Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Yaani waandishi wa habari banaa hii yote ni kwa ajili wauze gazeti tu yaani kilichoandikwa hapa na nilichoona Ifakara ni vitu viwili tofauti Dk Slaa alipangwa kukaa jukwaa jingine na Kikwete jukwaa jingine sasa watu walikuwa wanataka kwamba Slaa anyanyuke ndio akamsalimie JK yaani mimi sijaona mantiki yoyote kwenye hili suala zaidi ya watu kulifanya kubwa ili wauze magazeti yaani ukiwa haupo kwenye eneo la tukio waandishi wa habari wanaandika vitu vya ajabu na uwongo tu ili wauze magazeti.

Yaani mtu umepangwa kukaa jukwaa la kushoto kama ilivyokuwa kwa Dr Slaa halafu Kikwete ndio kakaa jukwaa kuu ambapo alikuwa pamoja na Mbowe, Zitto, Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Job Ndugai na wengineo sasa mtu unataka kuniambia Dr Slaa atoke jukwaa la kushoto ili tu akamsalimie JK jukwaa kuu naona ndio mawazo ya watu yalivyo ikumbukwe pia kiprotokali pia ilikuwa imepangwa hivyo tulipokutana na Slaa, Pasco alimuuliza Dr Slaa kuhusiana na hili na akamjibu vizuri jinsi utaraatibu ulivyokuwa...ila naelewa ni kwa ajili ya kuuza magazeti ndio maana waandishi wa habari lazima waandike hivyo..

The Finest, you are obsolutely right, Dr. Slaa alipangiwa upande tofauti na alipopangiwa JK nakiri niliposema kiti cha nyuma I meant upande mwingine!.

Nilipoongea na Dr pale pale msibani ni kweli alieleza kupangwa sehemu tofauti hivyo haikuwa busara yeye kutoka huko alikopangwa kuja pale JK alikopangiwa.

Neno kiti cha nyuma was supposed to mean upande tofauti. Hata hivyo the main theme still stands kuwa hawakusalimiana ila sio delibarate wasisalimiane bali imetokea tuucoincidentaly hawakusaliniana!.
 
Duh!

Hizi thread zinanchanganya!

Kuna abiria wengine wanaachwa kwenye hizi hamisha hamisha lol

Mara nimwone Pasco, mara simwoni, anyways Paso kama unaiona hii, basi tumeshaunganishwa meli moja mkuu, hivyo na assume unamwona Captain Finest na mapendekezo yake kwamba meli inaenda kusiko lol

hahhahahahaha! wote tunaletwa huku, nadhani mods wanafanya hivyo kumfariji pasco, vinginevyo sioni vigezo vya hii thread ya pasco kuletwa huku, au labda ndo campain ya kuitangaza chit chat.
 
hahhahahahaha! wote tunaletwa huku, nadhani mods wanafanya hivyo kumfariji pasco, vinginevyo sioni vigezo vya hii thread ya pasco kuletwa huku, au labda ndo campain ya kuitangaza chit chat.
Bora huku, kule chit chat bana kuna thread za ajabu, kwa mfano chini ya hii ya Pasco kulikuwa na inayokwenda kwa jina la "K"

Go figure lol
 
Hapa zishaunganishwa hizi au?

Pasco aje aseme alivyoambiwa na Dr.Slaa kwa sababu The Finest anaongelea alichokiona na sio kujua mipango ilikuwaje awali

Gaijin,

The finest anaongelea alichokiona.
Pasco naye anaongelea alichokiona.
The finest kaweka picha kuthibitisha alichokiona. Pasco hajaweka picha kuthibitisha alichokiona.

Suala la kujua mipango ya kukaa ilikuwaje si la Pasco wala The finest, hilo liko nje ya majukumu yao.

Na kama shida ni kujua mipango ya kukaa ilikuwaje atafutwe mhusika.
 
Duh!

Hizi thread zinanchanganya!

Kuna abiria wengine wanaachwa kwenye hizi hamisha hamisha lol

Mara nimwone Pasco, mara simwoni, anyways Paso kama unaiona hii, basi tumeshaunganishwa meli moja mkuu, hivyo na assume unamwona Captain Finest na mapendekezo yake kwamba meli inaenda kusiko lol
jmushi1, nimeshajibu ile ya finest na nitajibu nyingine zote na kama thead imehamishwa toka chit chat, nami nitairudisha tuendelee!.
 
Pasco una maana ulisafiri mpaka Ifakara kufuatilia kama Dr Slaa atasalimiana na huyo JK wala sio kushiriki mazishi,maana taarifa yako ukiiangalia kwa makini inatoa picha ya kwamba lengo lako ni ama upeleke ujumbe kwa watanzania ya kwamba Dr Slaa anachuki na JK au ni ana kisasi ni ama amejenga uadui.
Imenisikitisha kuona kuwa umesafiri hadi mbali kwa ajili ya udaku usio na faida,kwa taarifa yako kilichokupeleka wala hakina athari kwa Dr Slaa na mimi mfuasi wake na kwa wengine walio wafuasi wake hasa CDM
 
Pasco kaamua kutuchinjia baharini .....:lol:
Itakuwa hivyo, mi naenda kulala, maybe baadae ntakuta majibu yake humu.

