Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

KNKCU

Kwa hiyo wa kulaumiwa ni wasaidizi?
 
Katika usomi anaojivunia JK si ndio huu wa Economics pale mlimani?

kusoma,kujivunia kusoma na kutekeleza kwa vitendo uliyoyasoma ni vitu vitatu tofauti....na haviko automatic! hata manualization yake ni kaazi kweli kweli!.

si lazima uwe mchumi ili uchumi wende vizuri...kinyume chake ni sahihi pia!.
 
KNKCU

Kwa hiyo wa kulaumiwa ni wasaidizi?
Kila mmoja anatakiwa awajibike vizuri ktk nafasi yake kiutendaji ili kuleta mafanikio kwa timu nzima,Sasa kuna watu wanaitwa washauri na wanalipwa kutokana na kodi zetu ,sasa wao wamecheza vipi kwenye hizo nafasi zao ili kufanikisha jukumu zima la kukuza uchumi wetu.
 
Mwanauchumi huyu tangu ahitimu hajaufanyia kazi wala kupitia tena Vitabu na kuutekeleza kivitendo.Lakini washauri Je?Wanamsaidije kwenye kuleta ufanisi?

wasaidizi ni vitendea kazi tu!....kama vinafaa utavitumia na kunufaika...kama sivyo,basi,unaviacha na kutumia viwezavyo!.

wakati mwingine...mtumiaji huamua kutotumia hiki au kile kwa utashi na uelewa wake!.

wakati mwingine...huwezi kujua una jembe mpaka usikie njaa[ukatafute mihogo na usiipate]na kuona umuhimu wa kulima mihogo!ili kesho kutwa uinywee chai...tartiiibu!.
 
Kila mmoja anatakiwa awajibike vizuri ktk nafasi yake kiutendaji ili kuleta mafanikio kwa timu nzima,Sasa kuna watu wanaitwa washauri na wanalipwa kutokana na kodi zetu ,sasa wao wamecheza vipi kwenye hizo nafasi zao ili kufanikisha jukumu zima la kukuza uchumi wetu.

kama ulivyosema....wao ni washauri....na hivyo kazi yao hushia hapo!full stop!.

sasa,kutenda....hutokana na maamuzi[kiongozi ndio hufanya haya]halafu watendaji watekeleze!.
 
wasaidizi ni vitendea kazi tu!....kama vinafaa utavitumia na kunufaika...kama sivyo,basi,unaviacha na kutumia viwezavyo!.!.
Sasa kwake Mh. Rais ni lipi linamuhusu ni vitendea kazi kufaa au kutofaa?Kama vinafaa amezitumiaje na kama havifai amevishughulikiaje?
wakati mwingine...mtumiaji huamua kutotumia hiki au kile kwa utashi na uelewa wake!.QUOTE]
Hili nalo kwa Mh. Rais amesimamia upande gani?
 
Sasa kwake Mh. Rais ni lipi linamuhusu ni vitendea kazi kufaa au kutofaa?Kama vinafaa amezitumiaje na kama havifai amevishughulikiaje?
wakati mwingine...mtumiaji huamua kutotumia hiki au kile kwa utashi na uelewa wake!.QUOTE]
Hili nalo kwa Mh. Rais amesimamia upande gani?

mjomba!

hapo nilikuwa nayawezesha maswali yako yawe rahisi zaidi kujibika...si na hao wasaidizi tu,bali pia na wanajumuiya!

bado nafanya tafiti yangu....labda itatanguliwa na majibu ya wengine!
 
Kama timu inafungwa kila siku? Je, dawa yake ni nini?
 
