Tanzania, Msumbiji zakubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya Ulinzi na Usalama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax akizungumza baada ya kufunga Mkutano wa ulinzi na Usalama baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, amesema:

Tulikuwa na kikao cha tano cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano ya Sekta ya Ulinzi na Usalama ambapo tumekubaliana mengi na tumezungumza mengi.
2a20eca3-e562-4b11-9f73-e01af6ff90c2.jpeg

1e3b1859-c815-4e07-a5e4-9911fe5d703b.jpeg
Kikubwa ni kuendelezea ushirikia na masuala ya ulinzi na usalama, matishio yake hayatambui mipaka, yapo ambayo tunayashughulikia ndani ya Nchi.

Ugaidi ni moja ya matishio ambayo hayatambui mipaka, huu ni mwendelezo, Msumbiji na Tanzania tumekuwa ndugu na marafiki tangu wakati wa kupigania uhuru.

Tanzania tunashirikiana nao kama Nchi pia tunashirikiana nao kupitia Jumuia ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika, tumekubaliana mambo mbalimbali ya kutekeleza katika ulinzi na usalama na tutaendelea kushirikiana kila mwaka.

Mkutano wa Sita utafanyika Msumbiji baada ya mwaka mmoja lakini hapo katikati tutakuwa tunatekeleza yale ambayo tumekubaliana.
d34ebd45-c554-44d8-9523-de5a731f84e0.jpeg

6310bf03-a001-4367-b070-b457ff8a6388.jpeg
Kuhusu matukio ya ugaidi
Hali ya usalama ni nzuri lakini kama inavyojulikana inaweza kubadilika muda wowote, hakuna matishio wala matukio lakini tunaendelea kusimama imara, hatujabweteka.

Kila Mwananchi analo jukumu la kulinda Taifa lake, kwa kufanya matendo ya usahihi yanayodumisha ulinzi na usalama lakini anapoona viashiria vyovyote anatakiwa kutoa taarifa.
2cd659d7-8603-4020-8446-42fd6e87ceff.jpeg
 
Back
Top Bottom