Hapa sasa naona kuna makundi mawili, moja likisema inawezekana ni JK hataki kuonana na Slaa.
Na jingine ni kuwa Slaa bado hataki kuonana na JK.
Na tukirudi nyuma kwenye matukio hayo, "tukachanganya na zetu" basi inawezekana tukapata mweleko flani.
Kuna wanaodai kuwa JK angetaka kuonana na Dr Slaa, basi angeweza muda wowote hata kumwita kwasababu yeye ni Rais, jambo moja wanalosahau ni kwamba JK hawezi kumwita Slaa bila sababu hata kama yeye ni rais.
Na tunachotizama hapa si wao kuitana, rather ni kwanini hawasalimiani hata pale inapotokea nafasi ya kuweza kufanya hivyo?
Kwanza kuna issue ya bungeni kuhusu kumtambua Rais mara baada a uchaguzi mkuu, pia kuna kauli kadhaa wa kadha kuwa uchaguzi haukuwa huru na uchakachuaji ulikuwepo, hilo pekee linapelekea confusions, na speculations kama hizi.
Walikwenda ikulu kuonana na JK, Slaa hakwenda.Mtu yeyote anaweza kuwa na tafsiri yoyote isiyo rasmi kwasababu ofcourse hata Zitto hakwenda na pia kuna watakaodai haikuwa na ulazima yeye Slaa kwenda, na kwamba hilo hali constitute yeye kutokutaka kuonana na JK etc.
Sikubaliani na wale wanaodai kuwa JK ndiyo hataki kuonana na Slaa kwasababu ushahidi wa kimazingira hauonyeshi hivyo.
Mara zote ambazo hawakukutana, ni Slaa ndiye aliyemiss, kwa mfano ikulu na kwenye mazishi na bungeni.
Haya yote si kwamba nina uhakika kuwa mkwepaji hapa ni Slaa, maybe not, or maybe yes...
Its a matter of disscussion.
BTW mimi sina chama na hivyo msishangazwe na neutrality yangu na maswali ambayo simply ni yenye kuleta changamoto zaidi towards finding any truth, if any at all!lol