Watanzania lazima tuangalie sana. Sasa hivi katika nchi yetu kuna hatari ya mamilioni ya watu kukata tamaa na kupoteza matumaini. Endapo tutafikia mahali (au kama tayari tumeshafikia) ambapo wananchi wa nchi hii watakata tamaa ya uongozi wao na kuamua "kila mtu na lwake" basi tujue kabisa hatima ya nchi yetu iko matatani. Picha ya watoto wa shule ya msingi, je hawa wakikata tamaa, Taifa lina hatima gani? Je Rais Kikwete anaweza kuturudishia matumaini kwa kizazi cha sasa na kijacho?

sikiliza maoni yangu na ya kwako yanakaribishwa: http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Kuna katabia ambako naona kanaanza kuota mzizi ambapo kila jambo hata dogo kiasi gani watu wanakimbilia kwa Rais! Wanafunzi wanataka nyongeza wanakimbilia kwa Rais, Pesa zinagawanywa vibaya, wanakimbilia kwa Rais, Kuna msongamano wa magari dar, wanakimbilia kwa Rais, Timu ya Taifa inaboronga; wanakimbilia kwa Rais, wameachishwa wafanyakazi TRC; wanakimbilia kwa Rais!!

Hivi huu mtindo wa kumfanya Kikwete "mwenye uwezo wote, anayejua yote, na mwenye nguvu zote" utakoma lini? Kwanini tumefikia mahali kwamba hata jambo dogo kiasi gani watu wanataka Rais aingilie kati? Kama Rais angetaka kufanya kila jambo yeye mwenyewe si asingewateua wasaidizi wake? Na Rais Kikwete mwenyewe aanze kukataa vimajukumu visivyo na kichwa wala miguu, kama aliowapa dhamana ya kusimamia nafasi husika hawawezi hadi iwe kama "punde isipokuwa kwa mijeredi" wakati umefika kwa Rais kuwatema na kuwaweka watu wanaoweza kufanya kazi zao bila kusubiri "maelekezo toka Ikulu"!!!

Hii sasa inakera, inaudhi, na inasononesha!! Kikwete hawezi kufanya kila kitu na asijaribu kufanya kila kitu mwisho tutajikuta tunamkaribisha Rais nyumbani kutuamulia mambo yetu ya chumbani kisa kuna kiongozi ana "ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya"!
 
Kama atawasimamia vizuri mawaziri wake haya yasingemkuta.

kama waziri wa elimu ya juu anaboronga amtimue kabla hakujaharibika huko mavyuoni, kama waziri wa miundo mbinu atatekeleza wajibu wake huko TRC tusingesikia vilio. Kama Tamisemi watasimamia vizuri "mabilioni ya Kikwete" hakutakuwa na malalamiko. Kama Mayor na watendaji watajipanga vizuri na kuleta m-badala wa "vipanya" city centre msongamano utakwisha.

Kwa kushindwa kuyasimamia haya, yeye na msanii wake EL ndio maana kutwa kucha watu wanakimbilia kwa JK
 
Huo ndio utaratibu wa tanzania na wala haukuanza jana upo miaka ndenda rudi.Watawala wetu wameshindwa kabisa kuachia madaraka kwa watendaji kwa kuhisi kuwa wao wataonekana sio wachapakazi wakati hakuna wanalolifanya.
Kutokana na tabia hii ndio utaona hata kunapotokea ubadhirifu wa pesa hakuna hatua zinazo chukuliwa kwa sababu waliousika ndio hao hao viongozi kwa hiyo hapa ndipo ilipoanzia kitu kulindana.lakini kama kila mfanyakazi angepewa madaraka kamili na kufanya kazi kwa kufuata taratibu zilizopo tugeweza kupiga hatua.
 
Kwa upande mmoja namlaumu Jeikei kwa hilo. He has delegated powers to other watendaji but went ahead and behave like they dont exist; kwenye kila jambo msemaji yeye..whats the use of having those people around if you do everthing..Suala la michezo kalitaka mwenyewe..kaweka wizara ya michezo na waziri yupo, lakini yeye kawa msemaji wa mpira hata nje akiomba makocha, sasa waziri afanye nini, na tukishindwa mechi yeye ando wa kumuuliza.
Na kuwa-entertain wanaompelekea malalamiko nako kunachangia, he should be firm. (ingawa sio utamaduni wetu maana huko nyuma raisi aliwahi kufungua kijiwe pale Lumumba kila mwezi kusikiliza kero- yaaani hata kesi ya kuku akapelekewa!)
On the other hand, watu wanakosa pa kukimbilia. Kwa administrative structure ya TZ hutegemei mwananchi akose pa kwenda hadi amlilie raisi; there are so many authorities (na ndio maana sirikali ina matumizi ya kutisha)..But who cares...ndo maana kila kilio ni kwake..this is how i see it
 
