Ikiwa leo hii Rais Samia anatia sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji basi kuna kitu kiliharibika hapo nyuma

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Leo hii nimesoma habari kwamba Tanzania na Msumbiji tumetia sahhi makubaliano ya ulinzi na usalama. Kwanza sikuamini kama ni Msumbiji kweli, au nchi nyingine. Yaani Msumbji, ile ninayoijua mimi, ambayo maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walikufa huko katika kuisaidia kupambana na majeshi ya uasi ya wakati huo Renamo?

Nimejiuliza, ikiwa leo hii tunatia sahihi huu mkataba, basi huko nyuma Watanzania tulifia Msumbiji chini ya kivuli gani?

Kwa wale msiojua historia, Tanzania tulipoingia vita na Uganda ya chini ya Idd Amin, Raisi Samora wa Msumbiji alileta vikosi vyake Tanzania ili viende kupigana na Idd Amin bila hata kushauriana na Nyerere! Nyerere alimkatalia Samora kupeleka askari wake Uganda, akidai ingesababisha vita kupanuka zaidi ya Uganda na Tanzania - japo baadae majeshi ya Libya yalikuja kumsaidia Idd Amin. Ikabidi askari wa Msumbiji wabaki hap Dar kulinda doria usiku. Nadhani mtakumbuka walifundishwa neno moja tu la kiswahili, "kitambulisho?"

Sasa toka ule uhusiano uliokuwapo, nini kimetokea kati yetu na Msumbiji hadi tufikie mahali pa kutiliana sahihi kusaidana ulinzi? Na pia nikakumbuka kwamba hapa juzi Msumbiji walipopata tatizo la ugaidi tena walikimbilia Rwanda kuomba msaaada sio ndugu zao wa Tanzania. Nikajiuliza kwa nini?

Je inawezekana uhusiano uliharika wakati wa serikali ya awamu iliyopita chini ya John Pombe Magufuli? Hilo ni jambo nazidi kujiuliza. Kwangu mimi kutiliana sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji ni sawa na mtu na kaka yake kutiliana sahihi makubaliano ya kusaidiana wakati wa shida! Kweli Raisi Samia hilo ni jambo mojawapo muhimu ya yaliyokupeleka Msumbiji?

Na kama kulikuwa na tatizo, basi nitasema wazi haikuwa busara kwenu Raisi Samia na Raisi Nyusi wa Msumbiji kulitangaza hili hadharani. Lingejadiliwa kimya kimya kati ya dada na kaka.

Reference: Tanzania, Msumbiji zatiliana saini ulinzi na usalama
 
Nadhani issue haipo kwenye kushughulika nao, issue ipo kwenye kutuchafulia CV.

Ni ngumu sana kukuamini na kushirikiana na wewe ikiwa wanao kila siku wanakuja kufanya fujo nyumbani kwangu.
Mkuu, panya road kwenda kufanya fujo Msumbiji hakuwezi kuharibu uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji. Tanzania haiwatumi panya road kwenda Msumbiji
 
Hakuna uhusiano wowote umewahi kuharibika, huo ni mkataba wa ushirikiano zaidi kutokana na yaanayoendelea kaskazini mwa msumbiji na kusini kusini mwa Tanzania.

Mabeyo aliwahi kwenda, sirro aliwahi kwenda. Ila waasi bado Wana nguvu.

Uhusianonwetu uliwahi kuvunjika na Malawi, lakinj uliona kuna mkataba wa amani?
 
Miaka michache iliyopita nilisikia askari kutoka huko wakiingia mikoa ya kusini, kuvamia na kuua.

Ikasemwa humu jf ikapita.

Wiki iliyopita naongea na mjeshi mmoja akaniambia alikuwa mtwara,

Nikawaza kama mleta huu uzi alivyowaza.

Kutakuwa na kitu hakipo sawa.

Ngoja wajuzi waje
Sio Askari ni Islamic State (IS). Bado pia wanaendelea kuingia mara moja moja japo Tz inapambana nao sana.

Kuna kambi kubwa huko imewekwa kwa ajili ya hao IS, Ila msumbiji wana jeshi dhaifu sana
 
Ngoja tusubiri atujui Rais wetu aliongea kitu gani na serikali ya France wamiliki wa kampuni ya Total.
Lakini basi busara ingetumika wasingekuwa na haja ya kutangaza kutia sahihi makubaliano ya amani. Wangeongea kimya kimya. Kukiwa na tatizo kati yako na kaka yako, hamtoki nje kuwatangazia majirani kwamba sasa mmekubaliana kuendelea kuwa ndugu
 
Leo hii nimesoma habari kwamba Tanzania na Msumbiji tumetia sahhi makubaliano ya ulinzi na usalama. Kwanza sikuamini kama ni Msumbiji kweli, au nchi nyingine. Yaani Msumbji, ile ninayoijua mimi, ambayo maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walifa huko katika kuisaidia kupambana na majeshi ya uasi ya wakati huo Renamo?

