Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi
Baada ya kumpumzisha mpendwa wetu, Regia sasa hatupeani pole tena bali sasa tunafanya reflections za baadhi ya legacy Regia aliotuachia na lessons ambazo tumezipata kwenye msiba huu!.

Kwa wale tuliofika Ifakara tumeushuhudia umati na divesity ya vyama iliothibitisha Regia hakuwa proponent wa politics za hostilities ndio maana alimpigia kampeni Diwani wa CUF na yeye aliungwa mkono na wapinzani.

Kitendo cha JK kushiriki kwenye msiba huu kwa nguvu alioshiriki nayo, siamini ndio alimpenda Regia kihivyo kiasi cha kwenda Tabata na baadae akahudhuria maziko mpaka makaburini!.

Kwa maoni yangu, ushiriki huu wa JK ni genuine sympathy kwa msiba huu uliotokea as a shock na aka streach na ku extend his consoling hands kwa Chadema with inner signs za "Lets burry the hatchet" and move forward!.

JK alipokubali kukutana na uongozi wa Chadema kuzungumzia muswada wa katiba, Dr. Slaa hakuhudhuria na hakuna excuse yoyote rasmi iliotolewa kwa public!.

Haya umetokea msiba, JK kaenda Tabata kutoa pole, Dr. Slaa akawa hayupo, JK alipondoka Dr. Slaa ndipo akaibuka!.

Leo kwenye maziko, JK amekuja all that way na Dr.Slaa alikuwepo jee kwa nini hawakusalimiana?!.

Mimi nilihudhuria maziko na nikategesha camera yangu ili nipige picha moja tuu, one and only JK akisalimiana na Dr. Slaa!.

Kwa vile mimi sio mwandishi rasmi, hivyo kupata good shot ya kusalimiana huko kwa karibu ingekuwa ngumu, nilijiegesha mahala pa ukosefu wa heshima kwa marehemu nilipolazimika kupanda juu ya kaburi ili kuipata hiyo picha!.

Nikavizia sana, na muda muafaka ni baada ya mashada au baada ya msiba!. Kweli baada ya msiba JK akasalimiana na huyu na yule nikitarajia this time Dr.Slaa atakuwemo lakini wapi!.

Mara JK huyo akaondoka zake kuelekea kwenye gari yake na kujiondokea zake!. Ndipo Dr. Slaa akaibuka pale mbele!.

Kusema ukweli nilitafuta nafasi ya kumsalimu Dr. Slaa na bila kukopesha nilimuuliza ilikuwaje asisalimiane na rais wakati mkuu wa nchi amekuja all this way kuwapa pole!.

Dr. Slaa alinijibu very genuinely kuwa "Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa ni upande mwingine na rais alikaa upande mwingine, isingekuwa busara mimi kutoka huko upande wangu kukatiza pale mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!.

Mazungumzo yangu na Dr. Slaa yalikatizwa baada ya gari yake kufika ambapo aliingia kwenye gari yake huku akishangiliwa na umati wa watu ambao walifanya maandamano yasiyo rasmi kwa mchaka mchaka kulisindikiza gari la Dr. Slaa huku wakiimba raisi raisi...

My Take.
Kwa vile bado tunaugulia machungu ya msiba, nauliza kutokuonana huku is it just a mare coincidence or there is more to it?!.

Poleni sana Chadema,
2015 bado ni mbali sana!.
Wasalaam
Pasco wa jf
kutoka mazikoni Ifakara.

Update-1
Baadae nimekutana Dr. Slaa mahali na kupata fursa ya kumuuliza yale maswali yangu yaliyobakia.

Dr. Slaa menithibitishia kuwa hajawahi kumkacha Jk hata mara moja, bali kila zilipotokea fursa za kukutana hutokea by chances tuu hawajakutana!,

Hivyo ile dhana yangu ya muendelezo wa misuso nimeifuta.

Asanteni kwa kunielewa!.

Pasco!.
 
mmh
mbona nimemwona Mbowe akisalimiana na Jk? labda wamesalimiana wakati wewe ukiwa na mishemishe nyingine so hukuweza kuona tukio halisi.
 
