DOKEZO Kurasini - Dar: Baadhi ya maofisa wa Uhamiaji, wamekuwa na vitendo vya wazi vya kuomba rushwa ili kukupatia huduma kwa wakati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
319
Ndugu ZANGU,

Mimi kimajukumu ni mchungaji wa Kanisa hapa Dar es Salaam.

Napenda kueleza uma masikitiko yangu juu ya ofisi za uhamiaji (immigration) zilizopo kurasini.

Baadhi ya maofisa wa Immigration hapo wamekuwa na vitendo vya wazi vya kuomba rushwa ili kukupatia huduma kwa wakati. Na usipo kubali basi wata hakikisha unazungushwa kupata huduma na mwishowe utajikuta umeingia gharama kubwa.

Mfano; Mimi na mke wangu tulikwenda kwaajili ya kupata pasi za kusafiria, tumezungushwa sasa mwezi mzima na hakuna sababu yeyote ya msingi. Ila kwa ujasiri afisa anakupa namba umpigie simu na nilipopiga waliomba rushwa kwa ujasiri kabisa ili nipate passport yangu.

Nilipokataa kutoa, mpaka leo ninapo andika mwezi umeisha nimeenda zaidi ya mara tatu, Kila baada ya wiki moja na sijapata passport yangu. Katika upelelezi wangu kupitia wateja wengine, ndipo niligundua huu ni mchezo wao wa rushwa ya wazi wazi kabisa.

Ningependa mamlaka husika zichukue hatua, TAKUKURU, wizara ya mambo ya ndani na Jeshi la Polisi as well .

Nilitakuwa niwe nimesafiri sijafanikiwa, ratiba imevurugika ya safari, nazidi kuingia gharama. Kila nikienda ninapigwa tarehe, njoo siku fulani, njoo siku fulani. Na nikija naambiwa tu bado bado, huku naombwa rushwa!

Tupaze Sauti zetu Kukomesha uovu huu katika ofisi za UHAMIAJI. Huduma Bora ni haki yetu , sisi ni walipa Kodi sio watoa rushwa!
 
1. Fika ofisi ya TAKUKURU au piga simu 113 ukawashikishe za Moto. Tupate ushahidi mahakamani.

2. Hiyo picha ndio Kurasini? Au umetunga majungu tu?
 
Mkuu ulikua na vigezo vyote vya kupata hiyo passport? Kwa watu ambao wana vigezo vyote ni ngumu sana kuzungushwa ila kama kuna baadhi ya documents haziko sawa lazima wakuzungushe ili kutengeneza mianya ya upigaji
 
Wewe ni mchungaji tunaamini usemayo ni mkweli na una ushahidi na kwa kuwa lengo lako ni kukomesha hizi mambo na kwa kuwa umeshavutugiwa ratiba zako na kwa kuwa kila mstaarabu anapinga hivi vitendo katika jamii basi ni kwanini usimtaje huyo ofisa na kuweka namba yake hapa?
 
Ndugu ZANGU,
Mimi kimajukumu ni mchungaji wa Kanisa hapa Dar es Salaam.


Kwanza niwe PILATO hapa:
Picha uliyoiambatanisha kuhusisha na lawama zako,
Mahakamani zinakutia hatiani. Huwezi kumtuhumu Juma kwa Kosa fulani kisha unaleta picha yenye taswira ya John ndani ya tuhuma hizohizo, Hapa UMEFELI na inatia mashaka juu ya umakini wako.

Nathubutu kusema kuna kila dalili Nyaraka zako HAZIJITOSHELEZI na upo mwanya unaolazimisha kufanyiwa 'namna fulani' ili upate 'Nondo' yaani kama ka-upendeleo fulani hivi na hilo ndilo 'Tundu la Panya',
Wazee wanataka utoe 'ushiriano wa aina hiyo' sasa kumbe nini? kila mtu anakula pake.
Sababu vinginevyo walipaswa wakuambie huwezi kupata kabisa,
Jema lipi sasa? wakusaidie uwasaidie kidogo ama vipi?

Jamani, mnyonge mnyongeni na anapokuwa na Haki msimbanie, Mpeni tu.
Hakuna sehemu rahisi na isiyo na usumbufu kupata huduma kama Idara ya Uhamiaji hii naongea kwa uzoefu.
Angalizo ni kuwa ujaze form zao vizuri na uwe na nyaraka sahihi zinazohitajika za kuambatanisha na pia ukihojiwa uwe umenyooka ukieleta mashaka unataka wao wafanyeje?

Kumbuka Hati ya Kusaifiria sio Tiketi ya Daladala, ni Nyaraka nyeti,
Shurti wazee wajiridhishe wanampa nani na hata likitokea la kutokea wawe na maelezo ya kwa nini walikupatia.

