Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Leo hii nimesoma habari kwamba Tanzania na Msumbiji tumetia sahhi makubaliano ya ulinzi na usalama. Kwanza sikuamini kama ni Msumbiji kweli, au nchi nyingine. Yaani Msumbji, ile ninayoijua mimi, ambayo maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walikufa huko katika kuisaidia kupambana na majeshi ya uasi ya wakati huo Renamo?
Nimejiuliza, ikiwa leo hii tunatia sahihi huu mkataba, basi huko nyuma Watanzania tulifia Msumbiji chini ya kivuli gani?
Kwa wale msiojua historia, Tanzania tulipoingia vita na Uganda ya chini ya Idd Amin, Raisi Samora wa Msumbiji alileta vikosi vyake Tanzania ili viende kupigana na Idd Amin bila hata kushauriana na Nyerere! Nyerere alimkatalia Samora kupeleka askari wake Uganda, akidai ingesababisha vita kupanuka zaidi ya Uganda na Tanzania - japo baadae majeshi ya Libya yalikuja kumsaidia Idd Amin. Ikabidi askari wa Msumbiji wabaki hap Dar kulinda doria usiku. Nadhani mtakumbuka walifundishwa neno moja tu la kiswahili, "kitambulisho?"
Sasa toka ule uhusiano uliokuwapo, nini kimetokea kati yetu na Msumbiji hadi tufikie mahali pa kutiliana sahihi kusaidana ulinzi? Na pia nikakumbuka kwamba hapa juzi Msumbiji walipopata tatizo la ugaidi tena walikimbilia Rwanda kuomba msaaada sio ndugu zao wa Tanzania. Nikajiuliza kwa nini?
Je inawezekana uhusiano uliharika wakati wa serikali ya awamu iliyopita chini ya John Pombe Magufuli? Hilo ni jambo nazidi kujiuliza. Kwangu mimi kutiliana sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji ni sawa na mtu na kaka yake kutiliana sahihi makubaliano ya kusaidiana wakati wa shida! Kweli Raisi Samia hilo ni jambo mojawapo muhimu ya yaliyokupeleka Msumbiji?
Na kama kulikuwa na tatizo, basi nitasema wazi haikuwa busara kwenu Raisi Samia na Raisi Nyusi wa Msumbiji kulitangaza hili hadharani. Lingejadiliwa kimya kimya kati ya dada na kaka.
Reference: Tanzania, Msumbiji zatiliana saini ulinzi na usalama