mapesa yamejaa
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 1,412
- 3,403
Kwamba panya road tumewashindwa hadi kuingia mkataba na msumbiji ili watusaidie?kwa nini kipindi cha magu tulikisambaratisha hiki kikundi cha panya road?
Usilete za kuleta mkuu.Kama huelewi haya mambo kaa kimya. Kwani nani amekuambia hatutaki mama afanye kazi? Tatizo wengi humu JF tunaangalia mambo juu juu sana
Kwa hiyo tuliweka kambi na sasa ndio tuna saini mkataba? Tuliweka kambi chini ya mkataba gani sasa, na huu ni kwa ajili ya nini, kuweka kambi ya pili?Una tatizo kubwa la uelewa.
Nimekueleza sababu ya kutiliana sana kwenye ulinzi na usalama ni kutokana na kinachoendelea mpakani kupambana na Wanamgambo wa kiislamu(IS). Na Tanzania ilianza kuchukua hatua ikiwemo kuweka kambi kubwa huko mpakani na hata hili suala lilifika bungeni na kujadiliwa.
Huenda hata hukusoma walichoongea hawa maraisi
Pitia hapa
Mmmh, udhaifu wa Msumbiji sidhani, japo inawezekana pia, lakini naomba nizungumzie upande wa TZ.Sio Askari ni Islamic State (IS). Bado pia wanaendelea kuingia mara moja moja japo Tz inapambana nao sana.
Kuna kambi kubwa huko imewekwa kwa ajili ya hao IS, Ila msumbiji wana jeshi dhaifu sana
Kaka lile kabila sio la kuongoza nchi, ndo maana hayati baba wa taifa aliyapinga baadhi ya makabila, yeye aliona mbali mno. Hatujawahi kuongozwa na mtu mshamba wa madalaka sampuli ya jiwe. Sifa, kutukuzwa, kuabudiwa n.kJiwe hakufaa kuwa Rais kabisa, sipati picha mpk leo angekuwepo, tungevunja mahusiano na nchi nyingi sababu ya kiburi chake Cha kishamba
Aiseeee, kuna mambo huyatambui. Kuna kipindi TZ tulishutumiwa kuuza silaha mipakani, hasa burundi. Sijui una muda gani JF, kipindi JK anaruhusu JWTZ kwenda Congo kupambana na M23, Kagame alikuja juu na kusema Tz inafadhili vikundi vya Interahamwe/FDLR ambavyo ni maadui wa Rwanda.Huenda una tatizo la uelewa. Hakujawahi kuwa na tatizo Kati ya Tz na msumbiji. Kutiliana saini kwenye masuala ya ulinzi hufanyika Mara kwa Mara kulingana na hali ya kiusalama mpakani ilivyo.
Tanzania hapa tulisaini mkataba wa ulinzi na usalama na Burundi, unataka kusema pia tumewahi kuwa na tatizo na Burundi?
View attachment 2364605
Achana nao hawana akili hao, watakusumbua bure, mambo ya kiusalama wanachukulia simple.Kwa hiyo tuliweka kambi na sasa ndio tuna saini mkataba? Tuliweka kambi chini ya mkataba gani sasa, na huu ni kwa ajili ya nini, kuweka kambi ya pili?
Nyusi alienda Chato na tukaambiwa kuna makubaliano ya ulinzi na Usalama yaliweza kusainiwa na Hayati Magufuli, labda kuna Amendments zimefanyika Kati ya Tanzania na Msumbiji katika huo MkatabaNyusi alikuwa anaenda kupumzika Chato
hatari Sana mkuuKaka lile kabila sio la kuongoza nchi, ndo maana hayati baba wa taifa aliyapinga baadhi ya makabila, yeye aliona mbali mno. Hatujawahi kuongozwa na mtu mshamba wa madalaka sampuli ya jiwe. Sifa, kutukuzwa, kuabudiwa n.k
Umesema kweli tupu! UshambaJiwe hakufaa kuwa Rais kabisa, sipati picha mpk leo angekuwepo, tungevunja mahusiano na nchi nyingi sababu ya kiburi chake Cha kishamba
nakubali kabisa haina ubishiAah Mkuu kushughulika na hao hakuhitaji kutiliana sahihi mkataba wa amani na usalama!
haina ubishi kabisaInasemekana majority ya trouble makers/waasi kule msumbiji, ni panya road wetu.
"Inasemekana"
Yule mtu mlikuwa mnamuita Rais alikuwa na matatizo makubwa kichwani na aliharibu kila mahala na kugombana na kila jirani.Leo hii nimesoma habari kwamba Tanzania na Msumbiji tumetia sahhi makubaliano ya ulinzi na usalama. Kwanza sikuamini kama ni Msumbiji kweli, au nchi nyingine. Yaani Msumbji, ile ninayoijua mimi, ambayo maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walikufa huko katika kuisaidia kupambana na majeshi ya uasi ya wakati huo Renamo?
Nimejiuliza, ikiwa leo hii tunatia sahihi huu mkataba, basi huko nyuma Watanzania tulifia Msumbiji chini ya kivuli gani?
Kwa wale msiojua historia, Tanzania tulipoingia vita na Uganda ya chini ya Idd Amin, Raisi Samora wa Msumbiji alileta vikosi vyake Tanzania ili viende kupigana na Idd Amin bila hata kushauriana na Nyerere! Nyerere alimkatalia Samora kupeleka askari wake Uganda, akidai ingesababisha vita kupanuka zaidi ya Uganda na Tanzania - japo baadae majeshi ya Libya yalikuja kumsaidia Idd Amin. Ikabidi askari wa Msumbiji wabaki hap Dar kulinda doria usiku. Nadhani mtakumbuka walifundishwa neno moja tu la kiswahili, "kitambulisho?"
Sasa toka ule uhusiano uliokuwapo, nini kimetokea kati yetu na Msumbiji hadi tufikie mahali pa kutiliana sahihi kusaidana ulinzi? Na pia nikakumbuka kwamba hapa juzi Msumbiji walipopata tatizo la ugaidi tena walikimbilia Rwanda kuomba msaaada sio ndugu zao wa Tanzania. Nikajiuliza kwa nini?
Je inawezekana uhusiano uliharika wakati wa serikali ya awamu iliyopita chini ya John Pombe Magufuli? Hilo ni jambo nazidi kujiuliza. Kwangu mimi kutiliana sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji ni sawa na mtu na kaka yake kutiliana sahihi makubaliano ya kusaidiana wakati wa shida! Kweli Raisi Samia hilo ni jambo mojawapo muhimu ya yaliyokupeleka Msumbiji?
Na kama kulikuwa na tatizo, basi nitasema wazi haikuwa busara kwenu Raisi Samia na Raisi Nyusi wa Msumbiji kulitangaza hili hadharani. Lingejadiliwa kimya kimya kati ya dada na kaka.
Reference: Tanzania, Msumbiji zatiliana saini ulinzi na usalama
Hakuna kosa,mambo yote ya amani huwa yanasemwa wazi hivi hivi..IKiwa ndivyo basi Raisi Samia na Raisi Nyusi watakuwa wamefanya jambo bila busara. Walipaswa kujadili hili jambo kimya kimya bila kutanganza hadharani kutiliana sahihi mkatana wa ulinzi na usalama. Wao ni dada na kaka kwa jinsi tulivyo Msumbiji na Tanzania