Mmesahau anaitwa au kufaahamika kama MTU WA WATU thats why they have to run to him.It would be nice to see that he really meant it when he said he didn't want to see or hear people only praise him.Unafikie kibao Bongo.
 
sasa ataweza au hajawahi kusikia watu wanapomsusia mkubwa kazi! Micromanagement haifai kwa Rais vinginevyo waliochini watakuwa wanakaa na kuanza kuwaambia raia "nendeni kashtakini kwa Rais", na kwa vile Rais hayuko tayari kumwajibisha mtu kwa uzembe, uvivu, ubadhirifu, ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi n.k basi hakuna kitachotokea. Matokeo yake, Rais atapata ugonjwa wa moyo usio wa lazima (puh! Mungu aepushie mbali)! lakini mamo mengine siyo ya lazima. Kuna siku nchi yetu itapatwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, Rais atachanganyikiwa. Kama amewaamini watu na kuwapa nafasi basi awaachie wafanye kazi!

Huu mtindo wa kusubiri "ikulu" iseme ni mtindo wa nchi ya wagoigoi!! Matokeo yake ni haya "Bilioni za Kikwete zinatolewa bila ya Masharti" mara "hell no, kuna masharti" , "masharti, masharti gani?"!! Ndiyo haya haya ya "tutadai fedha zetu toka serikali ya Uingereza", "fedha fedha gani?",!!
 
ya kwetu ndio hiyo wanzungu wanaita nanny state; viongozi wakiongea ni kama vile wanaweza kufanya kila kitu. Ni kama vile wananchi tukae tu, tusubiri matunda. Ndio shida ya kupenda sifa kupita kiasi.

Watu wanaacha kufanya kazi mashambani, kuzibua vyoo, n.k., wanaenda kwa Kiwete wanamlilia naye anawaambia, tatizo lenu la ajira nimelisikia, nitalishughulikia.Makofi wawa, magazeti kesho yanaandika, JK kiboko! What do you expect!
 
Read this, an experience from Nyerere's son.


A Letter From Butiama:

Presidents and their Assistants
G. Madaraka Nyerere
Sunday News; Sunday,April 08, 2007 @00:05



IN a novel whose leading character is the president of a powerful country, the president, caught in a crisis and feeling helpless to come up with a solution, realizes his predicament: the president is expected to have an answer to every problem, from the trivial to crises.

Ordinary citizens can sit on a problem while weighing alternative solutions. A president does not always have that luxury. We demand of him immediate solutions for issues affecting our livelihood.

When one of my friends was refused a trading licence by a corrupt official he asked me to use my family connections to grant him an audience with President Nyerere. I was still in my teen years then, and I did not want to disappoint my friend, but I hardly felt that the President was the ideal person to solve his problem.

I took him home and he made his request, but he left disappointed, without the satisfaction of witnessing the corrupt official trembling before the president. Later, Mwalimu Nyerere asked me where I got the unusual idea that he should handle my friend's case. I confessed that I did not think it was a good idea, but I recounted to him the dilemma I faced of preventing a friend's access to his leader, and I believe Mwalimu understood me.

With that experience, over the years I have gained both respect and pity for administrative assistants who constantly face the difficult and thankless task of filtering and deciding who gets to meet the boss and who does not. These assistants are at times some of the most hated people in the country, because it is suspected they have a preference for saying "no" when the boss said "yes."

Recently, I received again one of those unusual requests that only a president could resolve. And, as with the earlier request, it was from one of my friends.

He requested that, should the opportunity arise, I should ask the president to appoint him to an important government administrative position.

I was more than flattered to think that he considered that I could recommend anyone for such an important responsibility. But that was the only positive attitude I had about his request. Because I knew him for many years, I did not believe he had the experience to even dare ask for such an important position. I knew he had some experience as an accountant, but I doubted whether those skills were suited for the presidential appointment.

Besides, it appeared to me that the position he was asking for necessitated constant human contact and demanded excellent humanhandling abilities. I asked myself a few questions.