Pengine tuanzie hapa kidogo;
1-Wewe ni Raia wa Tanzania? Sio uanze Baba alioa.... au Mama aliolewa aka, ..na mimi ikawa...Sio Stori?
Kama huna ushahidi lazima watakung'ang'ania tu.
2-Je, Unacho Cheti/Uthibitisho wa kuzaliwa hapa Tanzania? au kuzaliwa na Wazazi/Mzazi mmojawapo mwenye Uraia wa Tanzania?
3-Je, Unao uthibitisho wa Kuzaliwa/Cheti au Kiapo cha Kuzaliwa cha angalau Mzazi wako mmoja mwenye Uraia wa Tanzania?
4-Je, Unayo sababuyenye mashiko na Uthibitisho wake wa Shughuli inayokupeleka huko nje unakotaka kwenda?

Kama unakosa kumiliki chochote kati ya hivyo nilivyovitaja hapo juu,
Ndugu kuwa mpole na ongea nao kwa utulivu hao waungwana, sio wajinga hao.
Ni upendeleo wanaokufanyia lakini kiukweli hustahili hata kusogelea Ofisi za uhamiaji.

Iwapo vyote hivyo unavyo na bado unazunguushwa naungana na wewe na nitakuwa mmojawapo kwenye maandamano yako twende tukamuone Mama MAKAKALA.

Nawasilisha.
 
Angekusanya ushahidi na kuripoti panapohusika kuliko kuwastua na kubadili mbinu za kuomba iyo kitu
angekuja tu kuwaanika kwenye mitandao akiwa na ushahidi sasa mtu mpaka unapigiwa simu na unazungushwa hivyo unashindwa kukusanya ushahidi wakati mange kimambi ndio kazi yake hiyo😂
 
Rushwa hapa Tanzania ni halali
Acha ujuaji kama jambo unalotaka kusafiria linakupa pesa ndefu unashindwa nini kumpenyezea huyo mkuu kitengo hata laki tu

Mambo yako yakunyokee
Tanzania hakuna haki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu ZANGU,
Mimi kimajukumu ni mchungaji wa Kanisa hapa Dar es Salaam.

Napenda kueleza uma masikitiko yangu juu ya ofisi za uhamiaji (immigration) zilizopo kurasini.

Baadhi ya maofisa wa Immigration hapo wamekuwa na vitendo vya wazi vya kuomba rushwa ili kukupatia huduma kwa wakati. Na usipo kubali basi wata hakikisha unazungushwa kupata huduma na mwishowe utajikuta umeingia gharama kubwa.

Mfano; Mimi na mke wangu tulikwenda kwaajili ya kupata pasi za kusafiria, tumezungushwa sasa mwezi mzima na hakuna sababu yeyote ya msingi. Ila kwa ujasiri afisa anakupa namba umpigie simu na nilipopiga waliomba rushwa kwa ujasiri kabisa ili nipate passport yangu.

Nilipokataa kutoa , mpaka leo ninapo andika mwezi umeisha nimeenda zaidi ya mara tatu, Kila baada ya wiki moja na sijapata passport yangu. Katika upelelezi wangu kupitia wateja wengine, ndipo niligundua huu ni mchezo wao wa rushwa ya wazi wazi kabisa.

Ningependa mamlaka husika zichukue hatua, takukuru, wizara ya mambo ya ndani na Jeshi la Polisi as well .

Nilitakuwa niwe nimesafiri sijafanikiwa, ratiba imevurugika ya safari, nazidi kuingia gharama. Kila nikienda ninapigwa tarehe ,njoo siku fulani, njoo siku fulani. Na nikija naambiwa tu bado bado, huku naombwa rushwa!

Tupaze Sauti zetu Kukomesha uovu huu katika ofisi za UHAMIAJI. Huduma Bora ni haki yetu , sisi ni walipa Kodi sio watoa rushwa!
View attachment 2889446
Suala lako limeshawafikia wahusika ukishapata passport yako uje ufanye update ya Uzi wako hapa useme umeshapata na umeshasafiri,
 
Passport yangu ya zamani, vile nilikua na haraka ya kusafiri, niliwahi kutoa Rushwa, ila Passport hizi mpya zilipotoka, nikasema sitoi hata Kumi, moja ya maeneo ambayo wanatengeneza mazingira ya Rushwa ni pale wanapotaka Vyeti vya kuzaliwa vya Mzazi angalau mmoja....!

Unakuta Mzazi alishafariki, Bibi alijifungulia Nyumbani, miaka hiyo Nyerere bado anachunga Ng'ombe Musoma, unataka mimi niwe na Cheti cha Mzee nakitoa wapi....!?

Nikawaambia kama mlinipa Passport ya zamani bila maswali haya mnayoniuliza sasa, japo nawapa majibu na bado mnaweka Vikwazo, mimi sitaridhika, nitaenda kulalamika kwa Boss wenu...!

Uso ukiwa Mbuzi, nanyoosha maelezo.... Kidogo ikasaidia, nikapata Passport...!

Mtoa mada kama unaona hujatendewa haki, nenda kamuone Boss wao, toa malalamiko yako, Watakusikiliza, Officers wanaochukua Rushwa ni hawa officers wa chini, nenda juu utasaidika.
 
Back
Top Bottom