Ila bado niko sceptical kuhusu kutuchinjia baharini, unaweza kuta ana type hapo alipo, and maybe it takes time.
 
Thread Hii Nimeifuta kutokana na kudhalilishwa na mode!. Niliiposti Jukwaa la Siasa imehamishiwa jukwaa la kupiga soga!. Kuliko mimi kuonekana mpiga soga nimeifutilia mbali hii thread ila nitajibu tuhuma na shutuma!.

Asanteni kwa kunielewa!.

Maadam imewekwa hoja mchanganyiko nitairudisha hii post na kila hoja itajibiwa!
 
Gaijin,

The finest anaongelea alichokiona.
Pasco naye anaongelea alichokiona.
The finest kaweka picha kuthibitisha alichokiona. Pasco hajaweka picha kuthibitisha alichokiona.

Suala la kujua mipango ya kukaa ilikuwaje si la Pasco wala The finest, hilo liko nje ya majukumu yao.

Na kama shida ni kujua mipango ya kukaa ilikuwaje atafutwe mhusika.

Pasco anasema alimfuata mhusika (Dr.Slaa) na alimjibu kuwa "alipangiwa siiti za nyuma" ......
 
Itakuwa hivyo, mi naenda kulala, maybe baadae ntakuta majibu yake humu.

Ila bado niko sceptical kuhusu kutuchinjia baharini, unaweza kuta ana type hapo alipo, and maybe it takes time.

Yupo kumbe, na kila post itajibiwa, usiondoke hata kidogo :lol:
 
jmushi1, nimeshajibu ile ya finest na nitajibu nyingine zote na kama thead imehamishwa toka chit chat, nami nitairudisha tuendelee!.
Ok mkuu,point noted, sijaiona bado hiyo uliyomjibu The Finest, however ni uamuzi wa busara kuurudhisha mjadala, ok lets move on.
 
mmh!
mbona nimemwona Mbowe akisalimiana na Jk? Labda wamesalimiana wakati wewe ukiwa na mishemishe nyingine so hukuweza kuona tukio halisi.
Uzuri wa Mbowe ni kwamba hapindishi jambo, he calls a spade a spade na hatunzi kinyongo! he is a leader kwa hiyo lazima aonyenyeshe mfano kwa anaowaongoza, besides huo ni msiba wa familia ya Mtema si sehemu ya kuonyesha kinyongo kwa mtu yeyeyote akiwemo JK. so much respect to Mh. Mbowe  he is real gentleman!
 
Bora huku, kule chit chat bana kuna thread za ajabu, kwa mfano chini ya hii ya Pasco kulikuwa na inayokwenda kwa jina la "K"

Go figure lol

aisee nilikuwa sijaona, kumbe tupo habari mchanganyiko? mbona hawa mods wanatupiga danadana hivi? mara wakosee watupeleke jukwaa la kikubwa.
 
aisee nilikuwa sijaona, kumbe tupo habari mchanganyiko? mbona hawa mods wanatupiga danadana hivi? mara wakosee watupeleke jukwaa la kikubwa.
Ha ha ha ha!

Wakitupeleka la wakubwa mbona itakuwa makubwa kwa wengine humu?teh teh teh, mbavu zangu tafadhali!

The fact ni kwamba unaweza jikuta uko ama umeenda "porn" incase wakitupeleka huko "bila kukusudia" kama ilivyotokea kwa chit chat lol
 
Du watu bana kwani kusalimiana na mafisadi lazima?pale ni msibani bana, sio sehemu ya kutambulishana na kushikana mikono ovyo ovyo,wengine wako ki kazi zaidi tunashukuru walimaliza mazishi salama.
 
Nina swali: Viongozi kama Lema waliokuwa wamekaa upande wa dr.slaa walienda kupeana mkono na rais? Je kupeana mkono na rais kulikuwa na significance gani kwenye msiba hasa kwamba Mwenyekiti wa CDM alipeana mkoni na CDM walishakubali kumtambua JK kama Rais?. Kama Slaa na watu wengine wanaamini kua JK alipata urais mara ya pili kwa kutumia mbinde hawana haki ya kuonesha hivyo hata kama ni hadharani? Lakini ni kwa nini watu wa JK wanataka kupata legitimacy toka kwa Dr. Slaa? Kikwete ni rais ametangazwa hivyo na tume that settles it.
 
Njaa ni kitu haramu sana, ndo maana Escobar alijisemea:

There are two hundred million i.d.i..t..s, manipulated by a million intelligent men.
Everyone has a price, the important thing is to find out what it is.

Fanya kazi, watoto wapate kula yao.

Back
Top Bottom