When did accountants ever spend a time trying to resolve conflicts between pastoralists and farmers? When did accountants convene meetings to discuss the deteriorating security situation in a district? Since independence, how many accountants have made introductory remarks before an address by the president of the United Republic of Tanzania at a public meeting? Each answer I came up with convinced me that my friend had no business thinking he possessed the necessary skills and experience.

If for any reason I found him suitable for the job and an opportunity arose, how would I go about it? "Mr President, I have a friend, with experience in accounting, and he worked as an administrative assistant for a woodworking and furniture workshop. He currently runs a printing business and was wondering whether you could shortlist his name for the post of…."

Presidents and their Assistants I also thought he took our friendship for granted. You do not ask for a presidential appointment through a text message, which is what he did. I had no way of helping him, but I still thought he should have called me to ask for such an important favour.

Although he made such an unusual request I understood his motive, even though it made little sense.

We have a common friend who holds a similar position and so I reasoned he assumed that if our friend has managed, he also can. In my reaction I tried, as much as possible, to apply the skills of a presidential assistant. I replied, by a short text message, and told him that I thought that the post he wanted had already been filled, that I heard that the president was in the process of announcing those appointments soon. Privately, I concluded to myself, he had made one of the most idiotic requests that I had received for years.

I also suspected that my friend probably was drunk when he sent me the message, because I received it at four in the morning. Later that day, I realized what had happened. It was the first day of April. I had become, unwittingly, the perfect April fool.

madarakanyerere@yahoo.com
 
Mheshimiwa rais kwa heshima na taadhima napenda kutoa malalamiko yangu japo yawezekana ni mapema sana kulaumiwa lakini kadiri siku zinavyosogea ndo mambo yanazidi kuwa magumu.

Mheshimiwa lawama kwako isiwe mzigo bali uone kuwa nawakilisha umati wa watanzania walio wengi na ambao wanakosa jinsi ya kufikisha kilio chao kwako.

Muungwana nina machache ya kuanza nayo ambapo naamini wenzangu wanaweza kuongeza mengine lundo na lundo kisha wewe kwa hekima yako ukachambua mchele na pumba.

Nianze na hali ya maisha kwa ufupi:-

MOSI:

Maisha Tanzania yanazidi kuwa magumu kila kukicha. Sisi walalahoi tunazidi kushindwa kuelewa wapi twaelekea na hii kauli mbiu yako ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania itaanza lini kufanya kazi.

Maisha ya watanzania walio wengi yamezidi kudorora na wengi tunaishi chini ya dola moja kwa siku (Nikimaanisha shilingi elfu moja na mia mbili hamsini za kitanzania - Tshs 1,250/=).

Muungwana maisha ya Dar es Salaam yamekuwa magumu zaidi kwani gharama za usafiri hazilingani na vipato vya wakazi wa jiji hili na ndiyo maana usanii na u-kibaka unazidi katika jiji letu hili. Hawa wanaokwapua mikufu, hereni, simu (vilongalonga) n.k maeneo ya mataa si kuwa wanafanya hivi kwa uzembe wao tu; hapana hawajawezeshwa na hali hairuhusu. Kwa matokeo ya kutowezeshwa watu hawa wengine tukijitahidi kununua vilongalonga vyetu vinakwapuliwa na kututia hasara zisizotarajiwa!

Mheshimiwa ni kuwa nauli za jiji la Dar es Salaam na kwingineko (daladala) si kubwa na tunashukuru kwa hilo; lakini kwa namna ambayo najua wewe binafsi huijui ni kuwa ukipanda daladala linatangaza nusu safari kwa mia 3 na baada ya kufika eneo lililotangazwa basi ujue litadai linaenda service; wenye mamlaka husika wamelalamikiwa na hawajali na yaelekea nao wana vipanya vyao barabarani. Masikini kama mie nani anitetee kama si SUMATRA???

Mheshimiwa sijui utaendelea kutoa maonyo hadi lini? Hawa kwanini hawawajibishwi? Kwanini kabla yako kulikuwa na sheria ya Level Seat kwenye daladala na ikawezekana na ulipoingia mamlaka husika wakiwemo askari wa usalama barabarani wakakaa kimya na kuacha usafiri Dar es Salaam uwe kero kiasi hiki?

