt & Whitney, mambo ambayo Kampuni hiyo kubwa ya Kimataifa imeyakanusha vikali.

(5) Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini ama ubinafsi katika kuiwakilisha Serikali. Kwa mfano, kushindwa kutambua ukosefu wa sifa za kikampuni za Richmond Development Company LLC; kushindwa kuishauri Serikali kuifanyia kampuni hiyo ukaguzi wa awali (due deligence) au ukaguzi baada ya uteuzi (post qualification); kushindwa kutambua tofauti kati ya consortium agreement na proprietary information agreement; kushindwa kuona dosari kisheria za proprietary information agreement; kushindwa kuona tofauti kisheria kati ya Richmond Development Company LLC, RDEVCO,RDVECO na RDC, majina ambayo wamiliki wa Richmond Development Company LLC walikuwa wanayatumia kwa kubadilisha badilisha (interchangerbly) kwa makusudi; kushindwa kuwashauri Wajumbe wa GNT kwamba business card si mbadala wa hati mahsusi kisheria; kushindwa kuishauri Serikali kuhakikisha kuwa muhtasari wa majadiliano kati ya Kamati ya Serikali ya Majadiliano (GNT) na Richmond Development Company LLC ambao ulizingatia baadhi ya maslahi ya nchi, uwe sehemu ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC; kushindwa kuishauri Serikali kutumia fursa iliyokuwepo wazi ya kuvunja Mkataba baada ya Richmond Development Company LLC kushindwa kutekeleza sehemu yake ya Mkataba; kushindwa kuhudhuria idadi kubwa ya vikao muhimu vya majadiliano;n.k. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye katika majadiliano yake na Kamati Teule alionyesha kutokuelewa kabisa kilichokuwa kinatendeka na wasaidizi wake, na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili wa Serikali Donald Chidowu, ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yeyote, wawajibishwe na Mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.

(6) Katika mikataba yote na makampuni ya nje Serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu katika kupata taarifa kamili za kampuni hizo, kama vile wanahisa, mitaji na anwani. Aidha, Ofisi zetu za Ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya Serikali.

(7) Madhumuni ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC yalikuwa kuzalisha umeme wa dharura kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12) tu.
Muda huo ungeweza kuongezwa baada ya kutathmini hali ya ongezeko la maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme nchini. Kabla ya muda wa tathmini hiyo haujafikiwa, wakati majadiliano yakiendelea GNT ikaongezea Richmond Development Company LLC muda wa kukodi mitambo hiyo kuwa miaka miwili (2). Kamati Teule haikuona vielelezo vyovyote vilivyojenga uhalali kwa GNT kuongeza muda huo. Uamuzi huo umeliongezea Taifa mzigo mkubwa wa gharama zisizokuwa za lazima. Mathalan, kwa upande wa capacity charges tu, TANESCO itailipa Dowans Holdings S.A jumla ya shilingi bilioni 54.8 kwa kipindi kilichongezwa cha mwaka mmoja. Aidha, GNT ilishindwa kutambua ulaghai wa Richmond Development Company LLC kuhusu mwakilishi wa Pratt & Whitney na hivyo kuamini karatasi ambayo ilikuwa haijathibitishwa na mawakili na diskette zenye picha za mitambo ya Pratt & Whitney, vielelezo ambavyo Kamati Teule imegundua na kuthibitisha kuwa vilikuwa vya kugushi. Vilevile, bila kujali kwamba TANESCO ingelezimika kuilipa Richmond Development Company LLC shilingi milioni 152 kwa siku kama gharama ya kuweka vifaa vyao nchini, GNT ikakubali kilegelege kuitoza Richmond Development Company LLC shilingi milioni 12 tu kwa siku kama fidia kwa ucheleweshaji wa kuanza kuzalisha umeme kulingana na tarehe iliyokubalika kwenye mkataba. Kamati Teule inapendekeza kuwa Wajumbe wote wa GNT ambao ni maafisa waandamizi wa Serikali wawajibishwe mara moja kwa kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya Taifa.

