Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,483
- 30,155
Kwa taarifa tunayopewa na Jeshi la Polisi nchini, kuhusu tuhuma za ugaidi zinazomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ni kuwa alipanga njama za kulipua vituo vya mafuta, Katika hoteli yake ya Aishi, iliyopo huko mkoani Kilimanjaro, Kati ya mwezi May na August mwaka Jana.
Swali la kwanza ninalowauliza hao Polisi wetu ni kwanini huku mkijua kuwa "gaidi" Mbowe, alipanga njama za kulipua vituo vya mafuta nchini, tokea mwaka Jana, mkamuachia akawa anaendelea na shughuli zake, hadi majuzi wakati anaandaa kongamano la Katiba mpya ndiyo mkamkamata?
Kama jukumu lenu na 1 nchini ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, je kwa kumwachia "gaidi" Mbowe atanue anavyotaka, hivi hamjui hatari kubwa mno mliosababisha wa usalama wa raia n a mali zao wa nchi hii?
Swali la pili kwa hao Polisi wetu, iwapo ni kweli kuwa "gaidi" Mbowe alipanga njama za kulipua vituo vya mafuta, ni kwanini hamjakitaja angalau kituo kimoja, Kati ya hivyo vilivyopangwa kulipuliwa?
Swali la tatu ninalowauliza hao Polisi wetu, mmetueleza kuwa "gaidi" Mbowe alikuwa akifadhili vitendo hivyo vya kigaidi, lakini hamkutujulisha ni kwa kiwango gani cha pesa alichofadhili Katika kipindi hicho?
Kama kweli Jeshi la Polisi linao huo ushahidi, kama alivyojitapa IGP Sirro, tunaliomba Jeshi hilo lijitokeze hadharani na kunijibia maswali yangu hayo.
Ni dhahiri kama Jeshi la Polisi lisipojitokeza hadharani na kunijibia maswali yangu, basi wananchi tulio wengi tutaamini kuwa kesi hii ni ya kisiasa na ya kubambika.