Wanabodi
......................................
Dr. Slaa alinijibu very genuinely kuwa "Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa kule nyuma na rais alikaa mbele, isingekuwa busara mimi kutoka huko nyuma kuja huku mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!.

Mazungumzo yangu na Dr. Slaa yalikatizwa baada ya gari yake kufika ambapo aliingia kwenye gari yake huku akishangiliwa na umati wa watu ambao walifanya maandamano yasiyo rasmi kwa mchaka mchaka kulisindikiza gari la Dr. Slaa huku wakiimba raisi raisi...

My Take. Kwa wale wenye kumbukumbu niliwahi kusema nini kuhusu tabia za misuso za Chadema na matokeo yake huwa ni nini na katika misuso hiyo Chadema huwa ina gain nini, inavuna nini na ku loose nini!.

Kwa vile bado tunaugulia machungu ya msiba, nauliza kutokuonana huku is it just a mare coincidence or there is more to it?!.

Poleni sana Chadema,
2015 bado ni mbali sana!.
Wasalaam
Pasco wa jf
kutoka mazikoni Ifakara.

mkuu, nadhani hapo penye bold ndiopenye majibu sahihi................

lakini naomba nikuulize, ....................... ni kwa nini unadhani dr ndiye kasusa na hudhani hata kidogo kuwa (huenda) jk kaambia watu wake kuwa hataki kumshika mkono huyo mtu???...................... nakuomba ujaribu kuwa neutral kidogo ili tupate habari isiyoegemea upande wowote..................

pole na hekaheka za ifakara mkuu....................... RIP regia.......................
 
CHADEMA MSIWE WAPOFU
Hebu soma kwanza hapa
"Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa kule nyuma na rais alikaa mbele, isingekuwa busara mimi kutoka huko nyuma kuja huku mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!.
MS mimi siyo CHADEMA.

Kama ningekuwa hivyo, why hide?

Nikijiunga na chama nitakuwa proud to say it loud, kwa sababu huwa sikurupuki kwenye maamuzi kama hayo.

Hilo alilosema Slaa ni sawa tu, i was just speculating kwasababu kuna wakati walisema uchaguzi ulichakachuliwa.
 
Sijaambulia kitu hapa. Mbona mi simsalimiagi MS na maisha yanaendelea?
 
mkuu pasco mimi nakuheshimu sana!sioni sababu za kumlaumu Dr Slaa kiasi hicho bila kufikiri'ok huu msiba umetuunganisha na hawa wadhalimu ccm?umesema Jk kasafiri all way from where?si alikuwa huko huko morogoro akifungua vidaraja?tusijidanganye'Regia kamaliza safari yake sisi bado tunaendelea'mapambano yako palepale hakuna mabadiliko!
 
CHADEMA MSIWE WAPOFU
Hebu soma kwanza hapa
"Mahali nilipopangiwa kukaa palikuwa kule nyuma na rais alikaa mbele, isingekuwa busara mimi kutoka huko nyuma kuja huku mbele just kusalimia!. Pia Dr. Slaa aliongezea ni kawaida rais akifika mahali huanza kwa kusalimia watu wawili watatu ndipo hukaa!.

huu ndio ukweli
aliingia kwenye gari yake huku akishangiliwa na umati wa watu ambao walifanya maandamano yasiyo rasmi kwa mchaka mchaka kulisindikiza gari la Dr. Slaa huku wakiimba raisi raisi
 
Mazishini siyo sehemu ya kuja kusalimiana. Kama JK akitaka kusalimiana na Dr. Slaa amuite Ikulu atakuja lakini si kwa bahati mbaya.
 
mkuu, nadhani hapo penye bold ndiopenye majibu sahihi................

lakini naomba nikuulize, ....................... ni kwa nini unadhani dr ndiye kasusa na hudhani hata kidogo kuwa (huenda) jk kaambia watu wake kuwa hataki kumshika mkono huyo mtu???...................... nakuomba ujaribu kuwa neutral kidogo ili tupate habari isiyoegemea upande wowote................

How many 'political gentlemen' do you know?
 
Back
Top Bottom