(8) Pamoja na Uongozi wa TANESCO kubainisha mapungufu ya Richmond Development Company LLC na kutoa notisi tarehe 27 Octoba 2006 ya kusitisha Mkataba tena kwa ushauri mahsusi kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Mawakili, Wizara ya Nishati na Madini haikuupenda mwelekeo huo hivyo tarehe 28 Novemba 2006 baadaye Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Nazir Karamagi, Mb akiwa nje ya nchi Calgary, Canada alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Kazaura kuangalia uwezekano wa kuhaulisha Mkataba wa Richmond kwa kampuni nyingine. Siku tano baada ya mawasiliano hayo, yaani tarehe 4 Desemba 2006, TANESCO ikapokea barua kutoka Richmond Development Company LLC ikielezea nia ya kampuni hiyo kutumia haki yake chini ya kifungu 15.12 cha mkataba ili kuhamisha majukumu yake ndani ya mkataba kwenda kwa kampuni mpya ya Dowans Holdings S.A. Kamati Teule ilipata taarifa za ndani ya Wizara na TANESCO kuwa viongozi wa Wizara kama kawaida yao waliishinikiza TANESCO kuridhia ombi hilo la Richmond Development Company LLC kuhaulisha mkataba kwa Dowans Holdings S.A. TANESCO ikalazimika kuridhia uhaulishaji wa mkataba huu badala ya kutumia fursa iliyokuwepo ya kusitisha mkataba baada ya kutoa notisi ya siku thelathini. Kamati Teule inaamini kwamba uamuzi wa Wizara ya Nishati na Madini kuizuia TANESCO isitumie fursa ya kusitisha mkataba huo, unaashiria jinsi viongozi wetu wanavyojali zaidi faida na maslahi ya makampuni ya nje kuliko maslahi mapana ya Taifa. Tarehe 3 Desemba TANESCO kama ilivyoagizwa ikaridhia uhaulishwaji wa mkataba huo lakini kipindi ambacho hali ya maji katika mabwawa yetu ya kuzalishia umeme ilishaanza kurejea kuwa ya kawaida. Uamuzi huo umeingizia Taifa hasara kubwa. Hivyo basi Kamati Teule inapendekeza kwamba Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Nazir Karamagi, Mb aliyeshabikia sana uhaulishaji huo, awajibishwe.

(9)
Matokeo ya uchunguzi ya Kamati Teule kama yalivyoainishwa hapo juu yanadhihirisha wazi jinsi Taifa lilivyotumbukizwa kwenye hasara kubwa kutokana na mkataba huo wa Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A, kinyume na taarifa iliyotolewa na TAKUKURU (wakati huo TAKURU) kwamba Taifa halikupata hasara yoyote. Taarifa ya TAKUKURU ililenga kuficha ukweli (white wash) hivyo ikaishia kujikanganya kwa kukiri kuwepo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imemong’onyoa kwa kiasi kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana ya kupambana na rushwa na sio kuipamba ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo. Kamati teule inapendekeza mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo.

(10) Taratibu za malipo ya madai ya mkataba wa umeme wa dharura zinafanywa kupitia Barua ya Dhamana ya Benki iliyofunguliwa kati ya TANESCO na benki ya CRDB ya dola za Kimarekani milioni 30,696,598 iliyofunguliwa tarehe 27 Desemba 2006. Kamati Teule imethibitisha kwamba hadi kufikia tarehe 19 Juni 2007 malipo yaliyolipwa na Benki Kuu yamefikia Dola za Kimarekani 35,561,598 kiasi hicho ni zaidi ya Barua ya Dhamana ya Benki kwa dola za kimarekani milioni 4,565,000 wastani wa shilingi bilioni 5.7. Kamati Teule inashangaa ni vipi Benki Kuu iidhinishe malipo hayo
nje ya Barua ya Dhamana ya Benki iliyofunguliwa kati ya TANESCO, CRDB Bank na Dowans Holdings S.A. Kwa kuwa Benki Kuu ndio msimamizi mkuu wa akaunti maalum (Escrow Account), Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo hayo na kuhakikisha kwamba udhaifu wa namna hii haujitokezi tena hapo baadaye.

