Rutunga M
JF-Expert Member
- Mar 16, 2009
- 1,769
- 1,382
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:
“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”.
“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”.
“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”.
“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”.
“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi?, tupate nini? Tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”.
Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”.
“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”.
“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”.