Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Mimi nilihudhuria maziko na nikategesha camera yangu ili nipige picha moja tuu, one and only JK akisalimiana na Dr. Slaa!.
Pasco huyo!!!
kazi maalumu!
 
PASCO
nilipolazimika kupanda juu ya kaburi ili kuipata hiyo picha
nilikuona ulivyokosa adabu, nilkuona ulivyokua unaharibu kaburi la mpendwa wetu....
 
Ni kitu gani kinawafanya watu wafikirie kuwa Kikwete anataka kukutana na Dr. Slaa? Amewahi kusema kuwa anataka kukutana naye lakini amekuwa akimkwepa? Hivi kweli Kikwete akitaka kukutana na mtu yeyote Tanzania hawezi? Hakuna ushahidi wowote kuwa Kikwete anataka kukutana na Dr. Slaa kwa sababu yoyote ile. Dr. Slaa ameshamtambua kuwa ni Rais, na alishawahi kusema hana tatizo la kukutana na Kikwete. Naamini kama Kikwete anataka kuonana na Slaa ampigie simu na kumwambia wakutane mahali ambapo patakuwa muafaka kwa wote wawili kama kweli anataka kukutana naye.

Nashangaa watu wameweka mzigo kwa Dr. Slaa! "ooh Slaa amkimbia/amkwepa/ampiga chenga JK" hivi mkiambiwa kuwa Kikwete amesema hataki kukutana na Dr. Slaa kwa sababu amemletea matatizo na nusura amnyang'anye urais. Halafu mkaambiwa kuwa ndio sababu ya Slaa kushindwa kwenda Ikulu, na ndio sababu ya Slaa kushindwa kukaa karibu na Kikwete, mtakataa? Mnaushahidi gani kuwa Kikwete anataka kukutana na Slaa maana kama ana hilo hitaji sana atume hata polisi wamkamate kwa nguvu mbona waliweza kumsoma Mbowe kwa ndege hadi Arusha?

Hii ni habari isiyo habari.

i can't concur more, mate.....
 
NAnI hakumsalimia nani?'

KWA NINI ISIWE JK HAKUMSALIMIA SLAA NA IWE SLAA HAKUMSALIMIA JK?
 
Nafikiri kuna tatizo hapo. Lakin Ukweli unasiama tena kwa sheria zenu wenyewe kuwa Kikwete ni Rais wa Tz mpaka 2015 na ataendelea hivyo kisheria . Kumpinga au hata kummicha kunana nae ni upungufu wa maadili na uvunjifu wa katiba ya nchi yenu siku zote kisheria rais anakuwa mmoja .
 
"Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa ni upande mwingine na rais alikaa upande mwingine, isingekuwa busara mimi kutoka huko upande wangu kukatiza pale mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!."

Haiingii akilini Katibu Mkuu asiwekwe mbele. Hapo Slaa kama kawa kawahadaa waandishi.
 
Mbona Dr. Slaa haonyeshi ukomavu wa kisiasa. Nanusa harusi mbaya ndani ya CHADEMA! Huenda viongozi wengine CDM walikubaliana kumtambua JK lakini Dr. Slaa hakukubali na hataki kukubaliana na wengi ndio maana hataki kukutana na JK ili kuonyesha kwamba hamtambui. Dr. Slaa wenzio wamemtambua na wameishaenda Ikulu (mwingine mara mbili) basi nawe kubaliana na wenzio umtambue tu JK.

Hii itaonyesha uungwana badala ya kumkwepa mtu mzima mwenzio, hii inaonyesha kukosa ukomavu kisiasa na hali ya kuwa na vinyongo visivyoisha! Watu wanasema katika siasa hakuna uadui wa kudumu.

fikiria zaidi ya hapo.kama walimuweza nyerere ni dr.lazima ajihadhari na magamba maana wana maabara
 
Kwani watu walienda Kilombero kusalimiana au kuzika?
Na kwa nini Pasco usiwatufute watu waliopanga utaratibu wa kukaa na kuwauliza ilikuwaje hawakumpangia nafasi Dr Slaa karibu na Rais ili wasalimiane?

Kwa kumbukumbu zangu Rais Kikwete alituma salamu za rambirambi kwa CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti wake (Mbowe) sasa hizi chokochoko za kusalimiana zinatoka wapi? Na Rais Kikwete kasalimiana na kila aliyehudhuria mazishi? au watu wote waliokaa kwenye jukwaa alimokaa yeye Rais? Hii hoja ingekuwa na mashiko kama Rais na Dr Slaa wangekutana ana kwa ana mmoja wao akatoa mkoni kama ishara ya kusalimiana lakini mwingine akauchuna. Kinyume na hapo ni useless spinning. sorry!
PASCO hajawahi kuwa great thinker, hajawahi kuitumia akili yake kwa uwezo wake wote, daima huwa ni mtu mwepesi kufikiri, najua anajijua pia ...alizuka na hii mada akidhani kuna jipya katika hilo, hawa watu kama Pasco ni sawa na wale watu wanaoandaa makamera yao kusubiri mgonjwa afe , wakati wauginjwa hujificha na kukwepa wajibu,,,,,,,,,,,,,hatukwenda Ifakara kusalimiana , tulienda kuzika, uwe Rais , Makamu wa Rais, uwe Padre ama Shekhe.

"Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa ni upande mwingine na rais alikaa upande mwingine, isingekuwa busara mimi kutoka huko upande wangu kukatiza pale mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!."

Haiingii akilini Katibu Mkuu asiwekwe mbele. Hapo Slaa kama kawa kawahadaa waandishi.
Sioni shida hapa, labda za kiusalama tu, alafu itifaki ilizingatiwa, hata kule Matombo na Mtombozi hakusalimiana na wote.
 
hii stori ina utata, swali ni moja tu, Dr Slaa ni mtu mkubwa ndani ya Chadema, iweje yeye wampange jukwaa tofauti na mwenyekiti wake Mbowe, yaani wapangaji wameona wamweke Zitto jukwaa kubwa na Slaa jukwaa dogo la wabunge...probably ni coincidence ila i really doubt that

Hii nayo inaweza kuibua maswali mkuu. Haingii akilini kabisa aina hii ya protokali. Dr Slaa ni kiongozi wa chama kitaifa. Iweje asipangwe jukwaa na viongozi wenzake wa kitaifa. Kama ni kupangwa basi ilikuwa ni mpango wa makusudi kabisa kwa sababu mallumu.
 
Nikikuelewa, ntakujibu
Sitaki kujibu bila kuwa na hakika kama ulinipata.

Inawezekana wewe ni miongoni mwa wale abiria walioachwa?

Pole sana ndugu yangu, tupo mchanganyiko sasa, just to let you know, uki scroll all the way up you will realise lol
 
Kwenye ili tusitake kumtetea dr slaa ukweli ni kwamba dr slaa amemnunia rais kikwete na sababu ni dr slaa anaamini alishinda urais ila amezulumiwa na rais kikwete,na mwanzoni alishawishi ukawa ni msimamo wa chadema lakini sasa ivi chadema wanamkubali rais kikwete.kwaiyo umebaki kuwa ni msimamo wa dr slaa. Nakwa ili asipoangalia litamuomdolea heshima na iman walio nayo watanzania kwake matokeo yake kupolomoka kisiasa. Aache chuki ajiandae kwa uchaguzi ujao kwa maana asije akaamishia chuki kwa viongozi wenzie wanaomkubali rais kikwete akaja kukivuluga chama
 
"Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa ni upande mwingine na rais alikaa upande mwingine, isingekuwa busara mimi kutoka huko upande wangu kukatiza pale mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!."

Haiingii akilini Katibu Mkuu asiwekwe mbele. Hapo Slaa kama kawa kawahadaa waandishi.
Huwa hamkosi sababu FF hivi kwa kuwa ni Katibu Mkuu ndio lazima awekwe mbele afterall wapi panasema lazima Katibu Mkuu awekwe mbele ili asalimiane na Rais au kuna protokali gani inasema hivyo?
 
Kwenye ili tusitake kumtetea dr slaa ukweli ni kwamba dr slaa amemnunia rais kikwete na sababu ni dr slaa anaamini alishinda urais ila amezulumiwa na rais kikwete,na mwanzoni alishawishi ukawa ni msimamo wa chadema lakini sasa ivi chadema wanamkubali rais kikwete.kwaiyo umebaki kuwa ni msimamo wa dr slaa. Nakwa ili asipoangalia litamuomdolea heshima na iman walio nayo watanzania kwake matokeo yake kupolomoka kisiasa. Aache chuki ajiandae kwa uchaguzi ujao kwa maana asije akaamishia chuki kwa viongozi wenzie wanaomkubali rais kikwete akaja kukivuluga chama
Habari za kuambiwa changanya na za kwako...
 
Hivi ile siku chadema walipokwenda ikulu kuongea na kikwete dr. Slaa naye alikuwepo?
 
Sababu ni Dr. Slaa anaamini Kikwete alimuibia kura uchaguzi wa 2010 kwa hiyo bado ana beef naye.
 
Hii nayo inaweza kuibua maswali mkuu. Haingii akilini kabisa aina hii ya protokali. Dr Slaa ni kiongozi wa chama kitaifa. Iweje asipangwe jukwaa na viongozi wenzake wa kitaifa. Kama ni kupangwa basi ilikuwa ni mpango wa makusudi kabisa kwa sababu mallumu.

Kuna uzi ulianzishwa hapa kuwa Slaa ajihadhari atapokuwa msibani, inawezekana kutokuka jukwaa kuu na viongozi wenzie ndio tahadhari yenyewe. Speculations.
 
Back
Top Bottom