(11) Wakati umefika sasa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 (Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani, hivyo kuwaweka kwenye mtihani mkubwa wa mgongano wa kimaslahi katika maamuzi yao. Tufike mahali ambapo sheria iwalazimu kuchagua kati ya Utumishi wa Umma au biashara binafsi. Viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa (mawaziri na kuendelea) kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani hivyo kuwaweka kwenye mtihani mgumu wa mgongano wa kimaslahi.

(12) Serikali iondokane kabisa na utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini na kuhakikisha kuwa Wizara husika ina taarifa za bei halisi ya mitambo kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi. Kamati Teule ilishuhudia bei za mitambo hiyo jijini Houston, Texas Marekani kwa watengenezaji kiwandani ikiwemo kampuni ya Kawasaki Gas Turbines – Americas ambayo iko chini ikilinganishwa na bei zinazotolewa na mawakala hao, jambo ambalo lingeiwezesha Serikali kununua na kumiliki badala ya kukodi kwa muda mfupi na kwa gharama kubwa. Mathalan, MW 105 zingepatikana kwa kununua mitambo sita ya MW 17,5 kila mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 56.25 badala ya shilingi bilioni 108.7 tulizotandikwa na Richmond Development Company LLC mitambo hiyo ikibaki mali ya wakodishaji. Kwa kumalizia Kamati Teule ilithibitisha kwamba kauli iliyokuwa inatolewa mara kwa mara na baadhi ya viongozi wote tuliowahoji kwamba kipindi hicho cha ukame haikuwa rahisi kupata mitambo hiyo na ilikuwa ikigombaniwa na nchi nyingi kauli hiyo ilikuwa sio ya ukweli na upotoshaji mkubwa.

(13) Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, ambao Waziri wa Mipango Uchumi na Uwezeshaji Mhe. Dk Juma Ngasongwa (Mb) aliusifia bungeni tarehe 19 Aprili 2007 kuwa best practice wakati akijibu swali la Mhe. Masolwa C. Masolwa (Mb) Mbunge wa Bububu, umepitwa na wakati na unakiuka misingi ya demokrasia na uwajibikaji. Matokeo ya utaratibu huu ni kuwepo kwa mikataba mibovu inayoficha vipengele vinavyoibebesha Taifa mizigo mikubwa ya gharama zisizokuwa za lazima kama tulivyoainisha katika pendekezo namba 3 hapo juu. Kamati Teule inatoa wito kwa Serikali kuondokana na utaratibu huu usio na tija kwa kuzihusisha Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya mikataba hiyo. Aidha, Kamati Teule inatoa wito kwa Kamati zote za Bunge zihakikishe kuwa zinapitia mikataba mikubwa nay a muda mrefu ya kibiashara chini ya sekta zao ili kuliondolea Taifa mizigo isiyo ya lazima. Pale ambapo upatikanaji wa mikataba hiyo unakwamishwa kwa urasimu usio wa lazima Kamati zitumie utaratibu uliotumiwa na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara ya kuunda Kamati Teule yenye ufunguo wa mikataba iliyofichika.

(14) Pamoja na dharura iliyokuwa inalikabili Taifa, Serikali haiwezi kuwa kinara wa uvunjaji wa taratibu, kanuni na sheria za nchi kwa makusudi. Kamati Teule imeanisha katika taarifa hii vitendo vya ubabe, ujeuri na kiburi vilivyofanywa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini alimradi kampuni waliyoitaka iteuliwe kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote, kukaidi ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma mara tatu mfululizo na kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri lililotaka Sheria ya Ununuzi wa Umma izingatiwe, kukiuka sheria kwa makusudi kwa kuingilia mchakato wa zabuni wa taasisi nyingine ya ununuzi, kuvipuuza vyombo vya ndani vya maamuzi vya TANESCO (Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Zabuni n.k), kuilazimisha Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuridhia maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya kuibeba Richmond Development Company LLC kinyume cha sheria na taratibu n.k. Wizara hiyo katika kuibeba Richmond Development Company LLC ilifikia hatua ya kupotosha kwa makusudi ushauri wa Wizara ya Fedha uliozuia malipo ya awali ya Dola za Kimarekani Milioni 10 katika Barua ya Dhamana ya Benki ya Richmond Development company LLC. Siku iliyopotosha ilikuwa tarehe 6 Octoba 2006. Kamati Teule inapendekeza kwamba Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi. Aidha Kamishna wa Nishati Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.

