Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Kama jeshi la polisi ambalo linawajibika kwa Rais halina nidhamu unadhani hiyo idara ya uhamiaji kwa kufanywa jeshi kamili na kuwajibika kwa Rais ndiyo itaongeza nidhamu!?
hayo ni majeshi mawali tofauti yenye kazi tofauti kabisaaa. kila mmoja ana jukumu lake.
huwez linganisha weledi wa jeshi la uhamiaji kwa kutumia reference za police... hiyo sio fair comparison.
 
Kwa mujibu wa Katiba majeshi yako mengi sana.
Sijui ilikuwa mistake au nini, eti jeshi la Polisi, sijui linapambana na nani

Jeshi la Magereza linapambana na nani? Kazi ya kubadilisha tabia za wahalifu au wafungwa linahitaji wanasaikolojia, wataalamu wa fani mbali mbali kwa ajili ya kufundisha njia mbadala za maisha, sasa askari wa kukesha analinda atamfundisha nini mhalifu wakati ye mwenyewe ana stress zake kibao
Nope watu wengi wasicho kijua ni kuwa. Kuna jeshi kamili moja nchi hii.
nali ni jeshi la wananchi wa tanzania.

Taasisi zingine zinazofuata ni paramilitary element. sio full military elements.
na hii ni according to sheria za nchi.

ndio maana JWTZ wana oversee paramilitary forces zote nchi hii. akina police, uhamiaji, maliasili wote hao si full military forces ni paramilitary
 
Kuongeza nidhamu kwa kuwajibika kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye anamuhofia kumtimua kazi zero pamoja na kuvurunda kwa kiasi kikubwa ná jeshi hilo kukosa nidhamu kabisa na kusababisha Watanzania kila kona nchini kulichukia jeshi hilo kwa kutenda dhuluma na udhalimu kwa Watanzania!? 😳
Hii nchi sijui ililogwa na nani. Wizara iliyopswa kyvunjwa ni Ardhi na Makazi. Wizara hii imefeli sana kwenye Urbanisation... huwezi kuchanganya mambo ya Urbanisation na mashamba huko vijijini... this is absurd
 
Uhamiaji kuanzia enzi za kuanzishwa kwa Taifa hili ni Askari sijajua huo ujeshi mpya ni upya au labda makaratasi na sheria ndo havikusoma hivyo.

Lakini Duniani kote Hawa watu uingia kwenye kundi la maafisa usalama, Hawa ni watu wanaopaswa kuwa na ueledi wakung'amua ujasusi wa kiuchumi,kisiasa na kitamaduni kutoka nje. Bila kuwa na maafisa usalama kwenye chombo Kama hiki nchi itavamiwa kirahisi Sana.

Miaka ya nyuma Hawa watu walikuwa hawafahamiki wengi walikuwa wanaficha utambulisho wao, baadhi wanaofanya kazi mipakani ndo walikuwa wanafahamika......

Nadhani hakuna jipya maana Kama TISS Ni Jeshi kwanini tunatangaza uhamiaji kuwa ni Jeshi leo wakati ni tawi moja?

Nadhani wanatafuta sheria yakuwaingiza mtaani rasmi wakiwa na mitutu Jambo ambalo kwangu sioni Kama Lina tija, wabaki na ukachero Kama zamani waache kuwatisha wageni na ujeshi.....hatuahitaji ujeshi kushughulika na wageni nchini tunahitaji welcome face
 
Wakuu, hivi kuna tofauti kati ya jeshi na polisi?

Au ukitamka ujumla wake ndio unatamka kama jeshi.

Mimi hii inanichanganya wakati mwingine Wakuu

====

Bunge la Tanzania leo limepitisha Muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na 5) wa mwaka 2021 ambao unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria tisa (9) na moja wapo ni Sheria ya Uhamiaji.

