- Thread starter
- #61
Naomba kwa anaefaham huu mti unaitwaje kwa kiswahili aniambie..
View attachment 252429View attachment 252430
Mtunda ama mvinyo.
Hapana mzingifuri na huu ni tofauti
Huu hapa ndio mzingifuri View attachment 252560View attachment 252561
​Mnyonyo na Mbarika yote ni majina yake.
Nyonyo ndo mbarika? Au ni vitu viwili Tofauti?
Mbarika kwa kiingereza ni castor au sio?
Asante kwa sahihisho.
Haswa, kwetu unguja mjini twauita mbarika. Na hizo tunda zake tunaziita mbarika nyonyo. Kama hupati choo unazitafuna kdg, niskilizie huko kuharisha kwake. Unaweza ukabebwa.
Majani yake mazuri sana kwa kukandia.
Mmmmh sijui matumizi ayo ndio nakuskia wewe
Mbalika ni jina la lugha za asili hasa kimwela
Kwetu upareni ni m-bono na mafuta yake mbono. Tulivyokuwa wadogo kila baada ya miezi 3 tulikuwa tunapewa ili kusafisha tumbo kama kuna minyoo nk. yana harufu mbaya kweli, tulikuwa tunachanganyiwa kwenye chai. Utalia hata masaa kumi lakini sharti unywe! Ni dawa nzuri sana ila harufu... Huwa siikosinyumbani lakini hadi leo siku nikiinywa nitahangaika na kikombe weee huku nimejifungia chumbani watoto wasinione...