(15) Utaratibu wa kuteua wakurugenzi na makamishna katika Wizara kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi za mashirika yaliyo chini ya Wizara, unazua mgongano wa kimaslahi, kudhoofisha usimamizi na uwajibikaji, hivyo Serikali iupige marufuku mara moja. Mfano Kamishna wa Nishati ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ambaye alishiriki kwenye kikao kilichowakataa wazabuni wote kuwa hawafai na kuishauri Serikali vilivyo, aliporejea Wizarani alishiriki katika kutengua maamuzi ya Bodi ya TANESCO.

(16) Uhuru mkubwa ambao viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia bila wasiwasi katika kuhakikisha kwamba kampuni waliyoitaka, Richmond Development Company LLC, inapewa zabuni ya umeme wa dharura; maelekezo ya mara kwa mara ya Waziri Mkuu kwa Wizara katika kila hatua ya mchakato huo; upendeleo wa dhahiri ambao Richmond Development Company LLC iliupata kutoka taasisi mbalimbali za Serikali k.m Kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho kilifikia hatua ya kufumbia macho baadhi ya taratibu zake za msingi ili kuipa kampuni tanzu ya Richmond Development Company LLC cheti cha uwekezaji haraka iwezekanavyo; kutotimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria; uteuzi wa mwisho wa Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kufanywa na Waziri Mkuu mwenyewe tarehe 21 Juni 2006; uamuzi wa kuiteua Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kusafishwa na TAKURU ( sasa TAKUKURU) kuwa ulikuwa wa wazi na wa haki; uamuzi wa Serikali kuizuia TANESCO isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo, ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili na Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu.

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge
 
Weka na majibu ya kamati yaliyosomwa bungeni jana jioni na kamti kupitia kwa mjumbe wa kamati Seleli, kwani hapa inaonekana kuwa kuna jitihada za kumsafisha huyu fisadi mkuu.

Ametendewa haki na mkiendeleza zitawekwa hata barua ambazo alitumiwa ili kwenda kujitetea mbele ya kamati naye hakujibu wala kwenda kwenye kamati husika.

Kuna haja ya kukaa kimya kwani mengi hapa yatawekwa hadharani ,na itakuwa ni aibu zaidi kwa huyu mkuu .

Nawataka wote msifikiri kamati haina majibu juu ya tuhuma hizi na kutapatapa kwa huyu jamaa jana .

Ndugu tetea ukiwa na ushahidi kwanza la sivyo utaumbuka bure , na pia subiri kuhitimisha mjadala j3 uone kitakachojiri humo.
 

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.


Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.


Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.


Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.


Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.


hayo ndiyo majibu ya LOWASA

mwakyembe hajaeleza kwa nini hakumhoji huyu mtuhuimiwa mkuu na hiyo ni fault

kama unazo barua weka na si kutishia
 
Bugurunkwamnyamani,

Jamaa ni mwizi, period! Haitaji hata kulizwa this is now general knowledge to everybody in TZ. Kama ana cha kujitetea si angesema pale bungeni kila mtu akasikia na kujisafisha. Hotuba yake haina hata chembe ya kujitetea ukichulia kuwa alishaona ripoti tofauti na wenzake waliohojiwa kichwakichwa. Yeye kutuambia kuwa hakutendewa haki kwa kutokuhojiwa haitusaidii sisi wala yeye mwenyewe. Anachotakiwa kufanya ni kujisafisha kitu ambacho ameshindwa. Naomba majibu ya maswali yafuatayo:
1. Mbona sasa alikuwa kimbelembele kujaribu kuzuia ripoti isiwasilishwe bungeni?
2. Mbona alijaribu kuwatisha mawaziri na kuwanga'ang'aniza waitetee ripoti ambayo hata hawajaiona.
3. Mbona alitamka hadharani kuwa serikali ilikuwa ina nia nzuri kwenye swala la Richmond.
4. Atwambie kama ni kweli ripoti hii aliisikia na kuiona siku ile iliposomwa.
 
Nimekuambia kuwa mbona huweki majibu ya kamati yaliyowasilishwa na kamati jana jioni bungeni kumjibu?
 
Ni kuwa kama unamtetea mwambie akupe taarifa kamili za ni barua ngapi aliandikiwa na kamati na alichokijibu.

Alimtuma mjumbe wake wa karibu nyumbani kwa mwakyembe usiku alienda kufanya nini?

hizo ni dokezo tuu, kama umetumwa mwambie akupe nondo sio kukubaliana na maneno yake tuu.
 
mnasema jana Lowassa alitoa statement ya uwongo Bungeni kudai kuwa hakuna aliyemhoji?

kwa nini Mwakyembe na wenzie hawakumhoji tena under oath?
 
Bugurunkwamnyamani,

Jamaa ni mwizi, period! Haitaji hata kulizwa this is now general knowledge to everybody in TZ. Kama ana cha kujitetea si angesema pale bungeni kila mtu akasikia na kujisafisha. Hotuba yake haina hata chembe ya kujitetea ukichulia kuwa alishaona ripoti tofauti na wenzake waliohojiwa kichwakichwa. Yeye kutuambia kuwa hakutendewa haki kwa kutokuhojiwa haitusaidii sisi wala yeye mwenyewe. Anachotakiwa kufanya ni kujisafisha kitu ambacho ameshindwa. Naomba majibu ya maswali yafuatayo:
1. Mbona sasa alikuwa kimbelembele kujaribu kuzuia ripoti isiwasilishwe bungeni?
2. Mbona alijaribu kuwatisha mawaziri na kuwanga'ang'aniza waitetee ripoti ambayo hata hawajaiona.
3. Mbona alitamka hadharani kuwa serikali ilikuwa ina nia nzuri kwenye swala la Richmond.
4. Atwambie kama ni kweli ripoti hii aliisikia na kuiona siku ile iliposomwa.
 
bugurunikwa mnyamani,

Hivi umeshaisoma ripoti yote ya kamati teule?...........i doubt!!

1.Kama EL ansema kuwa ripoti ni ya uongo............kwanini kajiuzulu??
2.kama kweli ripoti ni ya uongo....je huoni kuwa huu ndio ungekuwa wakti mzuri wa yeye ku-prove kuwa yuko clean....na badala yake anajiuzulu!!!!

Kukimbilia kujiuzulu ni sehemu mojawapo ya kuficha madhambi yake ambayo ameshindwa kuyatetea bungeni
 
Those who are trying to defend Lowassa, I would like to ask a few questions?

1. I think all of us know that leadership in Tanzania has always been a top-down process where the guys at the top are considered to be above the law and no one is to question them. Don't you think that this commission decided upon its jurisdiction not call upon Lowassa because it may affect the final outcome of their report?

2. If the commission collected all the documents that were evidentially strong to put Lowassa and his allies on the spot, was there a need to call him to testify? That is not for the commission to do but to submit the evidence they have collected and have the courts then summon Lowassa and his brood to court. What was presented was a report of their findings which has incriminated Lowassa and his group, so what? The commission is not a jury.

From my understanding their job was not to question Lowassa but the people directly engaged in the transaction for evidential purposes but when the top brass were implicated there was no need to question them but to have the matter presented and for necessary steps to be taken.

Lowassa knew what was coming the moment he heard that Mwakyembe was the head of the commission.

Findings of commission have never been upheld this is just the beginning.
 
Hapa kuna vitu viwili,

Law and justice, the law is an ass anyway so I do not care much for it.

So if you go the legalistic route Mwakyembe is wrong and Lowassa is technically right, because every accused has a right to defend him/herself.And dont tell me that "every Tanzanian wa invited", the PM is not simply "every Tanzanian".