Nimejiuliza, ikiwa leo hii tunatia sahihi huu mkataba, basi huko nyuma Watanzania tulifia Msumbiji chini ya kivuli gani?

Kwa wale msiojua historia, Tanzania tulipoingia vita na Uganda ya chini ya Idd Amin, Raisi Samora wa Msumbiji alileta vikosi vyake Tanzania ili viende kupigana na Idd Amin bila hata kushauriana na Nyerere! Nyerere alimkatalia Samora kupeleka askari wake Uganda, akidai ingesababisha vita kupanuka zaidi ya Uganda na Tanzania - japo baadae majeshi ya Libya yalikuja kumsaidia Idd Amin. Ikabidi askari wa Msumbiji wabaki hap Dar kulinda doria usiku. Nadhani mtakumbuka walifundishwa neno moja tu la kiswahili, "kitambulisho?"

Sasa toka ule uhusiano uliokuwapo, nini kimetokea kati yetu na Msumbiji hadi tufikie mahali pa kutiliana sahihi kusaidana ulinzi? Na pia nikakumbuka kwamba hapa juzi Msumbiji walipopata tatizo la ugaidi tena walikimbilia Rwanda kuomba msaaada sio ndugu zao wa Tanzania. Nikajiuliza kwa nini?

Je inawezekana uhusiano uliharika wakati wa serikali ya awamu iliyopita chini ya John Pombe Magufuli? Hilo ni jambo nazidi kujiuliza. Kwangu mimi kutiliana sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji ni sawa na mtu na kaka yake kutiliana sahihi makubaliano ya kusaidiana wakati wa shida! Kweli Raisi Samia hilo ni jambo mojawapo muhimu ya yaliyokupeleka Msumbiji?

Reference: Tanzania, Msumbiji zatiliana saini ulinzi na usalama
Jiwe hakufaa kuwa Rais kabisa, sipati picha mpk leo angekuwepo, tungevunja mahusiano na nchi nyingi sababu ya kiburi chake Cha kishamba
 
Lakini basi busara ingetumika wasingekuwa na haja ya kutangaza kutia sahihi makubaliano ya amani. Wangeongea kimya kimya. Kukiwa na tatizo kati yako na kaka yako, hamtoki nje kuwatangazia majirani kwamba sasa mmekubaliana kuendelea kuwa ndugu
Huenda una tatizo la uelewa. Hakujawahi kuwa na tatizo Kati ya Tz na msumbiji. Kutiliana saini kwenye masuala ya ulinzi hufanyika Mara kwa Mara kulingana na hali ya kiusalama mpakani ilivyo.
Tanzania hapa tulisaini mkataba wa ulinzi na usalama na Burundi, unataka kusema pia tumewahi kuwa na tatizo na Burundi?
Screenshot_20220922-135650_1.jpg
 
Miaka michache iliyopita nilisikia askari kutoka huko wakiingia mikoa ya kusini, kuvamia na kuua.

Wiki iliyopita naongea na mjeshi mmoja akaniambia alikuwa mtwara,

Nikawaza kama mleta huu uzi alivyowaza.

Kutakuwa na kitu hakipo sawa.
IKiwa ndivyo basi Raisi Samia na Raisi Nyusi watakuwa wamefanya jambo bila busara. Walipaswa kujadili hili jambo kimya kimya bila kutanganza hadharani kutiliana sahihi mkatana wa ulinzi na usalama. Wao ni dada na kaka kwa jinsi tulivyo Msumbiji na Tanzania
 
Huenda una tatizo la uelewa. Hakujawahi kuwa na tatizo Kati ya Tz na msumbiji. Kutiliana saini kwenye masuala ya ulinzi hufanyika Mara kwa Mara kulingana na hali ya kiusalama mpakani ilivyo.
Tanzania hapa tulisaini mkataba wa ulinzi na usalama na Burundi, unataka kusema pia tumewahi kuwa na tatizo na Burundi?
Wewe ndio huelewi. Mikataba ya ulinzi na usalama sio jambo linalotokea tu la kisiasa. Tanzania na Msumbiji sio sawa na Tanzania na Burundi. Hatujawahi kufia Burundi kuwasaidia Warundi, na ili leo hii tuweze kuwasaidia huko mbele, kwa sababu hatuna uhakika na uhusiano wetu na Burundi, lazima tutiliane sahihi mkataba wa ulinzi na usalama. Pia ni kwa ajili ya kuepusha uwezekano wa kupigana tukikorofishana, au uwezekano wa Tanzania kusaidia waasi wa Burundi wakitokea na vice versa. Umeelewa sasa nature ya mikataba ya ulinzi na usalama?

