Swali kwa Wakuu wa Ulinzi na Usalama: Ni halali kwa Raia wanaopinga uhaini dhidi ya Jamhuri kupewa tuhuma za uhaini dhidi ya Rais wa Jamhuri?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1691899128235.png

Ndg. Said Hussein Nassoro, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Leo tunalo swali makini kwa wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama: Ni sawa kwa Raia wanaopinga uhaini uliofanywa wa Rais dhidi ya Jamhuri kunyamazishwa kwa kufunguliwa mashtaka ya uhaini dhidi ya Rais anayetuhumiwa kwa uhaini?

Waheshimiwa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, kuna kituko kinatokea nchini Tanzania, na kwa sababu ya kituko hiki, hali sio shwari tena.

Kituko chenyewe ni kwamba Raia waliomtuhumu Rais Samia kutenda kosa la uhaini wa kiuchumi dhidi ya Jamhuri sasa wanatuhumiwa kwa kosa la uhaini dhidi ya Rais Samia. Kituko hiki ni kama ifuatavyo:

1. Tarehe 25 Oktoba 2022 Rais Samia alisaini mkataba wa IGA wenye ibara inayotaja masharti ya utulivu wa kisheria yaani "stabilisation clause," katika ibara ya 30, inayomomonyoa ukuu wa mahakama, ukuu wa bunge na ukuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mpaka siku ya mwisho pale shughuli za bandari zitakapokoma. Mkataba huu uliidhinishwa kibabe na Bunge la Tanzania tarehe 10 Juni 2023. Ibara ya 30 inatamka yafuatayo:

"(1) Nchi Wanachama zinakubali kwamba mazingira ya kisheria na ya kimkatabayanayohusiana na Miradi yatadhibitiwa kwa namna ambayo ni sawa na yakuridhisha kwa Nchi Wanachama na Kampuni ya Mradi. Maelezo ya uimarishaji huo yatakubaliwa kati ya DPW au Kampuni husika ya Mradi na TPA na piakuonyeshwa katika HGA husika. Utulivu huo utatumia tarehe ya kutia saini IGA kama tarehe ya marejeleo ya uimarishaji, ili kushughulikia mabadiliko yoyote katikaSheria au mabadiliko ya kodi yanayoathiri Miradi husika.
(2) Tanzania itachukua hatua zote zinazohitajika au zinazofaa kufanya, kutoa au kutekeleza ndani ya Eneo lake sheria zote wezeshi na hatua nyingine za kisheria zinazohitajika ili kuwezesha na kutekeleza ahadi zilizoainishwa katika Mikataba ya Mradi na HGAs.
3. Ubaya wa "legal stabilisation lauses" ni kwamba, vifungu hivi vinazifunga mikono na miguu serikali na bunge, na kuikweza kampuni ya uwekezaji juu yake. Ukuu wa serikali na ukuu wa Bunge unaegwa kwa ajili ya kuanzisha ukuu wa kampuni ya uwekezaji wa kigeni.vifungu hivi vinazifunga mikono na miguu serikali na bunge, na kuikweza kampuni ya uwekezaji juu yake. Ukuu wa serikali na ukuu wa Bunge unamegwa kwa ajili ya kuanzisha ukuu wa kampuni ya uwekezaji wa kigeni. Paul Comeaux and Stephan Kinsella (1994:24), wanasema yafuatayo kuhusu uhalisia wa kifungu cha aina hii:

"A stabilization clause states that the law in force in the state at a given date-typically, the time the concession takes effect-is the law that will apply to supplement the terms of the contract, regardless of future legislation, decrees, or regulations issued by the government. Its purpose is to 'preclude the application to an agreement of any subsequent legislative (statutory) or administrative (regulatory) act issued by the government ... that modifies the legal situation of the investor.' In other words, by agreeing to a stabilization clause, a state alienates its right to unilaterally change the regime and rights relied upon by, and promised to, the investor. [Therefore, such clauses do not preclude a state from enacting new legislation, but rather prevent it from enforcing new regulations against a specific contractual party.]"

4. Wananchi wajuzi wa masuala haya kuhusu uendeshaji wa nchi, wakiwemo Profesa Anna Tibaijuka, Wakili Mwabukusi na Balozi Wilbroad Slaa, wanasema kuwa Rais Samia ametenda kosa la uhaini wa kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wawekezaji wa kigeni kutoka Dubai, ambao ni maadui wa [ustawi wa kiuchumi nchini] Tanzania, kuanzisha "vita ya kiuchumi," itakayopiganwa na wawekezaji hao kwa njia ya kukalia kimabavu ardhi ya Tanzania inayozunguka bandari 88 za Tanzania Bara.

5. Wanazuoni hawa wanasema kwamba, kosa lililofanywa na Rais Samia ni sawa na kosa lililofanywa na Marais wa Azerbaijan, Georgia na Uturuki mwaka 2020, kupitia mkataba wa IGA pamoja na viambatanisho vyake vya Mikataba mitatu ya HGA, iliyosaniwa mwaka 2000.