Kifungu cha 4 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuitambua Idara ya Uhamiaji kama Jeshi na kumpa Waziri mamlaka ya kutengeneza kanuni zitakazoainisha haki na stahili mbalimbali kwa Maafisa Uhamiaji kama za Majeshi mengine chini ya Wizara, pamoja na hayo pia inapendekezwa kubaki na dhana ya “Idara” katika Sheria badala ya kubadili jina kuwa “Jeshi la Uhamiaji” ili kuendeleza taswira ya kidiplomasia ya Idara katika Jumuiya ya Kimataifa.

"Niseme kweli Mh. Spika hata kwa ilivyo sasa ukimuangalia Kamishna Jenerali na wale Askari wote na wamevaa vyeo tayari wana sura ya Kijeshi na wanashiriki katika vikao vya kamati mbalimbali za Ulinzi na Usalama sambamba na Vyombo vingine vya kijeshi" ——— Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene.

"Kwanini leo hii tunataka kutunga sheria hii, unaposema Jeshi maana yake ni nidhamu, tunataka chombo hiki kiwe na nidhamu na kifanye kazi kwa amri, chombo kinachofanya kazi kama Jeshi kinakua chini ya Amiri Jeshi Mkuu lakini kwa ilivyokuwa kilikua ni kama hakipo chini ya Amiri Jeshi Mkuu lakini kinafanya kazi na Amiri Jeshi Mkuu sasa tunarasimisha

Waziri Simbachawene.
 
Kuongeza nidhamu kwa kuwajibika kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye anamuhofia kumtimua kazi zero pamoja na kuvurunda kwa kiasi kikubwa ná jeshi hilo kukosa nidhamu kabisa na kusababisha Watanzania kila kona nchini kulichukia jeshi hilo kwa kutenda dhuluma na udhalimu kwa Watanzania!?
Hamza kawakurupua , Mpaka UVCCM kutakuwa jeshi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hahahahahaha tusishangae Mkuu maccm YANAWEWESEKA sana sasa hivi. Nchi haiko shwari kwa hofu yao ya kutoruhusu UHURU, HAKI na USAWA nchini wa raia, vyombo vya habari na vyama vya siasa kwa miaka mingi sasa na nchi kujaa dhuluma na udhalimu. Wamejawa na hofu kubwa sana ya akina Hamza wengi kuibuka nchini. Imagine damage kubwa ya Hamza mmoja, itakuwa kizaa zaa na balaa kubwa kukiwa na akina Hamza 2,000 hivyo wameanza kugawa silaha hata kwa wasiohusu kitu.
Hamza kawakurupua , Mpaka UVCCM kutakuwa jeshi
 
Ukitaka kujua machadema aliyowaroga kafa soma comments zao,kweli ni vituko
 
Hili jeshi la wanawake wamejaamo wahamiaji haramu kutoka Rwanda wakijiita wanyambo
 
Bunge limefanya mabadiliko madogo ya sheria ya idara ya Uhamiaji ambapo sasa litakuwa ni jeshi kamili litakalowajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza nidhamu kwa idara ya Uhamiaji ambapo sasa litajiendesha kwa Amri.

Source: ITV habari
Mkuu kabla ya hapo ilikuwaje?

Lilikuwa likiwajibika kwa nani?
 
Kwahiyo wahamiaji haramu watakamatwa na uhamiaji moja kwa moja na sio polisi tena?
Inatakiwa iwe hivyo. Marekani kuna ICE ambao wako chini ya immigration moja kwa moja na ndio wanaowakamata wazamiaji na kuwatupa jela. Miaka ya nyuma kidogo waliwanasa watanzania wawili hapa kwetu, mmoja tukafanikiwa kumnasua lakini yule mwingine akawa deported- hakupata nafasi ya kurudi kwenye apartmenet yake wala kupewa nafasi ya kukusanya mali zake, bali alirudishwa Tanzania kama walivyomnasa akiwa amevaa kaptula na T-shirt. Gari lake zuri sana la Nissan Murano likabaki pale pale walipomnasia hadi baada ya wiki moja ndipo likaja kuvutwa na jamaa wa City kulipeleka Junkyard.
 
Back
Top Bottom