hata mimi nawashangaa wa -tz, yaani DR. akisalimiana na kikwete ndiyo nini? watu wanapenda kuunga unga vitu iwe habari...
Kama alisalimiana na Mbowe ambaye ni Mwenyekiti, Akasalimiana na Naibu Katibu Mkuu na wabunge wengi mashuhuri akiwemo Lema, sasa kibaya ni kipi? yaani mimacho yote ilikuwa DR. amfuate kikwete ampe mkono then mpige picha muuze magazeti!! front page!! (DR. Slaa akubali yaishe!!!)
Magazeti yamelikuza hili, Mara DR. Kamkwepa Kikwete Ikulu, Mara DR. Kamkwepa Kikwete siku ya Kuapishwa, sasa tuone kama atamkwepa tena Ifakara!!! ha ha ha - Ongeleeni Umeme umepanda bei si DR. Kumpa salaam kikwete.
Wadau wengine wamesema kama Kikwete ana nia ya kupeana mikono ya DR. si amwite Ikulu - au laa mbona hamkumuuliza Mkuu wa Kaya kwa nini hakumwita DR. wasalimiane alipofika tu pale msibani?