6. Wanafafanua kwamba, Rais Samia pamoja na Profesa Makame Mbarawa wametenda kosa hilo dhidi ya kifungu cha 39(1)(b) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya 2022, ambapo Rais Samia alitenda kosa hilo tarehe 3 Oktoba 2022 aliposaini hati ya kumpa madaraka Waziri Mbarawa, na Waziri Mbarawa akatenda kosa hilo aliposaini mkataba wa IGA tarehe 25 Oktoba 2022. Kifungu cha jinai walichokivunja kinasomeka kama ifuatavyo:

"Any person who, being under allegiance to the United Republic, and in the United Republic, levies [economic] war against the United Republic, shall be guilty of treason and shall be liable on conviction to suffer death."

7. Kutokana na tafsiri hii ya uhaini, ni wazi kwamba, mjadala wa mkataba wa IGA unafungamana na uhaini wa kiuchumi uliofanywa na Rais Samia, na mjadala wa uhaini wa kiuchumi uliofanywa na Rais Samia pamoja na serikali anayoiongoza unafungamana na uharamu wa kisheria wa Rais Samia na serikali anayoiongoza. Hivyo, mjadala kuhusu swali lifuatalo hauepukiki; "Ni mbinu gani zinaweza, na zinapaswa, kutumika kuiondoa serikali haramu madarakani?"

8. Rais Samia aliposikia tuhuma hiyo dhidi yake, huku akiwa anafahamu fika kwamba, ibara ya 46 (1) ya Katiba ya Tanzania inasema kwamba, yeye kama Rais aliye madarakani hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote [likwemo kosa la uhaini] alilolitenda akiwa madarakani, akaagiza kwamba sasa wakosoaji wake ndio wabebeshwe kosa la uhaini dhidi ya Rais na serikali yake.

9. Kwa sasa vyombo vya dola vinapanga kuwafungulia mashtaka wakosoaji wa Rais Samia mashtaka ya kosa la uhai chini ya kifungu cha 39(2) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya 2022. Kifungu hiki kinasomeka kama ifuatavyo:

"Any person who, being under allegiance to the United Republic, in the United Republic or elsewhere, forms an intention to effect or to cause to be effected, or forms an intention to instigate, persuade, counsel or advise any person or group of persons to effect or to cause to be effected, any of the following acts, deeds or purposes, that is to say:
(a) the death, maiming or wounding, or the imprisonment or restraint, of the President;
(b) the deposing by unlawful means of the President from his position as President or from the style, honour and name of Head of State and Commander-in-Chief of the Defence Forces of the United Republic;
(c) the overthrow by unlawful means, of the Government of the United Republic; or
(d) the intimidation of the Executive, the Legislature or the Judiciary of the United Republic,
and manifests such intention by publishing any writing or printing or by any overt act or deed whatsoever shall be guilty of treason and shall be liable on conviction to be sentenced to death."

10. Hitimisho kutokana na sakata hili ni kwamba, sasa Tanzania imefika mahali ambako kanuni ya maisha ni kwamba:

"Mwenye nguvu ya kukanyaga wenzake ndiye mwenye haki ya kusikilizwa, kuheshimiwa na kupewa utii, hata kama ni mhaini dhidi ya Jamhuri."

11. Ama kweli, ni kituko cha milenia pale Raia wanaopinga uhaini wa Rais dhidi ya Jamhuri wanapofunguliwa mashtaka ya uhaini dhidi ya Rais mhaini.

12. Hapa chini tumeambatanisha seti kamili ya Mkataba wa IGA na Viambatanisho vyake vya mikataba ya HGA kuhusiana na mradi wa Bomba la Mafuta la BTC, linalokatiza nchi tatu za Azerbaijan, Geogia na Uturuki. Huu ni mkataba wa kwanza wa IGA wenye kuammbatana na kiambatanisho /viambatanisho vya HGA, kama ilivyo kwa mkataba wa IGA kati ya Tanzania na Dubai. Tusome na kujifunza kutokana na historia ya mradi wa BTC.

13. Mikataba hii ya mradi wa BTC inazo "ibara za utulivu wa kisheria" yaani "legal stabilisation lauses," vinavyoifunga mikono na miguu ya serikali za Azerbaijan, Geogia na Uturuki kwa miaka 40 tangu mwaka 2020.

14. Mradi huu wa BTC unatengeneza "militarised corridor of corporate sovereignty" yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,700 na upana wa meta 200, kuania Bahari ya Kaspiani mpaka Bahari ya Mediteraniani. Kitu kama hiki kitatokea kwenye bandari zote 88 za Tanzania Bara, maana zitageuka kuwa "fiefdoms" zilizo chini ya himaya ya Waarabu wa Dubai kwa kipindi ambacho wanakijua Rais Samia na Mtawala wa Dubai pekee.

15. Marejeo:
  1. Paul Comeaux and Stephan Kinsella (1994), "Reducing Political Risk in Developing Countries: Bilateral Investment Treaties, Stabilization Clauses, Bilateral Investment Treaties, Stabilization Clauses, and Miga & Opic Investment Insurance And Miga & Opic Investment Insurance," NYLS Journal of International and Comparative Law: 15.1, Article 2:1-48.

Dawati Adhimu la Mama Amon (DAMA),
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga
16 Agosti 2023.
 

Attachments

  • COMPLETE IGA AND HGA FOR TURKEY, GEORGIA AND AZERBAIJAN.pdf
    6.9 MB · Views: 1
Back
Top Bottom