Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

AKWEPA KUKAA JUKWAA KUU,

WENGI WAMZIKA REGIA Juma Mtanda na Shakila Nyerere, Ifakara KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, jana alimkwepa tena Rais Jakaya Kikwete safari hii ikiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala.

Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana. Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Jana, Dk Slaa tofauti na viongozi wenzake wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hakutaka kujiweka katika mazingira ambayo yangemkutanisha na Rais Kikwete katika mazishi hayo. Nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalum kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe. Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais.

Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia. Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alikikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kuwa na mtu. Hata hivyo, Rais Kikwete hakuweza kufika nyumbani hadi mwili wa marehemu Regia ulipopelekwa katika Viwanya vya Viungani ambako uliagwa na mamia ya waombolezaji. Uwanjani hapo nako kulikuwa na majukwaa mawili.

Kama ilivyokuwa nyumbani, jukwaa moja lilikuwa la wabunge na jingine la viongozi wa ngazi za juu lakini bado, Dk Slaa alilikwepa jukwaa hilo ambalo Rais alitarajiwa kuwa angefikia. Rais hakuweza kufika Viungani pia. [Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana.

Picha na Juma Mtanda] Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana.

Picha na Juma Mtanda Baadaye wakiwa eneo la mazishi, Rais Kikwete alifika na kushiriki tukio hilo na kisha kusalimiana na wabunge mbalimbali na viongozi waliokuwa wamefika akiwemo Mbowe, Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, Zitto na viongozi wengine lakini Dk Slaa hakuonekana.

Ilitegemewa kuwa tukio hilo la msiba lingewaleta wanasiasa hao lakini hadi Rais Kikwete alipoondoka hakuna mahali ambako walisalimiana. Mbali ya tukio hilo, hata katika hafla mbalimbali ambazo viongozi wa Chadema wamekuwa wakialikwa ikiwemo Ikulu, Dk Slaa hakuwahi kuhudhuria.

Novemba mwaka jana viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, walifanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam kujadili suala la Katiba Mpya, lakini Dk Slaa hakuhudhuria.

Nafikiri imefika wakati sasa kwa waandishi wa habari wa Kitanzania muonyeshe angalau nini mnajua kuhusu fani yenu,hata kama hamkuiva sawa sawa vyuoni au hamkumpitia kabisa huko lakini mtumie akili zenu kidogo tu ili kufikisha habari sahihi kwa jamihi,tumekua hatujui magazeti ya udaku ni yapi na makini ni yapi!hv kwa akili ndogo tu mnashindwa kuelewa kua alipokaa Dr Slaa si kua alijipangia kupanga ila alipangwa?mmewataja Mbowe na Zitto,mnashindwa elewa kuwa wao ni wabunge,mwenyekiti wa chama,mkuu/naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni!sasa mlitegemea nini?muwe mnatafakuri kidogo kabla ya kufikisha habari kwa jamihi yetu!nyie pia mnachangia sana kudumaza fikra za watanzania kwa habari zenu za udaku udaku tu
 
Pasco kuna thread kule jukwaa la siasa inaendelea na ni same topic, tafadhali naomba uje kule ujibu kwasababu wanasema ulisema uongo kuhusu alichokisema Dr Slaa.
The Finest anasema walipangiwa majukwaa ya tofauti where as wewe ulisema Dr alikwambia alipangiwa siti za nyuma.
 
vyovyote itavokuwa..kama aliamua au alipangiwa, sipendi kabisa Dr.wetu apeane mkono na huyu jamaa.
 
Pasco usijishushe sana...........
MTM, sijajishusha bali kiukweli mimi ni chini!. Hii inamaana chini nilipo sasa ndio stahiki yangu, kule juu nilikotaka niwe nilikuwa najipandisha ili niwe juu ila sasa nimeshuka mpaka mahali panaponistahili!.
 
Hahahahaha!!! Zumbemkuu haya mambo ya siasa wewe yaone hivi hivi tu maana kuna mengine zaidi ya hayo ambayo Slaa alitueleza kule Ifakara nikabakia..:shock::shock:


dah! mkuu ungeyamwaga hata kwa mafumbo tu labda tungeyajua, kaazi kweli kweli.
 
Gee labda kama alitafsiri vibaya maana kila mtu aliyekuwepo kwenye mazishi pale makaburini aliona jinsi sitting arrangement ilivyokuwa

Mkuu hv huyu Pasco ni yule Pasco Mayalla nini?
 
Hahahahaha!!! Zumbemkuu haya mambo ya siasa wewe yaone hivi hivi tu maana kuna mengine zaidi ya hayo ambayo Slaa alitueleza kule Ifakara nikabakia..:shock::shock:


TF, sasa hapo unatuvuruga vichwa tunapata hamu ya kujua ili nasi tupigwe na shock!!
Tafadhali fanya ze needful.
 
Pasco naona meli iko mchanganyiko kwa sasa, nakutakia "sailing" njema lol
 
Pasco kuna thread kule jukwaa la siasa inaendelea na ni same topic, tafadhali naomba uje kule ujibu kwasababu wanasema ulisema uongo kuhusu alichokisema Dr Slaa.
The Finest anasema walipangiwa majukwaa ya tofauti where as wewe ulisema Dr alikwambia alipangiwa siti za nyuma.
Asante, ngoja niende
 
Yaani waandishi wetu ni matatizo tu. mambo wala si makubwa ki hivyo. shit
 
Mkuu nini kinachokufanya uamini aliyokuambia Pasco na sio anayokueleza The finest?