PILI:

Muungwana kuna jambo moja ambalo najua aidha umedharau au hukujua kuwa lina athari kiasi gani kwa raia wako uliowaahidi MAISHA BORA.

Mishahara! Mheshimiwa niliposikia kutokea kuongezwa kwa viwango vya mishahara kwa watumishi wa serikali nikahisi huenda kwakuwa asilimia kubwa ya watanzania wameajiriwa na sekta binafsi ungefikiria upande huu. Mzee ulikaa kimya na sasa umma wa watanzania umekuwa umasikini unaoendelea kukithiri. Sipingi watumishi wa serikali kuongezwa viwango vya mishahara yao lakini ukumbuke kuwa hata hawa wanaofanya kazi kupitia sekta binafsi nao wanalitumikia taifa tena kwa kutumikishwa na wawekezaji ambao kuna uwezekano hakuna scale ya mishahara mliyowapa kiasi wanalipa wanavyojisikia! Usitarajie maisha bora kwa kila mtanzania kwa mtindo huu!

Asilimia inayokatwa kwenye mishahara ya Tanzania (PAYE) sijui kama ipo katika mataifa yote vilevile. Ni kubwa sana na mfanyakazi hata hana raha na kazi yake! Fikiria mwenye mshahara wa milioni mbili (Tshs 2,000,000/=) as gross anakatwa Tshs 537,500/= kwa mwezi! Kodi hii hata mfanyabiashara mwenye kipato sawa na hiki hakatwi. Nini kosa la mfanyakazi??? Hapa Muungwana nako unafumba macho ukiahidi maisha bora kwa kila mtanzania? Binafsi nakosa uzalendo kwa sasa hadi nafikiria kwenda ng'ambo ambako nimehakikishiwa mshahara mzuri, usafiri na malazi ya kueleweka.

TATU:

Maisha bora bila malazi bora NI NDOTO ZA ALINACHA!
Mheshimiwa niliwahi kuandaa proposal flani ajili ya serikali na nikatoa mawazo juu ya nani watadhamini project yenyewe ili watanzania wanufaike na hata wengine niliwaandikia wakanijibu kuwa ni wazo zuri na kwamba wako tayari ku-finance lakini najua kuna uwezekano mkubwa kuwa proposal yenyewe iliishia mikononi mwa kina flani! Ama uliipata ukaona imekaa vibaya? Nilisubiria kuitwa ili nitoe maelezo ya ziada kama yanahitajika lakini hakuna kilichotokea na sasa almost miezi 6 imepita. Nilichokifanya kilikuwa ni kuonyesha uzalendo wangu na nilifanya BURE ili kutoa mchango wangu kwa taifa japo kuna uwezekano ningenufaika baadae (kama ningefikiriwa).

Najua si mimi pekee mwenye kuwa na wazo mbadala kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna wengine wameleta proposal zao na zikaishia kapuni!

Muungwana kitendo cha kuuzia watanzania viwanja na kuwaacha wasiokuwa na uwezo waendelee kulundikana Magomeni, Manzese, Tandale n.k badala ya maeneo haya kutumika kupanua jiji na wananchi hawa kujengewa Estates zikiwa kamili na miundombinu ya maji, umeme na barabara ni bure!

Wenye hela zao wanazidi kununua ardhi huku wakiwatumia wenye njaa wadai ni vyao! Muungwana watanzania wenye uwezo wa kujenga nyumba ni wachache sana na ninachoamini ni kuwa ardhi ya kuwajengea wananchi Low cost houses ipo ya kutosha na wafadhili wanaweza kusaidia katika hili!

NNE:

Muungwana nina mengi lakini nahisi hii inaweza kuwa MAKALA badala ya dhamira ya kuijadili, nitaendelea na NNE pale nikipata wenye mitizamo tofauti nami au wenye mitizamo sawa na wangu.

Sikupingi katika utendaji bali naomba uniruhusu kusema kuwa UNA MAPUNGUFU ambayo naamini kuwa muda bado unaruhusu kuyabadili na yakabadilika. Rafiki wa kweli ni anayekwambia ubovu wako ili ujirekebishe. Haya nayalenga kwako kwakuwa mamlaka husika hazibebi misalaba yake ipasavyo!
 
Back
Top Bottom