Rais Samia: Utafiti umebaini kuna matumizi mabaya ya fedha Idara ya Uhamiaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji Kozi na. 1/2022, katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba leo tarehe 15 Agosti, 2022 Mkoani Tanga.


MKUU WA MKOA TANGA – OMARY TABWETA MGUMBA

Mrundikano wa wafungwa kutoka nje wasio na makosa
Magereza yetu yamejaa wasafirishwaji ambao sio wafungwa, siyo mahabusu na hawajafanya kosa lolote. Kwa taarifa za leo kuna wafungwa zaidi ya 2053, kati ya hao 946 ni wa mataifa ya nje(wageni) na kati ya hawo 893 ndio wasafirishwaji. Wamemaliza vifungo vyao na wanasubiri kurudi kwenye mataifa yao lakini kwenye mataifa yao hakuna jitihada zozote zinazofanywa kuwachukua na matokeo yake wafungwa waofanya shughuli za uzalishaji kuwalisha hawa wanazidiwa.

Watumishi wa umma na biashara haramu ya binadamu
Baadhi ya watanzania ikiwemo watumishi wa umma wanajihusisha na biashara haramu ya kununua na kuuza binadamu, kichwa(mtu) kimoja kinauzwa kwa laki moja na hamsini. Kwa kushirikiana na vyombo vya usalama watumishi hao wamekamatwa na taratibu nyingine zitafatwa kuhakikisha wanashughulikiwa kukomesha vitendo hivyo.


SAMIA SULUHU HASSAN - RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ahadi ya serikali kwa vyombo vya ulinzi na usalama
Serikali itahakikisha kuendelea kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama ili viendelee kutekeleza vyema majukumu yake ya ulinzi wa taifa, kutoa ajira mpya, upandishwaji wa vyeo kwa wakati na kulipa stahiki mbalimbali kadri uchumi na hali ya bajeti itakavyokuwa inaruhusu.

Jeshi la Uhamiaji na kasi ya teknolojia
Pamoja na mafanikio mengi katika Jeshi la Uhamiaji bado kuna kazi kubwa ya kuendelea kubuni mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuboresha zaidi utendaji wao kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kukabiliana na mbinu mpya za uhalifu zinazijitokeza mara kwa mara. Haya yote yanatakiwa kufanyika bila ya kuwabugudhi wananchi, wageni na wawekezaji nchini.

Maafisa uhamiaji kurudi kambini kupigwa msasa
Maafisa amabo hawajui majukumu yao, wanaopokea rushwa na kufanya vitendo vya unyanyasaji kwa wageni wanatakiwa kurudi kupata mafunzo na kuimba wimbo unaohamasisha kufanya majuku yao kama inavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuiishi kauli mbiu yao ya umoja, upendo, mshikamano, uwajibikaji na kukataa rushwa. Wanaotakiwa pia kurudi kwenye mafunzo ni maafaisa waliokaa kazini mda refu na kufanya kazi kwa mazoea.

Idara ya Uhamiaji na vitendo vya rushwa
Utafiti mdogo uliofanywa mapema mwaka huu umebainisha kuwa na vitendo vya rushwa kutoka kwa maafisa wa uhamiaji ambayvo vinafanyika sana Zanzibar na Dar Es Salaam. Vitendo hivi vinatakiwa kukomeshwa ili kuweka taswira ndani ya jeshi kwamba atakayefanya makosa haya atashughulikiwa na wengine hawatakiwi kuiga vitendo vyao.

Chuo cha Uhamiaji kushirikiana na Wizara ya Kilimo
Chuo cha Uhamiaji washiriakiane na Wizara ya Kilimo wawajengee mabwawa ili waweze kuzalisha na kujitegemea kwenye chakula badala ya kulima mkonge pekee unaokaa miaka kadhaa kabla ya kuvunwa.

Maafisa wa Uhamiaji Zanzibar na Tanzania Bara kubadilishana uzoefu
Ili kuondoa mazoea kwenye kazi na kubadilishana uzoefu Rais Samia ameshuri maafisa wanaotoka Zanzibar wapelekwe Tanzania Bara na wanaotoka Tanzania Bara kupelekwa Zanzibar.​




RAIS SAMIA AGUSIA RUSHWA, UNYANYASAJI KUKITHIRI UHAMIAJI
Rais Samia Suluhu amesema kuna malalamiko mengi kuhusu maafisa wa Idara ya Uhamiaji zikiwemo tuhuma za rushwa, unyanyasaji na malalamiko mengine kutoka kwa wageni, na ameagiza maafisa wazoefu warejeshwe vyuoni kupigwa msasa.

Aidha, amesema wapo Maafisa ambao sio waaminifu, wanachukua fedha za Visa na vibali wanaweka mifukoni, akieleza utafiti uliofanywa umeonesha vituo vyenye matatizo zaidi katika suala hilo ni Zanzibar na Dar es Salaam.

Ameagiza urasimu huo ukomeshwe na wahusika washughulikiwe huku akisisitiza kuacha kuchelewesha Visa kwa wale ambao hawana tatizo la kuingia Nchini.
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu ameonesha kukerwa na vitendo vya rushwa na ubadhirifu miongoni mwa maafisa na askrai wa Jeshi la uhamiaji

Rais Samia akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Askari wa uhamiaji mkoani Tanga ameeleza kuwa kwa sasa kama Taifa tunashuhudia kiasi kikubwa cha kutoa rushwa kwa maafisa uhamiaji lakini pia tunashuhudia vitendo vya unyanyasaji kwa wageni wanaoingia nchini ambapo malalamiko kutoka kwa wageni ni mengi

Rais Samia ameagiza maafisa na askari walioko vituoni (Stations) hivi sasa ambao hawajapata mafunzo katika chuo hicho warudishwe katika chuo hicho ili wapikwe na kufunzwa upya na wale waliomaliza mafunzo yao wakachukue nafasi zitakazoachwa wazi.

Amesisitiza kusimamia kauli mbiu ya upendo ,umoja mshikamao uwajibikaji pamoja na kukaata rushwa
2 (8).jpg
 
Kwa kauli ya Mheshimiwa rais sidhani kama Kamishna mkuu wa uhamiaji atapona katika mabadiliko mapya kwa vyombo vya ulinzi na usalama !

Tutarajie mkuu mpya wa jeshi la uhamiaji muda si mrefu atakayeweza kuleta mabadiliko anayotaka Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania.
 
Kwa kauli ya Mheshimiwa rais sidhani kama Kamishna mkuu wa uhamiaji atapona katika mabadiliko mapya kwa vyombo vya ulinzi na usalama !

Tutarajie mkuu mpya wa jeshi la uhamiaji muda si mrefu atakayeweza kuleta mabadiliko anayotaka Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania.
Washamtafutia Zengwe tayari. Kama anajielewa hii ni warning sign anatakiwa ajiuzulu je huu si utakuwa ushindi ka kina Adv Madeleka?
 
Huyu Mama anayo haki ya kupata mapumziko , mbona mnamzungusha sana jamani ! mnataka aanguke jukwaani ?

Yeye ndio anapenda na ana amini kuonekana na tbc kila siku tutasifia kuonesha ana tenda kazi kisawa sawa. Kila siku awepo kwenye gazeti
 
Hili nalo suala la vitambi muende mkalitizame,Ummy Mwalimu na timu yako.
 
Back
Top Bottom