Hiyo ya kiti cha nyuma nabakia kucheka sana aisee sababu nakumbuka mpaka Dr Slaa alitueleza hadi scenario ya Tabata ilivyokuwa huku mke wake ambaye pia alikuwepo akatueleza ni kwanini Dr Slaa alifika Tabata amechelewa baada ya JK kuondoka, maana Tabata pia wakati JK alikuja ilikuwa the same story


Mimi sio kuwa namuamini Pasco na kumpinga Finest. Hapana. Nilichosema ni kuwa tumepata taarifa tofauti kwa source tofauti ambazo zinakinzana.


Ili taarifa za The Finest kuwa Dr.Slaa alipangiwa na ndio maana akakaa jukwa tofauti ziwe sahihi basi Pasco ametudanganya wana ukumbi, na ndio hoja yangu inaposimama

*Finest naamini anaongelea alichoona na sio kujua kwa uhakika mpango wa ukaaji ulikuwaje
 
Jmushi1, sasa kama ni mchangani sailing njema gani unanitakia?. Ingekuwa mchangani njema!.
Lol! Pasco i would've been dissapointed too.

Anyways sisi sote tu wanadamu, la muhimu ni kujifunza penye makosa.
 
Nimetokea mdharau sana Pasco Mayala! Sioni tofauti yake na malaria Sugu! Amekuwa muongo sana!!

Kumbe Pasco huyu ndio Pasco Mayala?aaaargh!nilimuona kwy kpindi fulani cha star tv aliulizaga maswali kwa Tindu Lissu,yaani ni full pumba,asante sana mkuu kunijuza kua ndie Mayalla,sitakua napitia tena thread za huyu jamaha,kwa kua nimeshamjua na kumdharau
 
Mimi sio kuwa namuamini Pasco na kumpinga Finest. Hapana. Nilichosema ni kuwa tumepata taarifa tofauti kwa source tofauti ambazo zinakinzana.


Ili taarifa za The Finest kuwa Dr.Slaa alipangiwa na ndio maana akakaa jukwa tofauti ziwe sahihi basi Pasco ametudanganya wana ukumbi, na ndio hoja yangu inaposimama

*Finest naamini anaongelea alichoona na sio kujua kwa uhakika mpango wa ukaaji ulikuwaje
Nimeenda kumtafuta Pasco, nimempata,meli yake iko kule hoja mchanganyiko, na akaniahidi kwamba anakuja hapa kujibu, nilimweleza everything kuhusu kupingana kwa kauli hizi, kule keshaondoka ila bado simwoni humu...
 
Yaani waandishi wa habari banaa hii yote ni kwa ajili wauze gazeti tu yaani kilichoandikwa hapa na nilichoona Ifakara ni vitu viwili tofauti Dk Slaa alipangwa kukaa jukwaa jingine na Kikwete jukwaa jingine sasa watu walikuwa wanataka kwamba Slaa anyanyuke ndio akamsalimie JK yaani mimi sijaona mantiki yoyote kwenye hili suala zaidi ya watu kulifanya kubwa ili wauze magazeti yaani ukiwa haupo kwenye eneo la tukio waandishi wa habari wanaandika vitu vya ajabu na uwongo tu ili wauze magazeti.

Yaani mtu umepangwa kukaa jukwaa la kushoto kama ilivyokuwa kwa Dr Slaa halafu Kikwete ndio kakaa jukwaa kuu ambapo alikuwa pamoja na Mbowe, Zitto, Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Job Ndugai na wengineo sasa mtu unataka kuniambia Dr Slaa atoke jukwaa la kushoto ili tu akamsalimie JK jukwaa kuu naona ndio mawazo ya watu yalivyo ikumbukwe pia kiprotokali pia ilikuwa imepangwa hivyo tulipokutana na Slaa, Pasco alimuuliza Dr Slaa kuhusiana na hili na akamjibu vizuri jinsi utaraatibu ulivyokuwa...ila naelewa ni kwa ajili ya kuuza magazeti ndio maana waandishi wa habari lazima waandike hivyo..

Bila shaka yatakuwa magazeti ya udaku.
 
Mimi sio kuwa namuamini Pasco na kumpinga Finest. Hapana. Nilichosema ni kuwa tumepata taarifa tofauti kwa source tofauti ambazo zinakinzana.


Ili taarifa za The Finest kuwa Dr.Slaa alipangiwa na ndio maana akakaa jukwa tofauti ziwe sahihi basi Pasco ametudanganya wana ukumbi, na ndio hoja yangu inaposimama

*Finest naamini anaongelea alichoona na sio kujua kwa uhakika mpango wa ukaaji ulikuwaje

Huyu Pasco anakuza mambo au anakurupuka kuleta habari huku akijua anaudanganya umma,protocal viongozi walikaa kutokana na jinsi walivyopangiwa na si walivyojiamulia
 
Nimeenda kumtafuta Pasco, nimempata,meli yake iko kule hoja mchanganyiko, na akaniahidi kwamba
anakuja hapa kujibu, nilimweleza everything kuhusu kupingana kwa kauli hizi, kule keshaondoka ila bado simwoni humu...

Hapa zishaunganishwa hizi au?

Pasco aje aseme alivyoambiwa na Dr.Slaa kwa sababu The Finest anaongelea alichokiona na sio kujua mipango ilikuwaje awali
 
Duh!

Hizi thread zinanchanganya!

Kuna abiria wengine wanaachwa kwenye hizi hamisha hamisha lol

Mara nimwone Pasco, mara simwoni, anyways Paso kama unaiona hii, basi tumeshaunganishwa meli moja mkuu, hivyo na assume unamwona Captain Finest na mapendekezo yake kwamba meli inaenda kusiko lol
 
Back
Top Bottom