Jeshi la Polisi tumieni Sheria na taratibu zilizopo kudhibiti mtu yeyote mwenye viashiria vya kuvuruga amani nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb), ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia sheria na taratibu zilizopo kudhibiti mtu yeyote mwenye viashiria au lengo la kuvuruga amani hapa nchini.

Mhe. Sagini ametoa maagizo hayo alipotembelea na kukagua Kituo kidogo cha Polisi Bwanga Wilayani Chato katika Mkoa wa Geita ambapo alipokelewa na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi wasaidizi wake hatutomvumilia mtu yeyote mwenye lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi yetu tutamshughulikia vilivyo bila kujali ni nani,” Amesema Sagini

Naibu Waziri Sagini amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kufanikiwa kudhibiti vurugu zilizoanzishwa na vijana dhidi ya Jeshi hilo kufuatia kuingilia kati kuokoa maisha ya raia aliyekuwa anashambuliwa na Wananchi kwa kutuhumiwa kuiba vifaa vya mziki msibani katika eneo la Bwanga Mkoani humo.

Pia ametoa rai kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kudhuru maisha ya wenzao kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na kuwataka kuimarisha shughuli za polisi jamii kwa lengo la kuimarisha usalama, kudhibiti uhalifu na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.

Aidha amemtaka Kamanda wa Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kufika kituoni hapo huku akimuhakikishia kuwa hali ya usalama mkoani humo ni shwari na wale wote wenye kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani watashughulikiwa.

F6eZt4eW4AAPORS.jpg
F6eZ1IwW4AAjVW4.jpg
 
Anaevuruga amani ya nchi ni huyu anaehamasisha ufisadi kwenye Taifa letu
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb), ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia sheria na taratibu zilizopo kudhibiti mtu yeyote mwenye viashiria au lengo la kuvuruga amani hapa nchini.
AMezungumzia chochote kuhusu ufisadi? Kule West Africa siku hizi ufisadi ndio unahatarisha amani ya nchi zao
 
Anaevuruga amani ya nchi ni huyu anaehamasisha ufisadi kwenye Taifa letu
View attachment 2756990
Tunaisingizia sana,Amani na ni neno limekua kichaka cha wahovu kujifichia huku wakifanya maovu,

Amani ni tunda la haki, hakuna mwananchi hapendi utulivu na Amani ,ila ni watawala kwa kutosikiliza wananchi wake ,kutotenda haki ,usawa, husababisha wananchi kuchoka au kuichoka mamlaka na kuamua liwalo na liwe,

Hii swala la nyanyasa watu, kamata watu , matendo mengine ya hivi sio kwamba ni zuri, bali linafanya wananchi kujaa hasira ndani ya vifua vyao , na hii sio afya kwa nchi, serikali na mamlaka zingatia hili.

Binadam akichafukwa anakua hatari sana, haogopi chochote,

Tujenge mfumo wa kueshimiana , kusikilizana , taifa letu wote
 
Back
Top Bottom