Kwa nini Israel inatiliana mkataba wa ulinzi na usalama na Egypt na sio na Tanzania?
 
Leo hii nimesoma habari kwamba Tanzania na Msumbiji tumetia sahhi makubaliano ya ulinzi na usalama. Kwanza sikuamini kama ni Msumbiji kweli, au nchi nyingine. Yaani Msumbji, ile ninayoijua mimi, ambayo maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walifa huko katika kuisaidia kupambana na majeshi ya uasi ya wakati huo Renamo?

Nimejiuliza, ikiwa leo hii tunatia sahihi huu mkataba, basi huko nyuma Watanzania tulifia Msumbiji chini ya kivuli gani?

Kwa wale msiojua historia, Tanzania tulipoingia vita na Uganda ya chini ya Idd Amin, Raisi Samora wa Msumbiji alileta vikosi vyake Tanzania ili viende kupigana na Idd Amin bila hata kushauriana na Nyerere! Nyerere alimkatalia Samora kupeleka askari wake Uganda, akidai ingesababisha vita kupanuka zaidi ya Uganda na Tanzania - japo baadae majeshi ya Libya yalikuja kumsaidia Idd Amin. Ikabidi askari wa Msumbiji wabaki hap Dar kulinda doria usiku. Nadhani mtakumbuka walifundishwa neno moja tu la kiswahili, "kitambulisho?"

Sasa toka ule uhusiano uliokuwapo, nini kimetokea kati yetu na Msumbiji hadi tufikie mahali pa kutiliana sahihi kusaidana ulinzi? Na pia nikakumbuka kwamba hapa juzi Msumbiji walipopata tatizo la ugaidi tena walikimbilia Rwanda kuomba msaaada sio ndugu zao wa Tanzania. Nikajiuliza kwa nini?

Je inawezekana uhusiano uliharika wakati wa serikali ya awamu iliyopita chini ya John Pombe Magufuli? Hilo ni jambo nazidi kujiuliza. Kwangu mimi kutiliana sahihi makubaliano ya ulinzi na usalama na Msumbiji ni sawa na mtu na kaka yake kutiliana sahihi makubaliano ya kusaidiana wakati wa shida! Kweli Raisi Samia hilo ni jambo mojawapo muhimu ya yaliyokupeleka Msumbiji?

Na kama kulikuwa na tatizo, basi nitasema wazi haikuwa busara kwenu Raisi Samia na Raisi Nyusi wa Msumbiji kulitangaza hili hadharani. Lingejadiliwa kimya kimya kati ya dada na kaka.

Reference: Tanzania, Msumbiji zatiliana saini ulinzi na usalama
Kwani kimeharibika kitu gani?
Hali ya usalama wakati wa Mwalimu 1978/79 ni tofauti kabisa na sasa.
Leo ni 2022, na mama yupo madarakani.
mwacheni mama afanyekazi.
 
Kama huelewi haya mambo kaa kimya. Kwani nani amekuambia hatutaki mama afanye kazi? Tatizo wengi humu JF tunaangalia mambo juu juu sana
 
Wewe ndio huelewi. Mikataba ya ulinzi na usalama sio jambo linalotokea tu la kisiasa. Tanzania na Msumbiji sio sawa na Tanzania na Burundi. Hatujawahi kufia Burundi kuwasaidia Warundi, na ili leo hii tuweze kuwasaidia. Na kwa sababu hatuna uhakika na uhusiano wetu na Burundi huko mbele lazima tutiliane sahihi mkataba wa ulizi na usalama, kuepusha uwezekano wa kupigana tukikorofishana, au uwezekano wa Tanzania kusaidia waasi wa Burundi wakitokea na vice versa. Umeelewa sasa nature ya mikataba ya ulinzi na usalama?

Kwa nini Israel inatiliana mkataba wa ulinzi na usalama na Egypt na sio na Tanzania?
Una tatizo kubwa la uelewa.

Nimekueleza sababu ya kutiliana sana kwenye ulinzi na usalama ni kutokana na kinachoendelea mpakani kupambana na Wanamgambo wa kiislamu(IS). Na Tanzania ilianza kuchukua hatua ikiwemo kuweka kambi kubwa huko mpakani na hata hili suala lilifika bungeni na kujadiliwa.

Huenda hata hukusoma walichoongea hawa maraisi
Pitia hapa
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom