Waziri wa Ulinzi afungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
836
534
WAZIRI WA ULINZI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

- Asisitiza Umuhimu wa Mshikamano na Uwajibikaji.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrance Tax, tarehe 06 Aprili, 2024 amefungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT na kuwataka washiriki wa Baraza la wafanyakazi kuzingatia umuhimu wa Mshikamano na Uwajibikaji katika utendaji kazi.

Waziri Tax ameyasema hayo alipokuwa akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT katika Ukumbi wa Magadu Mess - Mjini Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine amebainisha kuwa Baraza linao wajibu wa kuimarisha mshikamano sehemu za kazi kwa uwiano kwa lengo la kuleta tija na mshikamano baina ya watumishi na mwajiri.

"Haki huendana na wajibu, hivyo kama Baraza la Wafanyakazi mnao wajibu wa kuhamasisha watumishi wa Wizara yetu watekeleze majukumu kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu" Alisema Waziri Tax.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliwaambia washiriki wa baraza hilo kuwa na imani kuwa kupitia chombo hiki ambacho ni mhimili muhimu katika kuimarisha utendaji kazi, na kupitia kikao hicho cha baraza changamoto muhimu za wafanyakazi wa wizara zitachambuliwa kwa kina ili kuhakikisha vipaumbele vya Serikali, hususan vya Wizara ili katika kutekeleza majukumu iliyojipangia kama Wizara katika kuhakikisha maslahi ya watumishi yanazingatiwa.

Aidha, katika hotuba yake hiyo kwa baraza la wafanyakazi, Waziri Stergomena alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuendelea kutimiza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja kuzipatia fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo na pia kuiwezesha Wizara katika matumizi ya kawaida ikiwemo ulipwaji wa mishahara na marupurupu kwa wakati, stahiki za wanajeshi na watumishi wa umma, hivyo kuifanya wizara na taasisi zake za JWTZ, JKT, Nyumbu na Mizinga kuendelea kuimarika na kutekeleza majukumu kwa kiufanisi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akamshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT kwa kukubali kuhudhuria kikao cha baraza la wafanyakazi na kwa hotuba yake nzuri kwa baraza iliyosheheni maelekezo ya msingi ambapo alimuhaidi Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi kuyatekeleza kwa umakini na uharaka.
 

Attachments

 • 20240407_101706.jpg
  20240407_101706.jpg
  37.6 KB · Views: 4
 • 20240407_101710.jpg
  20240407_101710.jpg
  494.8 KB · Views: 4
 • 20240407_101708.jpg
  20240407_101708.jpg
  419.6 KB · Views: 3
 • IMG-20240407-WA0018.jpg
  IMG-20240407-WA0018.jpg
  81.8 KB · Views: 5
 • IMG-20240407-WA0020.jpg
  IMG-20240407-WA0020.jpg
  129.7 KB · Views: 5
 • IMG-20240407-WA0019.jpg
  IMG-20240407-WA0019.jpg
  65.1 KB · Views: 5
Dah magadu mess,,,,, enzi hizo utotoni tumecheza sana mziki hapo xmas na mwaka mpya..........,sijui kama hio kitu bado inaendelea hadi siku hizi, naona na mazingira yamebadilika
 
Back
Top Bottom