But on the side of justice, clearly the report has insurmountible and otherwise unimpeachable evidence.If you did not read it just the small part that Mrs. Malecela (god bless that woman's soul, we need more like her) was reading in parliament yesterday was damning enough to put both Lowassa and Msabaha away for good. So the Commitee expressed problems with people not being able to go on record and I expressed my solution to that in another thread here.

Kwa hiyo kama unataka kuwa technical and all that good stuff, Mwakyembe amekosea na Lowassa yuko right.Lakini technicalities hizi si ndiyo ziliifanya Ripoti ya Warioba iwe toothless na mpaka leo imewekwa kwenye makabrasha tu?

In my view the end justifies the means. It may be a bad precedent and all but I am sure it does not violate the spirit of the law, which is not to unfairly prosecute an innocent person.In addition the commitee did not pass judgement on Lowassa, it merely advised him to "use his wisdom" so if he is really innocent why not issue a rebuttal and let Tanzanians judge? His conscience must be heavy on him.

The means justifies the end so to speak.
 
Those who are trying to defend Lowassa, I would like to ask a few questions?

1. I think all of us know that leadership in Tanzania has always been a top-down process where the guys at the top are considered to be above the law and no one is to question them. Don't you think that this commission decided upon its jurisdiction not call upon Lowassa because it may affect the final outcome of their report?

2. If the commission collected all the documents that were evidentially strong to put Lowassa and his allies on the spot, was there a need to call him to testify? That is not for the commission to do but to submit the evidence they have collected and have the courts then summon Lowassa and his brood to court. What was presented was a report of their findings which has incriminated Lowassa and his group, so what? The commission is not a jury.

From my understanding their job was not to question Lowassa but the people directly engaged in the transaction for evidential purposes but when the top brass were implicated there was no need to question them but to have the matter presented and for necessary steps to be taken.

Lowassa knew what was coming the moment he heard that Mwakyembe was the head of the commission.

Findings of commission have never been upheld this is just the beginning.


Asante Bi Mkubwa. Kama watu wangeelewa hii analysis yako. Iam sure it would be a step ahead katika wote wanaotaka kumlaumu Harrison na wajumbe wenzake eti hawakumuita EL kumhoji....

Pundit, heshima yako mkuu.

Mwakyembe na Kamati yake hawana kosa either way Legally or otherwise. Ile kamati haikuwa Jury au mahakama. Ilitumwa kufanya utafiti wa hii issue ya Richmond. Hebu soma vizuri terms of reference zao. Wao walipata evidence ambazo either wangemwita Lowassa au wasingemwita zisingebadilisha hitimisho lao. na hawakusema Kwamba Lowassa ni guilty au otherwise. wao walitoa ushahidi walioupata wakamuachia PM atumie busara. Swala la natural justice linakuja (ie never condemn a person unheard!) pale mtu anaposhtakiwa au kuhukumiwa bila kusikilizwa... Lowassa hakuwa condemned! It was simply the facts/findings of the commission which implicated him. In otherwise unataka kusema whoever is mentioned in that report lazima aitwe na kamati. Thats not correct. Otherwise si angeita maelfu ya watu?

Kwa lugha nyingine, waziri mkuu kama angekuwa na chochote cha kuiambia kamati (as he admitted kwamba alikuwa anasikia tetesi na minong`ono mtaani) basi angeenda kwenye tume.

Tume haikuundwa kumchunguza Lowassa. NO! Lowassa angekuwa hajatendewa haki kama tume ingetumwa kuchunguza role yake kwenye hii saga na ikatoa conclusion bila kumsikiliza. That would be wrong. But for now, Mwakyembe hana any iota of blame! Sema tuu Lowassa alitaka kuanguka kwa kujihami..last kicks 0f a dying horse.....

Jamani tujaribu kutofautisha mambo hapa.
 
Kama wameshindwa kumhoji rostam wangeweza kweli kumhoji lowassa? Jamani kama Takukuru imemlinda Lowassa, mawaziri wawili walimlinda, kamati ya mwakyembe wangepenya vp? They used the back door with the interests of the people at heart and thats wot matters...(All the circumstantial evidence point to him and thats wot lead to the conclusion of the kamati..)
 
Kisheria, napenda kukumbusha kuwa Mwakyembe hakutoa hukumu kuwa Lowassa ana hatia; yeye alifanya kazi ya prosecutor, yaani kutoa tuhuma dhidi ya Lowassa mbele ya hakimu, ambaye hapa alikuwa ni Bunge, kwa kutumia vielelezo kadhaa alivyopata kwenye uchunguzi wake. Lowasa kwa upande wake alitakiwa atoe utetezi wake dhidi ya tuhuma hizo na pia kutoa vielelezo vyake ili Bunge lilinganishe vielelezo vya Mwakyembe na vile vya Lowasa ndipo litoe hukumu.

Lowasa ameshindwa kujitetea dhidi ya tuhuma hizo na hivyo moja kwa moja akawa amekubaliana nazo, ndiyo maana aka-opt kuachia ngazi ili labda kuzuia upande wa mashitaka usipate nafasi ya kutoa vielelezo zaidi ambavyo vingeweza kuwa ni vibaya zaidi.
 
Lowassa ni Jambazi and he should be EXECUTED.

Nilitoa wazo hili kuwa watu kama hawa kina Lowasa, Mramba, Mgonja, Jiiitu Patel, na wenzake wawekwe pale mnazi mmoja na watafutwe sharp shooterz kama mia moja hivi wawachape risasi kibao za miguuni..... baada ya hapo, wananchi waruhusiwe kuwaponda mawe hadi wafilie mbali......... grrrrrrrrr
 
Huwezi kukamilisha fact finding kama hujamuuliza mtu ambaye evidence ina m point out.Sasa kama vile vimemo vyote vina a plausible explanation from Lowassa je, si ripoti inakuwa hogwash bila kumuita Lowassa?

Guys lets face it, Bimkubwa ametoa analysis nzuri tu hapo juu ambayo hata mimi nimei endorse,political machinery yetu hairuhusu mtu mkubwa kama PM akamatwe na sheria kwani tumeona hata watu kutoa ushahidi ni tatizo, but at the end of the day the end justifies the means and sometimes when you are fighting gross corruption you have to improvise, kitu ambacho Mwakyembe alifanya.Hata katika uandishi wa habari, kwa wanaofuatilia principled journalism, huwezi kuandika article kumaccuse mtu bila ya kumpa nafasi ya kujieleza na ndiyo maana wanaojua kuandika watakuambia "tulipofanya jitihada za kuongea na so and so hatukufanukiwa" au tulipewa "no comment" il mradi wakuonyeshe kuwa article yao haiko one sided.

Sasa kwa msingi huo ripoti ya Mwakyembe technically iko one sided kwa sababu haikumpa accused nafasi ya kujitetea, which is what Lowassa is hanging on.Lakini ukiisoma ripoti au hata Kumsikiliza Mama Malecela bungeni utaona evidence ni kubwa sana, halafu hata zaidi ya hivyo Lowassa hakutoa a point by point rebuttal, kitu kinachoonyesha kuwa hana la kujibu on issues, atavielezaje vimemo? atazielezaje kauli za Msabaha?

Lets be fair, technically what was done is wrong but it was necessary as this was uncharted territory.Otherwise tungekuwa na ripoti nyingine ya Warioba.
 
buguruni Kwa Mnyamani::::

kwa Upande Wa Lowassa Hakukuwa Na Haja Ya Kumwita
wakati Kuna Barua Zimezagaa Na Sign Yake,,watanzania Embu Amkeni Jamani Fumbueni Macho,..."".jiasaidie Na Wewe Utasaidika"""
mimi Nawapongeza Sana Sana Wabunge Wa Ccm Naona Wameanza
kuamka.......vita Mbele.......
wana Jf Inabidi Tuanze Kupongezana Naona Uchafu Wote Tuliokuwa Tunahangaika Nao Umeanza Kuondolewa


"""sauti Ya Wengi Sauti Ya Mungu""
 
Back
Top Bottom